Polisi wa barabarani na weledi wao.

Polisi wa barabarani na weledi wao.

Asante sana kaka. Umenifumbua macho. Ndio maana nilikuwa napata mashaka sana juu ya weledi wake. Kama mtu kaweza kuandika hii lugha namna hii, inawezekana vipi ashindwe kutofautisha!!!. Kumbe ni mambo ya ku-click. Hiyo pia ime-explain jambo jingine ambalo sikulitaja kwenye andiko langu. Kosa ambalo nilisimamishwa halina uhusiano kabisa na hayo ya helmet na mkanda.
Yawezekana Kosa langu halipo kwenye system hivyo akaamuwa kuchagua Kosa lolote. Bado kuna shida.
Nimecheka Sana ,Polisi Ni janga Sana ,Ni sawa kwenda mahakamani ukiamini umeshtakiwa kwa wizi wa kuku ghafla unasomewa kesi ya uhujumu uchumi 😂😂lazima uhamaki na usipo kuwa na wakili mkojo huo unakuja kugonga kwenye nunda ya sanawari😂..

Polisi na Mpwayungu Ni kitu kimoja, enewei ... Huku kwetu wanaacha geti halafu wanakwenda kukaa porini Kama Nyani..... Enewei katika Taasisi isiyopokea rushwa Tz Ni polisi Tu
 
Kwa maelezo yako hayo, unadhani hapo mtenda kosa kakosea lipi kati ya hayo mawili?

Shuleni hua tunaenda kufanya nini hasa?
Upo sahihi, ikiwa mtafikishana mahakamani itabidi askari aeleze ni kosa lipi kati ya hayo lilifanywa na huyo dereva. Ila sasa kurahisisha uelewa hebu angalia makosa yalivyoandikwa katika Police Form No. 101 (PF. 101) na hayo ndiyo yamehamishiwa katika POS hivyohivyo yalivyo. PF 101 inapatikana kwenye PGO
 

Attachments

  • FB_IMG_1677997718335.jpg
    FB_IMG_1677997718335.jpg
    108.2 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1677997673508.jpg
    FB_IMG_1677997673508.jpg
    77.2 KB · Views: 2
Upo sahihi, ikiwa mtafikishana mahakamani itabidi askari aeleze ni kosa lipi kati ya hayo lilifanywa na huyo dereva. Ila sasa kurahisisha uelewa hebu angalia makosa yalivyoandikwa katika Police Form No. 101 (PF. 101) na hayo ndiyo yamehamishiwa katika POS hivyohivyo yalivyo. PF 101 inapatikana kwenye PGO

Duh hii hatari sana!
 
Asante sana kaka. Umenifumbua macho. Ndio maana nilikuwa napata mashaka sana juu ya weledi wake. Kama mtu kaweza kuandika hii lugha namna hii, inawezekana vipi ashindwe kutofautisha!!!. Kumbe ni mambo ya ku-click. Hiyo pia ime-explain jambo jingine ambalo sikulitaja kwenye andiko langu.
Kosa ambalo nilisimamishwa halina uhusiano kabisa na hayo ya helmet na mkanda, haswa ndiyo kitu kilichonikera zaidi.
Yawezekana Kosa langu halipo kwenye system hivyo akaamuwa kuchagua Kosa lolote. Nikisema nimesingiziwa Kosa nitakuwa nimekosea?? Bado kuna shida.
Kubambikia wanafanya sana. Kosa linaweza kuwa lipo kwenye system lakini hujalifanya na akakuandikia. Bahati mbaya hizi POS hazitoi nafasi ya kukataa kosa yaani ukiandikiwa maana yake ulipe au uende kulalamika kwa RTO ambako nako una nafasi ndogo ya kusaidiwa. Wakati wa kutumia fomu ya karatasi mtu ulikuwa na option ya kukataa kosa na ufikishwe mahakamani, sasa hivi hakuna na polisi hawataki kupelekana mahakamani, wanakulipua tu kosa ulipe faini.

Hapa panatakiwa kurekebishwa, maana walichofanya ni kuwa polisi wamekuwa juu ya sheria na wanafanya kazi ya mahakama kutia watu hatiani, kitu ambacho kisheria hakijakaa sawa.
 
View attachment 2537627
Habari zenu wana jamii. Leo nimeona tuongeee kidogo kuhusu hawa askari wetu wa úsalama barabarani. Ukiangalia hicho kiambatanisho hapo juu, hilo ni Kosa la barabarani ambalo askari amemuandikia dereva. Japo kuwa hilo Kosa inaonekana ni la kujitungia tu, lakini shaka yangu si juu ya hilo. Kinachonisikitisha ni weledi na namna ya kufikiri ya huyu askari wa barabarani. Kumbuka huyu amepewa dhamana ya kusimamia sheria za barabarani na kutupunguzia kero watumiaji wa hizi barabara. Kwa kichwa cha huyu askari, hakuna msaada wowote ama tija kwetu sisi au wateja wake. Ameandika kwamba Kosa ni "kushindwa kufunga mkanda wa úsalama" au "kushindwa kuvaa kofia ya úsalama". Hapa sijui wana jamii mnaelewa nini. Yawezekana mimi ni huu uzee ndio unanifanya nisielewe. Hayo makosa yana asili ya gari na pikipiki na haiwezekani mtu kuwa na gari na kufanya hayo makosa mawili. Ni wazi aliamuwa kutunga tu. Nina uhakika anajua haya ni makosa ya vyombo viwili tofauti, lakini bado akaamuwa kuandika. Hapo ndipo ninapotia mashaka sana juu ya jeshi letu la police.
Kama nilivyosema awali, kwa police kuamua tu kutunga Kosa hainisikitishi sana. Kinachotia hofu na simanzi ni weledi na mawazo ya huyu askari wakati anaandika hili Kosa na adhabu yake. Aliandika akijua si kweli lakini anaamini huyu mtanzania atalipa tu.
Kama ni hivyo ndugu zangu, kuna shida kubwa katikati ya hili jeshi letu la úsalama barabarani. Shida ya kimfumo, weledi, na maadili. Kuna haja ya kuliangalia upya hili jeshi. Jeshi haliwezi kupata ama kuwa na tija iwayoyote kutoka kwa askari wenye mtazamo na akili kama hizi. Watanzania wengi hatupendi usumbufu, kwa tabia yetu hiyo police kama hawa na wengine wengi huamua kututumia, ama kwa faida yao au kwa ujinga tu na kuridhisha kiburi chao.
Binafsi katika pilika zangu za kusaka tonge, huwa natumia muda mwingi nikiwa na raia wa kigeni. Ninapokutana na maafisa wa serekali nikiwa na hawa raia wa nje, huwa naipata wakati mgumu sana kuanzia kuitetea serekali yetu kwa hawa wageni. Yaani ni lazima mtu wa serekali afanye kituko cha kipumbavu tu. Huwa sependi kukubali serekali yetu ionekane ya kijinga kwa wageni. Basi naanza kujitutumua na kiingereza changu cha kuungaunga. Jamani mnatuchosha sana.
Kwa Kosa kama hilo hapo juu naanzaje kulitetea jeshi letu!!! Hapo pana tatizo kubwa la kimfumo, weledi, na maadili. Lakini endapo atatokea kiongozi wa jeshi kuelezea hilo Kosa, a naweza akaja na maelezo mepesi sana kiasi kwamba unaweza dhani muandishi wa hiyo fine na huyo kiongozi wa jeshi, ni mtu mmoja.

Wakatabahu
Infopaedia
Kuna siku jamaa alitaka kuniandika kisa mtoto wa miezi-11 hajafunga mkanda, nikamwambia MFUNGE MKANDA ukimtosha niandikie
 
Kitu kingine ambacho kina shida ni uelewa wa alama za barabara na namna ya kutafsiri.

Kuna siku nilikuwa Mbeya, tulisimama getini pa shule ya Aggrey kumshusha mwanafunzi, mita 100 mbele askari akatusimamisha na kutuambia kuwa tumevunja sheria ya barabara kwa kusimama mahali pasiporuhusiwa. Tukamuuliza akama ya kutuzuia kusimama iko wapi, akatuonesha upande wa pili wa barabara (uelekeo wa uyole kwenda mbeya mjini) kuna alama imechorwa kienyeji (ni kama temporary sign). Kibao kimechorwa basi halafu kuna ile alama ya kulikata katikati, tulimwambia sasa sisi tunatoka mjini tunaionaje hiyo alama wakati haipo upande wetu?? Pili tukamwambia, akama ikiwa na aina ya gari specific maana yake inahusu gari hilo tu, iweje useme inatumika kote? Kwa alama hiyo maana yake mabasi ndiyo yamezuiwa na sio magari mengine, akawa mkali tukabishana na akatuandikia faini. Hatukukubali, tukatafuta namba ya DTO akasema anatuma mtu aje, ila tutapoteza muda kumsubiri ni bora tulipe tu faini. Tukaondoka zetu.

Sasa tukiwa Ilembula nikapiga picha ya vibao vinavyohusu gari maalumu. Pichani utaona kuna stendi ya mabasi tu na pia kuna stendi kwa ajili ya malori, maana yake hizo zipo kwa gari maalum pichani. Ukizoom utaona mbele kuna stendi ya malori
 

Attachments

  • 20210613_153814.jpg
    20210613_153814.jpg
    596.3 KB · Views: 2
Kosa ambalo nilisimamishwa halina uhusiano kabisa na hayo ya helmet na mkanda, haswa ndiyo kitu kilichonikera zaidi.
Mdau hebu weka bayana kosa walilokusimisha kwalo na kuishia kukuhukumu kwa kosa lingine.

Kuweka wazi huu uozo wa hawa viumbe kutapunguza shombo zao.
 
Inawezekana kwenye mashine yao kuna changua A au B yeye akachagua yote...
 
Mdau hebu weka bayana kosa walilokusimisha kwalo na kuishia kukuhukumu kwa kosa lingine.

Kuweka wazi huu uozo wa hawa viumbe kutapunguza shombo zao.
Ilikuwa hiviii....... Niko njiani naendesha. Mbele nikakutana na daladala aina ya coaster. Ile daladala ilikuwa njiani inaenda huku ikitafuta abiria. Nadhani unajua Mwendo wa hawa jamaa wakiwa barabarani huku wanavizia abiria, ni taratibu sana. Nikaenda nae hivyo hivyo. Na hii barabara katikati kuna mstari siruhusiwi kumpita. Nikawa namfuata huku napiga honi akisimama barabarani. Mwisho uvumilivu ukanishinda Nikasema nimpite. Ile nampita, police hawa hapa. Akanisimamisha akaniambia Kosa langu la kupita sehemu isiyoruhusiwa. Sikubisha ila Nikamuuliza..... Unaona inachokifanya ile daladala, bahati nzuri ile coaster ilikuwa mbele inaendelea taratibu. Police akanijibu....." Mtu kama huyo ni kumpuuza tu" . Dah! Yaani niliishiwa pose. Akaniomba leseni, akaandika kwenye kitabu chake. Halafu akaniambia..... "mtandao umecheza, ukirudi nitakuandikia Kosa lako*. Nikaondoka, kwenda kuangalia ili nilipe si ndio nakutana na mambo ya mkanda na helmet. Nilichoka kabisa.
Hapo kama ni wewe, mawazo jumuishi yatakuwaje.???
Hilo ndio tukio lenyewe.
 
Sijui wanaofanya usaili kabla ya kuajiri hawa jamaa wanatumia vigezo gani.
 
Back
Top Bottom