Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio majukumu yao hayo sasaTutajie maana ya hilo neno Majukumu ya Kila siku.
Polisi wamejiandaa kwa vurugu dhidi ya wananchi hapo 23 Septemba
21 September 2024
Ulinzi umeimarishwa jijini Dar es Salaam huku magari ya polisi yakionekana yakizunguka kuweka ukuta wa kufikirika
View: https://m.youtube.com/watch?v=IJgCHuVI4dA
Tanzania ni nchi ya kipekee kwa kutoonekana askari polisi kuzagaa ambapo nchi zingine kama Ethiopia, Kenya n.k ni kawaida huko kuona hali hiyo kila siku huku vizuizi vya mageti ya misumari kutoboa matairi hukweka na polisi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam leo 21 September 2024 yamejaa askari wa Jeshi la Polisi, wanaozunguka huku na kule.
TOKA MAKTABA :
Ikulu
Dar es Salaam, Tanzania
View attachment 3101983
20 September 2024 amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye ni Rais Samia Hassan alipowaita IGP Camilius Wambura na viongozi wakuu waandamizi wa jeshi la Polisi katika Ikulu ya Dar es Salaam.
View attachment 3101984
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Samia S. Hassan akiwa ktk picha ya pamoja, mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo kumaliza mkutano uliyo fanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 20 Septemba, 2024.
Nakwambia utakuja kuniambia jumatatu hakuna maandamano yoyote yataofanikiwa zaidi ya vurugu uchwara na watadhibitiwa mapema sanaDamu zitakazomwagwa na polisi hawa Jumatatu ndiyo kaburi la CCM. Rais ameingizwa chaka kiboya sana
Mkwala wote huo wakati Maandamano ni ya AMANI.Wameamua kuwafuata kabisa wateja wao.
Amani wapi wewe asilimia 90 wanakua tayari wameshaharibu ubongo kwa kemikali mbali mbali.Mkwala wote huo wakati Maandamano ni ya AMANI.
nguvu ya umma wanaisikia tu hawajawahi kuishuhudia ila siku moja wataishuhudia
Mtawala akiona ana mamlaka ya uhai ya wanachi ndio shida inaanzia hapo
Raisi kajikuta kiziwi
yanayolalamikiwa na wananchi kachukua uuzaji personal ya kichama badala ya kutafuta suluhu kama jina lake linavojinadi na linavotamkwa
Wanaomshauri kutoa speech ile wameharibu kila kitu speech ya kujaza hamasa na nia ovu kwa wananchi
Chadema wanaweza wasifanikiwe kwenye maandamano vipi kihusu uelewa wa raia ambao wameeanza kuandamana kila mahali Kuhusu kudai haki zao za msingi. Ngorongoro , dar es salaam , Simanjiro na kwingine
Washauri wake hawamtakii mema ipo siku vijana wa kukosa ajira wakiamka ndio balaa zaidi maana hatasaidiwa na polisi kabsa
Anahitaji suluhu zaidi ya polisi ipo siku yake jazba na kiburi alichinacho ipo siku ataona havina muhimu zaidi ya kutafuta suluhu kumbe muda utakua umeenda
Chadema wanaweza wasifanikiwe kuhusu Maandamano yao hayo ambayo wamepanga kuyafanya hapo tarehe 23 Septemba, 2024. Isipokuwa Hakuna kitu kibaya hapa duniani Kama watu (raia) kufanya Maandamano ya Rohoni, hiyo ni hatari Sana kupita kiasi. Mathalani, nchi ya Iran inakabiliwa na kitisho kikubwa Sana cha Maandamano ya namna hii, Watawala wa nchi hiyo wamepiga marufuku kabisa mtu yoyote yule kuandamana kwa wazi Wazi katika nchi hiyo, na wananchi nao wamebuni njia nyingine mbadala ya kuandamana kwa kufanya maandamano ya rohoni ambayo nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na madhara makubwa Sana kutokana na maandamano ya namna hiyo.Nakwambia utakuja kuniambia jumatatu hakuna maandamano yoyote yataofanikiwa zaidi ya vurugu uchwara na watadhibitiwa mapema sana
Kweni haya ni Maandamano ya Amani kwanza ya CHADEMA?.Amani wapi wewe asilimia 90 wanakua tayari wameshaharibu ubongo kwa kemikali mbali mbali.
Katiba na sheria ni zawakoloni watu wanaishi kwa hisani ya Rais tuliondoa mkoloni tukabakiza katiba yake ambayo ndo mkoloni mwenyeweUlinzi umeimarishwa au wameshikwa na kiwewe???
Hata hivyo, Siyo kweli hata kidogo kwamba SSH au JPM ndio chanzo cha kushamiri kwa vitendo vya Utekaji na Mauaji hapa nchini kwa sababu tatizo lililopo siyo JPM wala siyo SSH, Bali tatizo ni kwamba Tanzania kuna Katiba mbaya sana pamoja na Sheria zilizopo ni mbaya sana ambazo pia ni sheria kandamizi.
Aidha, nasisitiza kwamba kutokana na kuwepo kwa janga la vitendo viovu hapa Tanzania, chanzo chake au tatizo siyo JPM wala siyo SSH. Mathalani, JPM tayari ameondoka zake, na SSH naye ipo siku lazima ataondoka, lakini vitendo viovu vya Utejaji, utesaji na Mauaji kamwe havitaondoka, na badala yake vitaendekea kuwepo kwa sababu Katiba na Sheria zinazohalalisha vitendo hivyo viovu kuwepo bado zipo na wala hazijaondolewa kutoka hapa nchini Tanzania.
Nguvu ya Umma itakuja yenyewe tu bila kupitia vyama amini ilo hapo ndo itakua balaahHivyo vitisho ni vya kijinga tu. Siku nguvu ya umma ikiamua, hakutakuwepo na 🐕🦺 wa kuizuia.
Yatawakuta siku moja ya Bangladesh.Watu sijui wakoje.Hivi kwani kuna shida gani,kwa nini wasiachie hao mateka wanaotakiwa na chadema? Hivi kama kweli wana nia njema na nchi,kuna ubaya gani kuwaachia kina soka ? Nasikitika sana.Ccm inatupeleka pabaya .Hiyo ni nguvu ya Chadema.
Sasa kuna siku watakutana na nguvu ya umma.
Nguvu ya Umma itakuja yenyewe tu bila kupitia vyama amini ilo hapo ndo itakua balaah