Polisi wafafanua tukio la Wakili Lusako Alphonce kukikimbizwa na Polisi katika Ofisi za "Reachout Tanzania"

Polisi wafafanua tukio la Wakili Lusako Alphonce kukikimbizwa na Polisi katika Ofisi za "Reachout Tanzania"

Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 sect 16 inasema ni kosa kusambaza taarifa za uongo kwa njia ya mtandao kama amedanganya akamatwe apelekwe mahakamani akafungwe miaka mitatu au alipe faini 5M ili asirudie
 
Ni kweli kabsa ila kumbuka pia hata Police wamewahi kutoa na kusambazq taarifa za uongo, je bado hii sheria inafanya kazi na kwao?!
 
Polisi bana [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Yaani kwenye taarifa yao wameshindwa kutoa hata namba ya jarada la kesi ya mtuhumiwa ili tujiridhishe kuwa ni kweli alikua na kesi. [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ungepewa no ya jalada, bado ungetaka kujua na mashahidi wa Jamuhuri ni akina nani!? Ufafanuzi naona umejitosheleza vizuri tu!!
 
Mtumieni wakili summons ofisini kwake ili mbaki na ushahidi kwamba mlimuita kwa tuhuma flani flani akikaidi mna haki ya kumkamata kwa nguvu/reasonable force sasa mnakurupuka tu kuna haja ya kuwa na wanasheria polisi. Manake mkiharibu serekali inaonekana imeharibu
.
 
Vyombo vyote vya usalama haviaminiki tena
Hili ndilo tatizo. Wamejitakia wenyewe hawa polisi. Siku hizi hata polisi akija kukukamata kwa kufuata sheria bado mtu unakuwa na wasiwasi kwa sababu walishaonyesha wao siyo watu wazuri.
 
Ni kweli kabsa ila kumbuka pia hata Police wamewahi kutoa na kusambazq taarifa za uongo, je bado hii sheria inafanya kazi na kwao?!
Kawashtaki mahakamani maana hata wao huwa wanashtaki watuhumiwa mahakamani kwahiyo kama wamesambaza unaweza kabisa kuwashtaki
 
Polisi hawaaminiki lazima utoke nduki kwanza kabla hawajakufikia
 
Sa mbona mmeondoka na magari yake km si yeye aliekuwa anahitajika? Polisi acheni kutuona ss ng'ombe,alah!

Hivi kuna watu wanapata teuzi kwa kuonea watu au ni nini?

Kama kuna katiba inayompa mamlaka mtu mmoja kufanya anachofanya kama Mungu ni katiba ya kishetani na matokeo yake ni matendo ya kishetani kushamiri kwa sababu ushetani umetamalaki.

Mtume na Nabii Mwingira aliwahi kusema kuwa pake Ikulu ya Venezuela alimuona shetani akiwa alekalia kiti anapunga upepo akiwa amekunja nne🤣🤣🤣🤣Wakamkamata na kumhoji.
Nadhani alikua sahihi.
 
Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 sect 16 inasema ni kosa kusambaza taarifa za uongo kwa njia ya mtandao kama amedanganya akamatwe apelekwe mahakamani akafungwe miaka mitatu au alipe faini 5M ili asirudie
Si uende mahakamani unatulilia sisi tufanye nini.
 
View attachment 3169735
TAARIFA KWA UMMA
Taarifa iliyo upande wa kushoto inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi lingependa kuitolea ufafanuzi ili isiendelee kuleta taharuki ambayo si ya lazima.

Ni kweli Askari Polisi walifika eneo hilo kumkamata mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mweta, ambaye awali alikamatwa na baada ya kudhaminiwa aliruka dhamana kwa muda mrefu.
Leo Desemba 5,2024, Mlalamikaji alitoa taarifa Polisi kuwa, amemuona mtuhumiwa huyo, ikabidi askari wawahi haraka kumkamata.

Tunaendelea na uchunguzi kubaini ni nini kilichomfanya anayetajwa kwa jina la Alphonce Lusako kukimbia kisha kujirekodi video voice na kuirusha kwenye mitandao wakati siyo yeye aliyekuwa anatafutwa na Askari waliofika pale walijitambulisha kwake na kumweleza wamefika pale kwa nia ya kumtafuta Emmanuel Mweta.
Imetolewa na:

David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

Pia soma ~ Makumbusho: Polisi wadaiwa kuvamia Ofisi za "Reachout Tanzania", wakidai kumtafuta Wakili Lusako Alphonce
😆😆😆😆😆 Hakika Jeshi la polisi linapaswa kuvunjwa na kuundwa upya kabisa.
 
Wa tz sio kabisaa within 2 minutes anatunga tukio na kukudanganya.
 
Back
Top Bottom