Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Polisi wa tanzania tumesoma na kusikia malalamiko mengi sana juu yao, mpaka inakuwa vigumu kuanza kutafuta mema yao.

Tunaona kuwa Polisi ndiyo wamekuwa chimbuko la rushwa, imefikia mpaka kuna msemo mitaani "kuingia kwa pesa, kutoka kwa pesa"

katika mema yao machache ni pale tunapoona kwenye vyombo vya habari wakijitangaza wao wenyewe kukamata majambazi na wezi, au, wameuwa jambazi fulani.

Nakumbuka sisi tulivyokuwa utotoni, miaka ya mwanzo 60s, tulibahatika kuliona jeshi la Polisi lililosheheni Wazungu, Wahindi, Waarabu na Waafrika. Na kila mtoto alitamani akikuwa awe polisi.

Polisi kilikuwa siyo chombo cha kutishia watoto, kila mtoto akipenda na kutamani awe polisi au kama polisi. Hivi sasa polisi imekuwa chombo cha kutishia watoto, ukimwambia mtoto "polisi huyo" basi mtoto anaweza kukulilia utafikiri kamuona ziraili mtowa roho za watu.

Tumefeli wapi na jeshi letu la Polisi?

Mtazamo wangu; Jeshi la polisi lilianza kufeli zamani sana, lilianza kufeli lilipoanza kutumiwa na wanasiasa kukandamiza wananchi wafanye watakavyo wao kwa nguvu au kwa hiyari. Chanzo nnachokikumbuka mimi ni vijiji vya ujamaa, watu walipoanzwa kuhamishwa makazi yao ya asili na kupelekwa vijiji vya ujamaa, jeshi la polisi likaanza kutumika kuwahamisha watu kwa nguvu na kuwapakia kwenye "makarandinga" kuwahamisha kutoka makazi yao ya asili na kwenda kuwatupa maporini waanzishe makazi mapya yaliyoitwa "vijiji vya ujamaa".

Kuanzia kipindi hicho serikali zote, mpaka leo hii, hazijaacha kuitumia polisi kama chombo chao cha kuhakikisha walitakalo wanasiasa ndilo wanalifanya polisi.

Tatizo liko wapi? Jee ni wakati siasa zikaachanishwa na kuendesha serikali? Serikali ibaki kama serikali na siasa zibaki kama siasa?

kinachotakiwa ni tafakuri ya kina, maji yakimwagika hayazoleki, lakini tunaweza kupiga deki na kuyakausha na kuchota mengine.

Wewe unaonaje? Umefikia wakati tuwe na Polisi binafsi?
 
74cnl2nohth31.jpg
 
Ukiona mwanamme anajidai kujibaraguza namna hiyo majukwaa ya siasa elewa kuwa tumeshakuelewa wewe ni mpapai tu au huna nguvu za kiume. Mwanamme wa kweli anaongea kijinga namna hiyo?

Kwa kukujuza tu, nenda Kikwete wameshaanza kurudishia mahanisi nguvu za kiume, kama ulikatwa mishipa wakati wakushughulikiwa pale wanairudisha, wametangaza jana.
 
Uzuri wa polisi wananjaa sana sana,hii ni fursa kubwa kwa wale watu wa deal chafu kufanya shughuli zao bila shida.
Polisi akiona laki anatetemeka keshawaza konyagi kubwa .
Sasa kwa wananchi walio wengi si majanga hayo?

Kweli nimekuelewa, ni neema kwa wafanya madhambi. Vipi, hilo ni tatizo au si tatizo?
 
Nashauri DP World waje kufundisha polisi wa bandarini, maana Polisi Dubai wanaenda na wakati:

CNN: Hakuna mahali pengine duniani unaweza kusifu gari la polisi na kupiga selfie na dereva. Hakuna mahali pengine duniani ni kwamba gari la polisi linaweza kuwa Bugatti Veyron, Ferrarri FF au Lamborghini Aventador.

Hii ni Dubai, ambapo jeshi la polisi limekabidhiwa cheti na Guinness World Records kwa kuwa na gari la polisi lenye kasi zaidi duniani - Bugatti Veyron -

1690530268313.png

Kinara ya gari hizo ni Veyron, lina kasi ya juu ya 253 mph (407 km / h).

Watoto wa kitajiri walikuwa wanachezea sna polisi, Mfalme wao akasema upuuzi huu, wasicheze tena na polisi, akwashushia vitu vya uhakika, waekoma ubishi.

Siyo kwetu hapa, polisi ukiwapigia simu wanakuuliza pesa ya mafuta!

Chanzo: CNN
 
rekebisha typing errors.
Polisi wengi wana njaa
Hivi polisi analipwa Tsh. ngapi,tuanzie hapo kwanza... tujue,ili serikali ikiwezekana,wawaboreshee mshahara kwanza.Mwenye digrii sijui analipwa laki ngapi,bado sijajua wa form four,ukute wanazidiwa na watumishi wote wa serikali,ndiyomaana umesema wananjaa.
 
Polisi wa tanzania tumesoma na kusikia malalamiko mengi sana juu yao, mpaka inakuwa vigumu kuanza kutafuta mema yao.

Tunaona kuwa Polisi ndiyo wamekuwa chimbuko la rushwa, imefikia mpaka kuna msemo mitaani "kuingia kwa pesa, kutoka kwa pesa"

katika mema yao machache ni pale tunapoona kwenye vyombo vya habari wakijitangaza wao wenyewe kukamata majambazi na wezi, au, wameuwa jambazi fulani.

Nakumbuka sisi tulivyokuwa utotoni, miaka ya mwanzo 60s, tulibahatika kuliona jeshi la Polisi lililosheheni Wazungu, Wahindi, Waarabu na Waafrika. Na kila mtoto alitamani akikuwa awe polisi.

Polisi kilikuwa siyo chombo cha kutishia watoto, kila mtoto akipenda na kutamani awe polisi au kama polisi. Hivi sasa polisi imekuwa chombo cha kutishia watoto, ukimwambia mtoto "polisi huyo" basi mtoto anaweza kukulilia utafikiri kamuona ziraili mtowa roho za watu.

Tumefeli wapi na jeshi letu la Polisi?

Mtazamo wangu; Jeshi la polisi lilianza kufeli zamani sana, lilianza kufeli lilipoanza kutumiwa na wanasiasa kukandamiza wananchi wafanye watakavyo wao kwa nguvu au kwa hiyari. Chanzo nnachokikumbuka mimi ni vijiji vya ujamaa, watu walipoanzwa kuhamishwa makazi yao ya asili na kupelekwa vijiji vya ujamaa, jeshi la polisi likaanza kutumika kuwahamisha watu kwa nguvu na kuwapakia kwenye "makarandinga" kuwahamisha kutoka makazi yao ya asili na kwenda kuwatupa maporini waanzishe makazi mapya yaliyoitwa "vijiji vya ujamaa".

Kuanzia kipindi hicho serikali zote, mpaka leo hii, hazijaacha kuitumia polisi kama chombo chao cha kuhakikisha walitakalo wanasiasa ndilo wanalifanya polisi.

Tatizo liko wapi? Jee ni wakati siasa zikaachanishwa na kuendesha serikali? Serikali ibaki kama serikali na siasa zibaki kama siasa?

kinachotakiwa ni tafakuri ya kina, maji yakimwagika hayazoleki, lakini tunaweza kupiga deki na kuyakausha na kuchota mengine.

Wewe unaonaje? Umefikia wakati tuwe na Polisi binafsi?
Waletwe polisi kutoka dubei
 
Back
Top Bottom