DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, limedhibiti vurugu zilizokuwa zinafanywa na baadhi ya watu katika eneo la Ubungo Kibo kuanzia saa 4:00 asubuhi hii ya Oktoba 29, 2025.
Watu hao walianza kufunga Barabara ya Morogoro kwa kupanga mawe na kuyarushia mawe magari yaliyokuwa yakipita eneo hilo.
Mwananchi imeshuhudia watu kadhaa wakikamatwa na polisi waliofika eneo la tukio kwa lengo la kuwatawanya watu hao.
Hadi saa 4:35 asubuhi hakuna aliyekuwa akivuka kwenda upande mwingine, polisi walikuwa wametanda na kupiga mabomu ya machozi.
Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa habari zaidi.