Wakati Fulani nilitaka kuungana na Mwajili wao kwamba mambo ya ndani ya Jeshi ni Siri na hii ni Kwa mujibu wa sheria au miongozo inayoliongoza Jeshi hilo. Lakini baadaye nikabaini kwamba hata hayo madai ni Kwa mujibu wa sheria siyo kwamba wanadai mshahara mpya la hasha wanachokidai kipo kwenye sheria hizohizo zinazowakataza kuongea hivyo bila kufuata utaratibu uliowekwa.
Pili nilitaka kuwalaumu Kwa kukosa Uvumilivu Kwa mujibu wa taaluma yao nikauliza kama tatizo ni la muda mfupi lakini nikabaini tatizo ni zaidi ya miaka kumi na nikabaini hata hao wakubwa hawajatimiziwa madai Yao mbalimbali nikahisi labda Kuna watu wapo NYUMA ya pazia wanachochea. Lakini nadhani malalamiko ya Askari yamekuja baada ya Uvumilivu kufika mwisho na kubanwa katika kutatua kero hizo Kwa wakati.