Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Inatisha, sasa mambo kama hayo ndiyo tuyaseme serikali watatusikia tu.

Tupe details tumwandikie Masauni na kopi tutapeleka Ikulu na kwa IGP. Tukikaa kimya na wao wanaona ni kawaida tu.


Polisi wanapofanya vyema tuwape maua yao, na wanapofanya mabaya tuwapakazie mpaka kieleweke.
Tusipoteze wakati tatizo la rushwa katika police force ni la kimfumo!!
Kama viongozi wa serikali wanapokea rushwa wazi wazi na wananchi wanajua; kumuandika barua Masauni atafanya nini? The problem is systemic!
 
Hao sio police ni kundi la majambazi waliojificha kwenye nguo za upolice
 
Nashauri DP World waje kufundisha polisi wa bandarini, maana Polisi Dubai wanaenda na wakati:

CNN: Hakuna mahali pengine duniani unaweza kusifu gari la polisi na kupiga selfie na dereva. Hakuna mahali pengine duniani ni kwamba gari la polisi linaweza kuwa Bugatti Veyron, Ferrarri FF au Lamborghini Aventador.

Hii ni Dubai, ambapo jeshi la polisi limekabidhiwa cheti na Guinness World Records kwa kuwa na gari la polisi lenye kasi zaidi duniani - Bugatti Veyron -


View attachment 2701204


Kinara ya gari hizo ni Veyron, lina kasi ya juu ya 253 mph (407 km / h).

Watoto wa kitajiri walikuwa wanachezea sna polisi, Mfalme wao akasema upuuzi huu, wasicheze tena na polisi, akwashushia vitu vya uhakika, waekoma ubishi.

Siyo kwetu hapa, polisi ukiwapigia simu wanakuuliza pesa ya mafuta!

Chanzo: CNN
Hapa ndo uzi umekamilika.
 
Polisi wa tanzania tumesoma na kusikia malalamiko mengi sana juu yao, mpaka inakuwa vigumu kuanza kutafuta mema yao.

Tunaona kuwa Polisi ndiyo wamekuwa chimbuko la rushwa, imefikia mpaka kuna msemo mitaani "kuingia kwa pesa, kutoka kwa pesa"

katika mema yao machache ni pale tunapoona kwenye vyombo vya habari wakijitangaza wao wenyewe kukamata majambazi na wezi, au, wameuwa jambazi fulani.

Nakumbuka sisi tulivyokuwa utotoni, miaka ya mwanzo 60s, tulibahatika kuliona jeshi la Polisi lililosheheni Wazungu, Wahindi, Waarabu na Waafrika. Na kila mtoto alitamani akikuwa awe polisi.

Polisi kilikuwa siyo chombo cha kutishia watoto, kila mtoto akipenda na kutamani awe polisi au kama polisi. Hivi sasa polisi imekuwa chombo cha kutishia watoto, ukimwambia mtoto "polisi huyo" basi mtoto anaweza kukulilia utafikiri kamuona ziraili mtowa roho za watu.

Tumefeli wapi na jeshi letu la Polisi?


Mtazamo wangu; Jeshi la polisi lilianza kufeli zamani sana, lilianza kufeli lilipoanza kutumiwa na wanasiasa kukandamiza wananchi wafanye watakavyo wao kwa nguvu au kwa hiyari. Chanzo nnachokikumbuka mimi ni vijiji vya ujamaa, watu walipoanzwa kuhamishwa makazi yao ya asili na kupelekwa vijiji vya ujamaa, jeshi la polisi likaanza kutumika kuwahamisha watu kwa nguvu na kuwapakia kwenye "makarandinga" kuwahamisha kutoka makazi yao ya asili na kwenda kuwatupa maporini waanzishe makazi mapya yaliyoitwa "vijiji vya ujamaa".

Kuanzia kipindi hicho serikali zote, mpaka leo hii, hazijaacha kuitumia polisi kama chombo chao cha kuhakikisha walitakalo wanasiasa ndilo wanalifanya polisi.

Tatizo liko wapi? Jee ni wakati siasa zikaachanishwa na kuendesha serikali? Serikali ibaki kama serikali na siasa zibaki kama siasa?

kinachotakiwa ni tafakuri ya kina, maji yakimwagika hayazoleki, lakini tunaweza kupiga deki na kuyakausha na kuchota mengine.

Wewe unaonaje? Umefikia wakati tuwe na Polisi binafsi?
Polisi wengi wala rushwa tu. Ukiwapelekea kesi umedhulumiwa au kutapeliwa basi jiandae kutoa chochote ili kesi yako iende ki haki. La sivyo watahamia upande wa tapeli kukunyima haki.
 
Kweli kabisa, natamani polisi wawe na nidhamu na sifa za polisi waliopo duniani.

Huko ulipopataja Polisi wanakuwa ni kimbilio la jamii na ni washauri wakuu wa jamii inapokosea. Hapa kwetu ni kinyume chake, jamii, inaiogopa polisi. Kwanini?
Siwapendi polisi wa tz, ukienda kituoni na tatizo wanakugeuza fursa. Pia wanaonea sana raia masikini
 
Polisi ni wazuri sana. Wanafanya kazi kubwa ya kuenforce law. Bila polisi hizi sheria tulizonazo ni takataka. Na polisi wanatakiwa kuwa wakali, watu wasio na mchezomchezo.

Wabaya wapo kama ambavyo kuna wabaya kila kona kuanzia marais, wabunge, madaktari, madereva nk.
Ingawa wanatulinda lakini sijawahi kuona polisi mzuri tz likija suala la kesi au ishu yoyote inayokufanya ufike polisi
 
kama walinzi mnao na kampuni tayari,fanyeni mchakato mpate taasisi binafsi za upelelezi sio polisi kamili.
Siyo "fanyeni", tufanye.

Tunaishauri serikali iweke sheria ya kuwa na kampuni za Polisi binafsi, Halafu mashirika makubwa ya serikali yaanze kwa makusudi kabisa kukodisha polisi binafsi, siyo kampuni za ulinzi.

Kama vile shirika la reli, SGR, bandari na mengine mengi tu.


Pia siioni sababu kwanini magereza zisiwepo za mashirika na askari jela binafsi.
 
Ingawa wanatulinda lakini sijawahi kuona polisi mzuri tz likija suala la kesi au ishu yoyote inayokufanya ufike polisi
Ukienda kushitaki kosa, ukishitakiwa kosa.

Jeshi la polisi limekuwa kubwa sana na halijitoshelezi mahitaji yake, linatakiwa lipunguzwe ukubwa kwa kulibinafsisha baadhi ya sehemu ili Polisi waanze kupata malipo mazuri na vifaa vya kisasa.
 
Back
Top Bottom