Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Jeshi la Polisi limemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam mfanyabiashara wa mtandaoni, Jenifer Jovin maarufu Niffer baada ya kujisalimisha polisi jana.

Mfanyabiashara huyo alijisalimisha kwa Jeshi la Polisi jana baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza Jeshi hilo kumhoji kwa kosa la kukusanya fedha za michango kwa ajili ya waathirika walioporomokewa na ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam bila kibali.
Pia, Soma:

Jengo hilo liliporomoka Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya watu 16, majeruhi 86 na uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 19, 2024 jijini Dodoma, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Anania Amo amesema Niffer amekamatwa na polisi baada ya kujisalimisha jana.

“Alijisalimisha jana baada ya kumtafuta, tayari tumemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam,”amesema.

Credit: Mwananchi
Haya manjagu hayaja mshika shika mapaja kweli
 
Nguvu Gani Nyingi imetumika Hapo? Si ameenda Mwenyewe Polisi

Nchi ina miongozo yake na Sheria zake. Hata Wewe sasa hivi huwezi kwenda Hospitalini ukaanza Kugawa Sabuni na Sukari kwa Wagonjwa Lazima Utakamatwa Tu
Vp mwenye jengo na wakandarasi waliyojenga wamekamatwa

Ova
 
😁 wewe hata ukikutana na mimi hutathubutu kuropoka upuuzi.
Kwenda huko wewe ni mjinga flani usiejielewa huku mtandaoni.
Hivi mtu mwenye anonymous id unawezaje kumuuliza swali kama hilo.
Hunijui, sikujui na wala sina ulazima wa kutaka kukujua.
Ila kwa maposti yako ya kijingajinga unayopost hapa JF nimekuelewa wewe kama mjinga flani usiejielewa,mtu wa kujikomba kwa watu, mla matapishi.
Ili uweze kuishi unafanya kazi ya uchawa .
Watu kama nyie nawachukulia kama ma idiot flani .
Pumbavu zako embu achana na mimi ,
Na ukome kureply koment zangu manake unareply mautumbo na maushenzi
 
Nchi hii badala ya kujadili issue ya kuokoa leo Niffer ndio ana trend kazi tunayo.
Binafsi Mimi kilichonisikitisha Zaid ni kuona suala la Niffer limepewa attention kubwa sana, wakati huo muhusika mkuu au mmiliki wa jengo mpaka dk hii hatujui hata sura yake...

Nashindwa kuelewa kwamba huyo mtu ana nguvu sana kiasi Cha kuogopwa mpaka na vyombo vya dola au?? Kwanini mpaka leo hii sijaona akiwa exposed?? Basi hata kampuni ya ujenzi ambayo imehusika na kujenga lile jengo wangeitaja hili watu waepuke kufanya kazi na kampuni ya ovyo kama hiyo, lakini hata yenyewe pia haijatajwa.... Hii nchi hii.
 
Kwenda huko wewe ni mjinga flani usiejielewa huku mtandaoni.
Hivi mtu mwenye anonymous id unawezaje kumuuliza swali kama hilo.
Hunijui, sikujui na wala sina ulazima wa kutaka kukujua.
Ila kwa maposti yako ya kijingajinga unayopost hapa JF nimekuelewa wewe kama mjinga flani usiejielewa,mtu wa kujikomba kwa watu, mla matapishi.
Ili uweze kuishi unafanya kazi ya uchawa .
Watu kama nyie nawachukulia kama ma idiot flani .
Pumbavu zako embu achana na mimi ,
Na ukome kureply koment zangu manake unareply mautumbo na maushenzi
Umeshajaa upepo? Ni mapema sana. Usirudie kuleta ushujaa wa kishamba mtandaoni kisa ID feki wakati hutaweza kuropoka tukikutana uso kwa uso.
 
Yaani niffer anaonekana ana kosa zaidi anye s mwenye ghorofa lililoanguka kwa uzembe....hovyo kabisa
Inauma sana kwakweli, na jinsi medias zetu zilivyotilia maanan suala la nifer wakati sijaona hata Moja akihoji kuhusu mmiliki wa jengo.

Hii nchi Ina maudhi sana kwa wenye akili timamu.
 
Hajafanya kosa lolote sheria inaruhusu watu wachangushe na fedha waziwasilishe kwenye kamati ya maafa .
Kuchangisha fedha sio kosa . Kosa ni kutokuzifikisha hizo fedha kwenye kamati ya maafa
Kwahiyo ni sawa kuanza kutumia hizo pesa kabla hujazifikisha kamati ya maafa?????

Vifungu vingi hata unachotetea hata wewe hukielewi
 
Back
Top Bottom