Polisi wa Kuzuia Fujo wasambazwa jijini Dar: Ni kutangaza hali ya hatari?

Polisi wa Kuzuia Fujo wasambazwa jijini Dar: Ni kutangaza hali ya hatari?

Ni kweli chama dola kongwe kijitokeze kunusuru tunapoelekea kwa CCM kukaza shingo kwa kiburi kutotaka kuongea kwa nia njema na chama cha kisiasa kinachosikilizwa pia kukubaliwa kinawawakilisha sehemu kubwa ya umma wa watanzania .

Umma utapogundua na kuona hata chama wanachokikubali kinachobeba matumaini yao kinasakamwa na kudoofishwa kwa njia za kiuovu na umma ukaamua sasa watachukua mamlaka mikononi mwao kujinusuru kwakuwa tegemeo lao kupitia mfumo rasmi wa kisiasa umeharamishwa kwa chama dola tawala kutumia mbinu chafu.

Basi umma huo unaweza kujichukulia mamlaka mikononi mwake huku hakuna tena viongozi wa kuwatuliza kama kule wakati wa mazishi ya kiongozi wa CHADEMA marehemu Ali Mohamed Kibao mjini Tanga, hali ya nchi itakuwa ngumu na CCM itakuwa hawana chama cha upinzani kukishawishi kupoza hasira za umma.

23 September 2024
Oysterbay Police Station
Mkoa wa Kinondoni
Dar es Salaam, Tanzania

FREEMAN MBOWE, TUNDU LISSU, GODBLESS LEMA USIKU HUU SAA TANO ZA USIKU


View: https://m.youtube.com/watch?v=Eqkw0-iKDDU

Waachiwa usiku huu viongozi wa CHADEMA ambao ni Freeman Mbowe ....
 
21 September 2024

Ulinzi umeimarishwa jijini Dar es Salaam huku magari ya polisi yakionekana yakizunguka kuweka ukuta wa kufikirika


View: https://m.youtube.com/watch?v=IJgCHuVI4dA

Tanzania ni nchi ya kipekee kwa kutoonekana askari polisi kuzagaa ambapo nchi zingine kama Ethiopia, Kenya n.k ni kawaida huko kuona hali hiyo kila siku huku vizuizi vya mageti ya misumari kutoboa matairi hukweka na polisi.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam leo 21 September 2024 yamejaa askari wa Jeshi la Polisi, wanaozunguka huku na kule.

TOKA MAKTABA :
Ikulu
Dar es Salaam, Tanzania

View attachment 3101983
20 September 2024 amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye ni Rais Samia Hassan alipowaita IGP Camilius Wambura na viongozi wakuu waandamizi wa jeshi la Polisi katika Ikulu ya Dar es Salaam.
View attachment 3101984

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Samia S. Hassan akiwa ktk picha ya pamoja, mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo kumaliza mkutano uliyo fanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 20 Septemba, 2024.

Oyy jaribu kutofautisha kati ya Jeshi na vibaraka wa bibi, Jeshi huwezi kuta wanatumika kipuuzi hivyo
 
Back
Top Bottom