Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni asema hana taarifa za kukamatwa na kushikiliwa kwa mwanaharakati,Tito Magoti
Mussa Taibu amesema kuwa mpaka sasa hana taarifa ya kukamatwa kwa Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu [LHRC] Tito Magoti, katika eneo la himaya yake na hata amejaribu kuwauliza wenzake lakini nao hawana taarifa hizo.
Awali Kamanda Lazaro Mambosasa aliuthibitisha Umma kwamba Magoti alikamatwa Mwenge wilayani Kinondoni
Taarifa za awali kuhusu kutekwa kwa Tito Magoti ni kuwa alikuwa katika bodaboda akielekea Mwenge kununua simu, alipofika katika kituo cha mafuta cha Puma watu 5 waliokuwa na gari aina ya Harrier walimchukua kwa mabavu kisha kuondoka kwa uelekeo wa Posta, Dar es Salaam.
Jana Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar, Lazaro Mambosasa amekaririwa akisema Polisi inamshikiliwa Magoti na wenzake watatu kwa uchunguzi wa tuhuma za makosa ya jinai inayowakabilia.
Hata hivyo, Mambosasa hajawahi kubainisha ni kituo gani ambacho Magoti anashikiliwa.
Zaidi, soma:
www.jamiiforums.com

Mwanasheria Tito Magoti wa LHRC achukuliwa na watu wasiojulikana; Polisi wasema wanamhoji na wenzake 3
Tito ambaye ni Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) inadaiwa ametekwa maeneo ya Mwenge, Jijini Dar Yaelezwa amechukuliwa na watu 5 waliovalia kiraia ambao walimfunga pingu kabla ya kuondoka naye Watu hao walikuwa kwenye gari aina ya Harrier. Taarifa za awali kuhusu...