Polisi waliofariki Singida wameagwa, je, mahabusu waliofariki wataagwa wakimaliza kesi zao?

Polisi waliofariki Singida wameagwa, je, mahabusu waliofariki wataagwa wakimaliza kesi zao?

Ila Mwaka Huu wanakufa kweli kweli.Nafikiri kadiri tunavyokaribia Tarehe ya Kilele kasi yao ya Kufa itaongezeka.Usishangae siku likaanguka basi zima au wakakamata mashine na kuanza kupelekeana moto wenyewe kwa wenyewe.
dhambi ua MO29 haitowaacha salama kamwe!
 
Mgonjwa kufungwa pingu ni kawaida tu. Inaweza kuwa ana kesi kubwa, kwahiyo haaminiki kulazwa bila pingu.

Hatima ya mahabusu waliofariki, unataka usikie neno gani? Mbona ni akili ya kawaida. Kuna unyama gani hapo sasa
Mara utasikia kaiba kuku wa jirani yake
 
Kuna nyuzi ukizisoma unaanza kuelewa mikopo ya simu imepelekea smartphone kuangukia katika mikono isiyo sahihi.

Kuna swali ukiuliza linadhihirisha kiwango cha uelewa wako na kupambanua uwezo wako wa kufikiri hata kupambanua mambo madogo ambayo yanahitaji akili ya kuvukia barabara tu kuweza kupata majibu sahihi.

Kuna watu wa kale waliwahi kusema "Ukimya unaweza kumfanya hata mpumbavu kuonekana mwerevu, ila atakapoongea itakuwa njia ya kujitambulisha"

Msemo mwingine wa watu wa kale waliwahi kusema, "Mwerevu ana uwezo wa kupata taarifa zaidi kupitia swali la mpumbavu, kuliko mpumbavu anavyoweza kupata maarifa kupitia jibu la mwerevu"

Kupitia swali lako mleta uzi imedhihirisha kuwa nyie ndiyo wale wa kudandia mada mitandaoni na kubishana bila kuwa na hoja wala facts bali kufuata mkumbo.
 
Tangu ajali ya gari iliyotokea Singida na kuua mahabusu na askari wanaozungumziwa ni askari tu huku mahabusu hatujui kama wao bado wanaendelea na tuhuma dhidi yao,! Kumbe gari lilibeba watu na mahabusu.
Ivi Kuna ulazima Gani kumtoa mtu mahabusu huku umemvua shati??? Yaani hii manake ni nini haswa?
Umempoka.viatu,.mkanda na shati pia?
Hawa ndo maana wakifa Mimi nashangilia kama nipo bar naongeza kinywaji
 
Polisi wameagwa vizuri sana kuanzia kwenye dini zao mpaka kazini kwao, nimeona kwa polisi mmojawapo hapa mtaani nyumbani kwake. Hao mahabusi sikushuhudia hata mmoja nione walivyoagwa

Utaratibu wa kuagwa hao, ni wa familia yao.
 
Back
Top Bottom