Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Tusipoteze wakati tatizo la rushwa katika police force ni la kimfumo!!
Kama viongozi wa serikali wanapokea rushwa wazi wazi na wananchi wanajua; kumuandika barua Masauni atafanya nini? The problem is systemic!
 
Hao sio police ni kundi la majambazi waliojificha kwenye nguo za upolice
 
Hapa ndo uzi umekamilika.
 
Umeandika kana kwamba wote tunauelewa juu ya hao polisi binafsi.
 
Polisi wengi wala rushwa tu. Ukiwapelekea kesi umedhulumiwa au kutapeliwa basi jiandae kutoa chochote ili kesi yako iende ki haki. La sivyo watahamia upande wa tapeli kukunyima haki.
 
Kweli kabisa, natamani polisi wawe na nidhamu na sifa za polisi waliopo duniani.

Huko ulipopataja Polisi wanakuwa ni kimbilio la jamii na ni washauri wakuu wa jamii inapokosea. Hapa kwetu ni kinyume chake, jamii, inaiogopa polisi. Kwanini?
Siwapendi polisi wa tz, ukienda kituoni na tatizo wanakugeuza fursa. Pia wanaonea sana raia masikini
 
Ingawa wanatulinda lakini sijawahi kuona polisi mzuri tz likija suala la kesi au ishu yoyote inayokufanya ufike polisi
 
kama walinzi mnao na kampuni tayari,fanyeni mchakato mpate taasisi binafsi za upelelezi sio polisi kamili.
Siyo "fanyeni", tufanye.

Tunaishauri serikali iweke sheria ya kuwa na kampuni za Polisi binafsi, Halafu mashirika makubwa ya serikali yaanze kwa makusudi kabisa kukodisha polisi binafsi, siyo kampuni za ulinzi.

Kama vile shirika la reli, SGR, bandari na mengine mengi tu.


Pia siioni sababu kwanini magereza zisiwepo za mashirika na askari jela binafsi.
 
Ingawa wanatulinda lakini sijawahi kuona polisi mzuri tz likija suala la kesi au ishu yoyote inayokufanya ufike polisi
Ukienda kushitaki kosa, ukishitakiwa kosa.

Jeshi la polisi limekuwa kubwa sana na halijitoshelezi mahitaji yake, linatakiwa lipunguzwe ukubwa kwa kulibinafsisha baadhi ya sehemu ili Polisi waanze kupata malipo mazuri na vifaa vya kisasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…