Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni asema hana taarifa za kukamatwa na kushikiliwa kwa mwanaharakati,Tito Magoti
Mussa Taibu amesema kuwa mpaka sasa hana taarifa ya kukamatwa kwa Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu [LHRC] Tito Magoti, katika eneo la himaya yake na hata amejaribu kuwauliza wenzake lakini nao hawana taarifa hizo.
Awali Kamanda Lazaro Mambosasa aliuthibitisha Umma kwamba Magoti alikamatwa Mwenge wilayani Kinondoni
Taarifa za awali kuhusu kutekwa kwa Tito Magoti ni kuwa alikuwa katika bodaboda akielekea Mwenge kununua simu, alipofika katika kituo cha mafuta cha Puma watu 5 waliokuwa na gari aina ya Harrier walimchukua kwa mabavu kisha kuondoka kwa uelekeo wa Posta, Dar es Salaam.
Jana Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar, Lazaro Mambosasa amekaririwa akisema Polisi inamshikiliwa Magoti na wenzake watatu kwa uchunguzi wa tuhuma za makosa ya jinai inayowakabilia.
Hata hivyo, Mambosasa hajawahi kubainisha ni kituo gani ambacho Magoti anashikiliwa.
Tito ambaye ni Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) inadaiwa ametekwa maeneo ya Mwenge, Jijini Dar Yaelezwa amechukuliwa na watu 5 waliovalia kiraia ambao walimfunga pingu kabla ya kuondoka naye Watu hao walikuwa kwenye gari aina ya Harrier. Taarifa za awali kuhusu...
Mpaka tutekwe wote ndio tutajua umuhimu wa kuungana kama Taifa kupinga huu udhalimu.
Naanza kupata mashaka kama Tito bado tunae na kama tunae,basi sijui atakuwa katika hali gani.
Ukiona hivi, ujue kuna uwezekana wa mambo mawawili:wamemtanguliza au wamemuumiza na kumjeruhi vibaya kiasi kwamba hawako tayari kuhusishwa/kutuhumiwa na hivyo tunaweza kumuokota akiwa kama Dr.Ulimboka.
Jeshi la polisi lilimkamata Tito Magoti kwa madai eti anatumia fake I'd kuitukana serikali huku wakimhusisha na Kigogo wa Twitter pamoja na I'd ya member maarufu mkosoaji wa Jf...Cha ajabu watu waliohusishwa naye bado wapo wanapost tu...Leo wanasema hawajui alipo ili baadaye wakamtelekeze sehemu kama walivyofanya kwa Mo baada ya kumsainisha nyaraka muhimu kwa nguvu.
KWANI HATUKUMBUKI MAREHEMU AKWELINA ALIPOULIWA MWANZO POLISI WALIKIRI KUPIGA RISASI JUU BAHATI MBAYA IKARUDI NA KULENGA GARI NA KUMUUA AKWELINA? HALAFU BAADAE WAKAKANUSHA KUHUSIKA NA KIFO HICHO NA KUWATUHUMU CHADEMA?
Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesisitiza hana taarifa za kukamatwa kwa Tito Magoti wa LHRC kwenye himaya yake licha ya Kamanda Lazaro Mambosasa kuthibitisha alikamatwa Mwenge wilayani Kinondoni #MwananchiUpdates
Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesisitiza hana taarifa za kukamatwa kwa Tito Magoti wa LHRC kwenye himaya yake licha ya Kamanda Lazaro Mambosasa kuthibitisha alikamatwa Mwenge wilayani Kinondoni #MwananchiUpdates