John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Wakati mwili wa Jacob Elias (44) mkazi wa Milanzi Manispaa ya Tabora anayedaiwa kufariki dunia kutokana na kipigo alichokipata akiwa mahabusu ukizikwa jana Februari 16, 2022, Jeshi la Polisi limekana kuhusika na kifo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amekana kuhusika kwa kifo hicho na kudai kuwa marehemu alionekana dhaifu kiafya wakati alipofikishwa kituo cha Polisi.
“Wakati upelelezi ukiendelea mtuhumiwa alibainika kuwa mgonjwa kutokana na kutapika huku akionekana kama mtu mwenye tatizo la ugonjwa wa akili, ndipo Polisi wakampeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete kwa matibabu,” ilisema taarifa ya Ambwao.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa ripoti ya daktari aliyempokea na kumhudumia, marehemu Jacob alibainika kuwa na tatizo la kisukari kushuka mwilini na baada ya matibabu Februari 10, 2022 alirejea kituo cha polisi.
Pia soma > INASIKITISHA; Tuhuma nyingine nzito kwa Jeshi la Polisi, watuhumiwa wawili wafariki Morogoro na Tabora