Polisi waliohusika na M.150 Wafukuzwa kazi!

wasingefanya mngesema viziwi,wakifanya mnasema legelege
 
Mbona nasikia hata wakubwa wengi tu wamepata mgao?na pIa mbona Chagonja hajafukuzwa?maana yeye na Mke wake wameshiriki kuwalipisha vijana pesa za kupata ajira polisi?mbona wao hawajafukuzwa wanamuonea Chalamila!
 
Kuna vitu hatuvijui ila kova na hao maaskari watano wanavijua
 

...safi kabisa...kesho utamkuta Kova ni gateman kwa hao aliowanadi kuwafukuza leo
 
Narudia tena Ccm wanajipanga kwa ajili ya 2015...
 
Kama watapigwa mvua ndogo bila kurudisha hizo hela itakuwa bingo kwao kuliko kazi yao ndani ya miaka 20.
 

Isije kuwa hao ndio huwa wanaandaliwa kuwa-Limboka watu!
 

hata me nahisi kuna kiini macho nahii nikwanin itokee baada yachmbi kuwacmamisha wengne je mda walikuwa wap? Je hzo m150 watazludsha vp achen hzo bana pengne mmekula wote baada yakunuka ndo mumeamua kuwa kuwaangushia jumba bovu askar wa chini nahv polisi wenyewe hawapendan na hawana uhuru mbona mwaka huu ni wao
 
Ni utaratibu wa Sheria za nchi polisi haruhusiwi kushtakiwa mahakama ya kiraia kabla ya kufukuzwa kazi kwa makosa ya jinai , hivyo basi tatizo jingine siku hizi ni kwamba mpaka hati ya mashtaka mpaka iende kwa DPP halafu DPP kama wmeshaenda kumwona unaweza ambiwa hakuna ushahidi wa kutosha, then Kimyaaaa
 
Kuwafukuza tu sio suluhisho,tatizo ni pale mtu aliyepewa dhamana ya kulinda uhai na mali za Mtanzania yeye ndiye anahusika kuhujumu na kumuibia mtu ambaye anamlinda,ni sawa unampa fisi kumlinda mbuzi ndio hali ilivyo sasa hivi
Pesa imepotea ikiwa mikononi mwa polisi ambao ni walinzi wa mali za wananchi,je polisi watamlipa muathirika aliyepotelewa na hizo pesa? Au kuwafukuza tu ndio tosha then pesa yake imepotea? Ukizingatia maisha ya Mtanzania mmoja kama si wawili yalikoma je fidia inakuwaje hapo?
Jeshi la polisi limelalamikiwa mara nyingi kiasi cha kufikia wananchi kukosa imani na jeshi hilo Kova atawahakikishiaje wananchi kuwa polisi ni sehemu salama kwa mwananchi wa Tanzania na kuondoa ile dhana kwamba polisi ni kichaka cha wahuni na wezi fulani ambao wanatumia madaraka waliyonayo ya kuvaa rangi ya taifa ili tu kufanikisha maovu yao?
Je ni hawa ndio watu walioaminiwa na nchi kuwapa ulinzi wa taifa letu?
Je haionekani sasa ni wakati muafaka wa serikali kuchuja na kufuatilia nyendo za wanaoajiriwa na jeshi hilo ili waajiriwe watu makini wasioliletea jeshi la polisi kashfa zisizokuwa na msingi,na jeshi limewekaje mazingira ya kuhakikisha kwamba hilo jeshi si kichaka cha wahuni na wezi?
Ndani ya wiki moja yametokea matukio yanayochafua sura ya jeshi la polisi na kuthibitisha si walinzi wa mali ha uhai wa wananchi kwani wao ndio wanaoongoza kwa kuwaua watanzania kwa silaha zilizonunuliwa kwa kodi wanazolipa hao watanzania wanaouawa,matukio ya rushwa,ujambazi kuuza vielelezo vya madawa ya kulevya na kuweka sukari na chumvi inathibitisha wazi kwamba jeshi la polisi kuanzia juu hadi chini hawako makini ni kundi fulani la wahuni au hawa wa chini hawathaminiwi ndio maana wanafanya vitendo vya ajabu na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa,na ndio maana wanaua halafu wanalindana hawataki wapigwe picha na kuondoana maakamani kiholela,mie nafikiri ifikie wakati jeshi hili waangalie je wanawasaidiaje wananchi au wanaangalia maslahi yao,watu wanauawa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa damu za watanzania zinamwagwa na watanzania wenzao bila aibu tumefikia huko?
Hatua zinazochukuliwa sasa hivi zimechelewa ilitakiwa zichukuliwe mapema na si sasa
 
vipi? kuhusu wale walioficha fedha Uswis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…