The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Maafisa wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora wakiongozwa na SACP Richard Abwao, Kamanda wa Polisi mkoani humo wamefanya mazoezi ya kawaida ya mwendo wa pole na haraka katika viunga vya Manispaa ya Tabora yakilenga kujiweka tayari kulinda amani na usalama kwa wananchi hususani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanya Oktoba 29 mwaka huu
Akizungumza baada ya kuhitimisha mazoezi hayo SACP Abwao amewahakikishia wananchi mkoa wa Tabora kuwa salama kipindi chote cha kabla, wakati na baada ya uchaguzi huku akiwasisitiza kwenda kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura pasipo kutanguliza mashaka yoyote au kuhofia kutokea kwa vurugu
Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo hususani vijana kutojihusisha na uchochezi wa kwenye mitandao ya kijamii unaolenga kuleta vurugu, na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote wanaolenga kuleta vurugu.