Yote haya yanalenga kuwatisha raia ili CCM iendelee kutawala kidhalimu hapa nchini. Very sad indeed.Mfano wa nguvu ya dola inapotumiwa na serikali inayoongozwa na chama dola kongwe kutosikiliza umma na kuamua kuonesha vifaa vilivyonunuliwa na kodi za wananchi kisha kuvitumia kutisha umma
View: https://m.youtube.com/watch?v=oBFPSBNFQz8
Ni kweli chama dola kongwe kijitokeze kunusuru tunapoelekea kwa CCM kukaza shingo kwa kiburi kutotaka kuongea kwa nia njema na chama cha kisiasa kinachosikilizwa pia kukubaliwa kinawawakilisha sehemu kubwa ya umma wa watanzania .
Umma utapogundua na kuona hata chama wanachokikubali kinachobeba matumaini yao kinasakamwa na kudoofishwa kwa njia za kiuovu na umma ukaamua sasa watachukua mamlaka mikononi mwao kujinusuru kwakuwa tegemeo lao kupitia mfumo rasmi wa kisiasa umeharamishwa kwa chama dola tawala kutumia mbinu chafu.
Basi umma huo unaweza kujichukulia mamlaka mikononi mwake huku hakuna tena viongozi wa kuwatuliza kama kule wakati wa mazishi ya kiongozi wa CHADEMA marehemu Ali Mohamed Kibao mjini Tanga, hali ya nchi itakuwa ngumu na CCM itakuwa hawana chama cha upinzani kukishawishi kupoza hasira za umma.
Oyy jaribu kutofautisha kati ya Jeshi na vibaraka wa bibi, Jeshi huwezi kuta wanatumika kipuuzi hivyo21 September 2024
Ulinzi umeimarishwa jijini Dar es Salaam huku magari ya polisi yakionekana yakizunguka kuweka ukuta wa kufikirika
View: https://m.youtube.com/watch?v=IJgCHuVI4dA
Tanzania ni nchi ya kipekee kwa kutoonekana askari polisi kuzagaa ambapo nchi zingine kama Ethiopia, Kenya n.k ni kawaida huko kuona hali hiyo kila siku huku vizuizi vya mageti ya misumari kutoboa matairi hukweka na polisi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam leo 21 September 2024 yamejaa askari wa Jeshi la Polisi, wanaozunguka huku na kule.
TOKA MAKTABA :
Ikulu
Dar es Salaam, Tanzania
View attachment 3101983
20 September 2024 amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye ni Rais Samia Hassan alipowaita IGP Camilius Wambura na viongozi wakuu waandamizi wa jeshi la Polisi katika Ikulu ya Dar es Salaam.
View attachment 3101984
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Samia S. Hassan akiwa ktk picha ya pamoja, mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo kumaliza mkutano uliyo fanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 20 Septemba, 2024.