Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Polisi walinasa malori mawili katika eneo bunge la Endebess Kaunti ya Trans Nzoia yakidaiwa kuwabeba wapiga kura 91 kutoka taifa jirani la Uganda kulekea vituo mbalimbali vya kupigia kura.
Watu 65 walifanikiwa kutoroka kufuatia usaidizi wa Mbunge wa Endebess Robert Pukose ambaye alipaza kilio cha kunyanyaswa na maafisa hao wa polisi. CPD wa Endebess Salesioh Muriithi amenukuliwa na Nation.
Kizaazaa kilizuka mbunge huyo ambayo alikuwa akisindikiza malori hayo alipofungua mlango wa nyuma wa lori moja kuwasaidia wapiga kura hao kutoroka.
Mbunge huyo alidai kuwa kulikuwa na njama ya kuwanyima wafuasi wake haki yao ya kupiga kura. Pukose anatetea kiti chake kwa tiketi ya chama cha UDA na ana wapinzani kumi. “OCPD amepewa pesa kuwatesa wafuasi wangu. Ni makosa kuwakamata wapiga kura ambao ni Wakenya halali,” Pukose alisema.
Maafisa wa polisi walifanikiwa kukamata 26 kati yao wakiaminika kusafirishwa kutoka taifa jirani la Uganda. OCPD Mureithi alitetea hatua yake akimtuhumu mbunge huyo kuwatoa wapiga kura kutoka nchi jirani.
“Kama hawa ni watu ni Wakenya halali, hawangetoroka. Mbunge huyo anajua amewaagiza wapiga kura kutoka nje ya taifa,” Mureithi alisema.
kiswahili tuko