Polisi wakikutwa wao hawajitaji majina, ila raia wanatajwa majina hata bila udhibitisho, sasa je, RTO wa Iringa anaitwa nani?

Polisi wakikutwa wao hawajitaji majina, ila raia wanatajwa majina hata bila udhibitisho, sasa je, RTO wa Iringa anaitwa nani?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
polisi.jpeg

Wanyonge wanaomba majina, mkoa gani na je , mbona huwa hamuwataji?
Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, amesema baada ya ukaguzi, wahusika walichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushtakiwa, Askari 8 wamefukuzwa kazi na kufutwa Jeshini na wengine kesi zao zipo hatua za mwisho.

WADAU WANASEMAJE?
1.jeshi liki amua kuchunguza mashine ya MSATA kutoka bagamoyo na MSATA kutoka MKATA,..ingine KOROGWE hawa wapo pale holet ya KILIMANJARO na MWAGA zichunguzwe pia zimekuwa ni kilio kikubwa sana kwetu madereva.
2. Fanyeni uchunguz mashine yachalinze manakilasku tunapgwa toshi spid iyoiyo.
3. WAsikilizwe, huenda mashine ni mbovu na si zao.
 
Wanyonge wanaomba majina, mkoa gani na je , mbona huwa hamuwataji?
Polisi hawataki kusema ukweli kwamba askari wameingilia mfumo wa malipo ya serikali na kuiba faini zilizokuwa zinalipwa, bali wanasema eti makosa ni ya kinyume cha taratibu kupima spidi.

Tumekuwa tukiona juhudi kubwa ya Polisi kutembea na mashine za kulipia fine, kuweka vizuizi barabarani kutoza watu faini, kumbe zile fedha zilikuwa zinachepushwa na kuingia mifukoni mwao, halafu leo mnatuambia ni askari nane tu walifanya hivyo. Ni karibu Polisi Tanzania nzima walihusika, na haiwezekani kwamba viongozi wa juu wa Polisi hawakuwamo kwenye hili dili.

Waambieni wananchi ukweli, Polisi wamefukuzwa kazi kwa kughushi mfumo wa malipo na kukwepesha hela kwenda serikalini na kuziingiza mifukoni mwao, msifichefiche uovu wa askari wenu. Na inajulikana sio nane tu, ni wengi mno hadi serikali imeona aibu kuwafukuza wote! Ni aibu kubwa hata kwa Raisi Samia mwenyewe, na waziri wa mambo ya ndani anapaswa kujiuzuru.

Yaani hii serikali ya Samia wizi umeingia hadi Polisi, sio tu halmashauri za miji na majiji kama huko Arusha Mbeya nk!
 
Kwa hakika wanapaswa kutoa ufafanuzi hasa katika maeneo yafuatayo
1. Wataje majina na maeneo walikokuwa wakifanyia kazi, kama ulivyo utaratibu wao wa kawaida.
2. Majina na mahali wanakofanyia kazi hao" wengine" wanaoendelea kushtakiwa.
3. Uhalifu huo umefanyika kwa muda gani? Na wasimamizi walikuwa wapi? Nao wamewajibishwa?
4. Kosa hasa ni nini, lilifanyikaje?
 
Askari wa usalama barabarani wengi ni wasumbufu sana. Kama hao wa Iringa ndiyo wanaendekeza rushwa mpaka basi.
 
Back
Top Bottom