Polisi waheshimu maandamano yajayo ya Gen Z kama walivyoheshimu maandamano ya ‘Wakatoliki Feki’ Leo!

Polisi waheshimu maandamano yajayo ya Gen Z kama walivyoheshimu maandamano ya ‘Wakatoliki Feki’ Leo!

Sawa na nyie nyumbu wahalifu tokeni kesho muandamane watawapa mapokezi mazuri
 

Attachments

  • IMG_20260106_000404_969.jpg
    IMG_20260106_000404_969.jpg
    47.4 KB · Views: 17
Andiko la Godbless Lema
"Nina uhakika kinachoendelea dhidi ya Katoliki si mzaha wala burudani, bali ni dharau, dhihaka na kejeli ya wazi dhidi ya Katoliki na Imani ya Kikristo kwa ujumla. Hii ni hatua hatari sana kwa Taifa.
Mzaha wa aina hii hauwezi hata kufikiriwa kufanywa na vijana wa Kikristo dhidi ya taasisi za dini ya Kiislamu. Hebu jaribu kufikiria, hata kwa sekunde moja, vijana wa Kikristo wajifanye Waislamu halafu waandamane hadi BAKWATA. Je, hali ingekuwaje? Jibu lake liko wazi, mambo yangechukua mwelekeo mwingine kabisa.

Leo watu wanaandamana hadi Ubalozi wa Vatican bila kizuizi chochote, huku vyombo vya dola vikitazama kana kwamba hakuna tatizo. Halafu bado mtu anataka kutuambia kwamba hili sio kazi ya dola wala uzembe wa makusudi? Huu ni ukimya unaohatarisha Taifa. Serikali, kwa kuruhusu hali hii, mnafungua mlango mpana wa uharibifu wa amani na mshikamano wa kitaifa. Mnasahau jambo moja muhimu sana, ndani ya vyombo vya dola kuna Polisi, Usalama wa Taifa, na Jeshi na ndani yake kuna Wakristo wengi, wakiwemo Wakatoliki.

Kuendelea kudharau imani yao hadharani ni kuchezea hisia za hao . Hili ni jambo la hatari kubwa. Mkiendelea hivi, mtakuwa mnaandaa mazingira ya mgongano wa kijamii na kidini ambao matokeo yake yatakuwa mabaya mno kwa Taifa. Onyo hili si la kejeli wala si la vitisho, ni mwito wa akili na busara. Acheni mara moja. Acheni kabisa. Rudisheni upumbavu huu nyuma kabla haujageuka janga la kitaifa".
 
Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza PhD atia neno Sinema ya wakatoliki Feki. Anena haya;
"POLISI NA “WAKATOLIKI”

1. Nalazimika kuwapongeza Polisi wetu kwa ukomavu wao na ustaarabu wa kutozuia maandamano ya “Wakatoliki” walioenda kueleza hisia zao kwa Balozi wa Papa hapa nchini.

2. Nachukulia uvumilivu wao kama ishara ya kuacha kupambana na maoni ya watu na hisia zao. Basi wafute hata kesi za Mzee Mwandambo aliyekamatwa kwa kueleza hisia zake za kidini.

3. Kumbe, msimamo huu wa Polisi ulianza mapema pale walipomvumilia kiongozi aliyesema atakata vichwa vya watakaoandamana. Shikilia hapo hapo Polisi, jizuie kuingilia uhuru wa watu na maoni yao.

4. “Wakatoliki” hawa wasiojua kusoma vizuri walichokiandaa; walioamua kumwimba “Mwamba ni Yesu” badala ya Bikira Maria Mlinzi wa Taifa letu, na waliosahau kuwa Baba Mtakatifu wa sasa anaitwa Papa Leo wa 16; wametimiza haki yao ya kikatiba.

5. Watakapokuja Wakatoliki halisi wanaojua kusoma na kuvaa kwa heshima mbele ya Balozi wa Papa, wakasoma tamko lao kuwataka Polisi wamkamate aliyempiga Fr. Kitima, na wamlete aliyeteka mapadre na kuwadhalilisha, akawavisha wake za watu mavazi ya kitawa ili waonekane ni watawa walioshika bendera za vyama nk - hawa Wakatoliki wakiandamana, Polisi kuweni wavumilivu kama mlivyokuwa wavumilivu kwa “Wakatoliki” hawa.

Sisi Wajaluo tunaamini kuwa chuki dhidi ya Ukatoliki inayoendeshwa kwa mikakati mibovu, ina nia mbaya dhidi ya serikali kuliko ilivyo na nia mbaya dhidi ya Ukatoliki.

Kupigana na Ukatoliki ni lazima uwe na dini nyingine ndani yako inayokusukuma kupigana vita hiyo. Wajaluo “tusiotahiriwa” tunajiuliza hiyo dini ni ipi"?
 
Jeshi la polisi liswavumilie hao kenge wavunja amani!
 
Jaribu kuandamana,
Nguvu na formula waliyotumia ni ile ile na wanapongezana imefanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana…
Wakina nan wanapongezana?? Siwajui tusije tukaanza kuwindana
 
Back
Top Bottom