Polisi walilia Mishahara na Posho kazini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kutorekebishwa kwa mishahara hata baada ya kupandishwa cheo kwa askari wa Jeshi la Polisi, kumezua malalamiko kwamba hali hiyo inaathiri mafao yao wanapostaafu.

Licha ya kilio hicho, kwa upande wa askari wa usalama barabarani wao wanalia kufutiwa posho ya pango la nyumba tangu Julai Mosi Serikali ilipoanza kulipa mishahara mipya kwa watumishi wake wote.

Kwa nyakati tofauti, askari wa jeshi hilo, kuanzia waliostaafu hata waliopo kazini, wameeleza kilio chao wakisema kinashusha ari ya kazi, kwani kinachofanyika ni kujenga msingi wa kuwapunja stahiki waliyoitolea jasho.

Baadhi ya askari hao, walilieleza Mwananchi kuwa mwaka 2013 walipandishwa cheo kutoka mkaguzi wa polisi kuwa mrakibu msaidizi wa polisi (ASP), lakini mishahara yao haikubadilishwa. Kuendelea kulipwa mishahara ya awali kwa muda mrefu, walisema kulipunguza michango yao ya hifadhi ya jamii.

“Juni 2013, askari 199 tulipandishwa cheo kutoka mkaguzi kuwa mrakibu msaidizi wa polisi lakini hatukuwahi kupandishwa mshahara kulingana na cheo hicho kipya tulichokuwa nacho hadi mwaka 2018 baadhi yetu wakastaafu, wengine wamefariki na wachache wamepandishwa tena cheo ila bado hatujui hatima ya malimbikizo yetu kitendo kinachotuathiri hadi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii,” inasomeka sehemu ya taarifa ya wapambanaji hao.

Askari hao wanasema wameingia kila ofisi kufuatilia haki hiyo lakini hawajafanikiwa kubadilisha nyepe kuwa njano hivyo kuendelea kuumia.

“Tunaomba mtusaidie kutusemea kwani tunaumia sana kiutendaji. Taarifa ipo kwa viongozi wa jeshi, wizarani nako wanajua hata hazina. Mpaka tunafika kwenu tumekosa msaada na hakuna majibu. Tunalitumikia Jeshi la Polisi kwa utiifu lakini mwisho wake unakuwa wa majonzi,” wameeleza askari polisi.

Polisi mwingine aliyekoma utumishi zaidi ya miaka mitano iliyopita alisema alistaafu akiwa na cheo cha sajenti na alilipwa mafao ya Sh32 milioni badala ya Sh70 milioni alizostahili kwa sababu hakupandishiwa mshahara wa cheo alichostaafia.

“Hilo tatizo lipo tena naomba mliandike kwa uzito mkubwa ili liwasaidie wenzetu ambao bado wapo kwenye utumishi wa umma ili lisiwakute. Mimi nimestaafu kwa cheo cha sajenti lakini mafao yamekokotolewa kama koplo matokeo yake nimepunjwa,” alisema.

Kutorekebishiwa mshahara kuendana na cheo kipya alichokuwa nacho wakati anastaafu, alisema kumeathiri kiwango cha pensheni anachopata pia kwani ni kidogo kuliko anachostahili kupata.

Hivi karibuni kumekuwa na madai ya askari polisi kupunjwa kwa baadhi ya stahiki zao hasa wanapokwenda kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ambako hukuta michango haijapelekwa kama ilivyotakiwa.

Baadhi ya wastaafu wanaeleza kukytana na usumbufu katika ufuatiliaji wa mafao yao unaowachosha kwa kuambiwa wasubiri kila wakati kwamba kuna vitu havijakamilika kutoka kwa mwajiri wao.

“Kitu kinachotuumiza sisi ni kuwa, wastaafu waliomaliza na vyeo vya juu hatukuingiziwa mafao yetu kulingana na vyeo tulivyomaliza navyo, unakuta michango yetu haiendani na hesabu na hili liko kwa wengi wetu,” alisema mstaafu huyo.

Kingine kinacholalamikiwa ni kuchelewa kulipwa kwa mafao hata wanapokamilisha nyaraka zote kwani hujitokeza usumbufu ambao hawajui unatokana na nini jambo linalowaumiza kwani hali hiyo hujitokeza baada ya kuitumikia nchi kwa moyo mmoja.

Aliyekuwa Kamishina wa Utawala wa Polisi, Benedict Wakulyamba alisema hakuna mstaafu ndani ya jeshi hilo ambaye atanyimwa haki yake kwa kuwa wanazifanyia kazi changamoto zote zinazojitokeza.

Baadhi ya changamoto ambazo zinatajwa kuchelewesha mafao, Wakulyamba alisema ni tofauti ya umri katika baadhi ya nyaraka za watumishi, mifumo ya upandishaji vyeo na kukosekana kwa taarifa sahihi kwa baadhi yao.

Wakulyamba alikiri kuwepo na suala hilo lakini akasema si matatizo yote yanafanana bali kuna utofauti kati ya mtu mmoja na mwingine na mara nyingi wanayashughulikia kulingana na aina ya tatizo.

Kuhusu michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, alisema upandishaji vyeo mara nyingi umekuwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji umakini mkubwa hivyo jambo hilo mara nyingi linakuwa moja ya sababu ya kuchelewesha au kulipa michango katika cheo cha chini.

Kwenye umri alisema uandikishaji wa nyaraka mara kwa mara kunawafanya watu wanachanganya ama kujisahau kwani baadhi yao nyaraka kwenye mafaili yao zinasoma tarehe nyingine tofautina zilizopo kwenye Kitambulisho cha Taifa (Nida) hivyo kunakuwa na ulazima wa kujiridhisha.

“Lakini yote kwa yote, hakuna mtu atakayekosa ama kunyimwa haki yake, lazima tushughulikie kikamilifu na kuyamaliza matatizo yote kwa wakati unaotakiwa kwani tunatambua na kuthamini mchango wa askari hawa walioitumikia nchi yao kwa uaminifu mkubwa,” alisema.

Kiongozi huyo alisema hadi sasa wamepunguza kwa kiasi kikubwa madai ya wastaafu kwani yalikuwa wengi ila yamebaki kidogo.

Wakulyamba aliondolewa katika wadhifa huo na nafasi yake kuchukuliwa na Salome Kaganda aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Trafiki nao si shwari

Askari wa usalama barabarani nao wanalalamika kuhusu mabadiliko waliyofanyiwa hivi karibuni ya kufutiwa posho tofauti na askari wa idara nyingine jambo linalowavunja moyo.

Kuanzia Julai mosi Serikali ilipoongeza mshahara kwa watumishi wake, mmoja wa trafiki hao aliliambia gazeti hili kwamba waliokuwa wanalipwa mpaka Sh600,000 kwa mwezi waliongezewa Sh60,000 kila mmoja lakini kuanzia mwezi huo posho yao ya pango la nyumba ambalo yeye analipwa Sh30,000 lililondolewa.

“Mimi nashangaa, CID (askari kanzu) wana posho, FFU (askari wa kutuliza ghasia) wanayo hata madereva pia wanayo, why (kwa nini) sisi na kazi yetu ni ngumu balaa,” alilalamika.

Kwa mabadiliko hayo yaliyofanywa na jeshi, trafiki mwingine alisema badala ya mshahara kuongezeka kwa Sh60,000 iliyopandishwa na Rais Samia, imekuwa Sh20,000 tu.

“Fikiria tu hata kama ungekuwa wewe, hiyo ni nini sasa? Tulipoambiwa mshahara unaongezeka tulitarajia itakuwa hivyo lakini Serikali inaongeza halafu jeshi linafuta posho utafikiri tunafanya kazi kwa mhindi,” alisema trafiki huyo.

Alipotafutwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camillius Wambura na kuulizwa kuhusu madai hayo ya askari wake, alijibu kwa ujumbe mfupi kwamba: “Nafuatilia.”

MWANANCHI
 
Wameambia mara nyingi kikwazo kikubwa cha maendeleo yao ni wao wenyewe - kukandamiza demokrasia nhini kwa kuwapendelea chama tawala.
 
Nin kosa la uhaini askari kullalamikia mshahara. Askari amekula kiapo cha utii na uaminifu na hata kuifia nchi yake. Iweje anadai nyongeza ya mshahara??

Watafutwe hao askari wanaolalamika wafutwe kazi na kisha wanyongwe.
 
kuna gari ya police huku imepata ajari ila kwa bahati mbaya hakuna aliyekufa
 
Kamanda Misime ambaye ndio msemaji wa Jeshi hilo amedai kwamba Mishara ya Polisi na posho zao ni vya Kutukuka .
 
Nakumbuka Utawala wa AWAMU ya 5 uliwaruhusu Wale RUSHWA sasa Imekuwaje
 
Back
Top Bottom