Polisi wa China wapata umaarufu tena kwenye mitandao ya kimataifa ya kijamii

Polisi wa China wapata umaarufu tena kwenye mitandao ya kimataifa ya kijamii

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
无标题.jpg
Video ya afisa wa polisi maalum wa China akiwasaidia watalii kupiga picha hivi karibuni imesambaa kwenye mitandao ya kimataifa ya kijamii. Jambo hili lilitokea wakati wa Sikukuu ya Kitaifa ya China mwaka jana. Wakati huo, Uwanja wa Agosti 1 huko Nanchang ulikuwa umejaa watu, na afisa mmoja wa polisi maalum, akiwa anasimama juu, aliwasaidia watalii kupiga picha mmoja baada ya mwingine. Hakuna mtu aliyetarajia kwamba video hii ingepakiwa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ya nje ya nchi, na kuzua mjadala kuhusu “jinsi polisi wanavyopaswa kuwa”.

Kwenye mitandao ya kijamii, mtu anayejiita @KevinCastley aliandika: “Sio polisi wote ni wapumbavu. Baadhi ya polisi ni Wachina”. Maoni haya yalikubaliwa mara 770,000. Mwanamtandao mwingine alisema, “Ukipata fursa ya kusafiri nchini China, unaweza kuwa na imani nao kabisa kwa sababu wao ni polisi wa watu”.

Hii si mara ya kwanza polisi wa China kupata umaarufu mtandaoni. Mwezi Machi mwaka huu, video ya maafisa wa polisi wa China wakiwa wamewaketisha watoto juu ya paa la gari la polisi ili kutazama maonyesho ilisambaa kwenye mitandao ya kimataifa ya kijamii. Katika video hiyo, maafisa wa polisi walikuwa wanaweka watoto mmoja baada ya mwingine juu ya paa la gari la polisi, wakihakikisha wamekaa kwa salama na kutazama maonesho. Watoto walifurahi sana, na maafisa waliwaangalia kwa uvumilivu ili kuwazuia wasianguke, huku pia wakilinda utulivu na usalama. Video hiyo ilisambaa sana mtandaoni. Wengi walitoa maoni kwamba walishangazwa na huruma ya polisi wa China. Baadhi ya wanamtandao wa Marekani walisema kwamba katika nchi zao, watoto hufundishwa tangu umri mdogo kukaa mbali na magari ya polisi, na polisi “hawawezi kufanya jambo kama hilo”.

Kwa nini vitendo hivi vinavyochukuliwa kuwa vya kawaida kwa polisi wa China, vinasababisha mshangao mkubwa miongoni mwa watumiaji wa mtandao duniani?

Tarehe 24, mwezi Januari, mwaka 2026, huko Minneapolis, Minnesota nchini Marekani, Alex Pretty mwenye umri wa miaka 37 alipigwa risasi na kuuawa barabarani na maafisa wa polisi wakati wa maandamano dhidi ya Uhamiaji na Utekelezaji wa Hatua za Forodha. Hili lilikuwa tukio la pili katika jiji hilo ndani ya siku 18 baada ya kesi ya Renee Good ambapo maafisa wa kutekeleza sheria walimpiga risasi na kumwua. Pretty alikuwa mfanyakazi shujaa wa afya wa mstari wa mbele wakati wa janga la COVID-19.

Katika jiji hilo hilo, tarehe 25 mwezi Mei, mwaka 2020, George Floyd alikamatwa kwa madai ya kutumia pesa bandia. Afisa mmoja wa polisi alipiga magoti shingoni mwake kwa zaidi ya dakika nane, ambapo Floyd alisikika akilalamika akisema, “Siwezi kupumua”, kabla ya kupoteza fahamu na kufa katika chumba cha dharura cha hospitali.

Kuanzia Floyd hadi Pretti, ukatili wa polisi nchini Marekani unaonekana kama “laana” isiyoepukika nchini Marekani.

Wakati huohuo, Ripoti ya Usalama wa Dunia 2025 iliyotolewa na Shirika la Gallup inaonesha kwamba China ni mojawapo ya nchi salama zaidi duniani. Viashiria mbalimbali vya usalama wa jamii vya China vinaongoza nchi zote kuu za Magharibi. Nchini China, zaidi ya asilimia 99 ya maafisa wa polisi hawabeba bastola wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Usalama wa China ni matunda ya kazi hodari za polisi, na pia unatokana na utawala wa China ambao unazingatia zaidi watu.
 
Kipo kipindi tulikuwa na Imani na polisi had tunaomba lifti magari ya polisi tukienda shule. Not any more , taasisi hii siku hizi imesheheni mbwa na mbwa na mbwa halisi.
 
Kipo kipindi tulikuwa na Imani na polisi had tunaomba lifti magari ya polisi tukienda shule. Not any more , taasisi hii siku hizi imesheheni mbwa na mbwa na mbwa halisi.

Taasis iliharibika ba ya kushikana na wanasiasa
 
Back
Top Bottom