Nshaelewa mkuu hakuna la kusubiri.ni muhimu zaidi kua wastahimilivu na wenye subra kusubiri uamuzi wa mahakama kulingana na ushahidi utakawasilishwa 🐒
Kwani binti mwenyewe anasemajeNaona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!
Tuko bara la giza ambapo kuna watu wapo juu ya sheria,hii kitu sio afya kama taifa sababu matukio kama yale yanaweza kufanywa tena na tena na mhusika akijua atalindwa kama alivyolindwa mwingine,tunatengeneza taifa la kijinga kwa vizazi vyetu vijavyo
FaizaFoxy weka neno hapa dada etu.Wakuu,
Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!
Mpaka utambulisho wa moja wao umebainika halafu leo maneno yanageuzwa hivi!
Nilikuwa saluni majuzi hapa, si mnajua stori za saluni zinavyonoga sasa wakawa wanajadili suala hili, sasa kwenye stori wakawa wanasema kwamba mmoja ya wale vijana waliohusika kwenye kumbaka binti ni mtoto wa askari mwenye cheo kikubwa, sasa katika malipo vijana wengine walipunjwa mgao, ili kumkomoa jamaa kwakua baba ake ni askari ndio wakaamua liwalo na liwe, wakaachia kideo. Ni kweli au ni story tu za vijiweni kama nyingine, sijui!
Anyways, kwa mara nyingine naona sheria inaenda kupindishwa wenye nguvu wanaenda kushinda hata kama ni wanyama na makatili wanaostahili kufungwa milele
=====
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imesema bado haijafikishiwa jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam.
Picha jongefu (video) kuhusu tukio hilo zilisambaa Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume cha maumbile.
Pia soma: Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama
Katika video nyingine watuhumiwa hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kumshurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la afande, naye alifanya hivyo.
Hata hivyo, katika taarifa aliyoitoa kwa umma Agosti 9, 2024, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema uchunguzi umewezesha kubaini tukio hilo lilifanyika Mei 2024 katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.
Aliwataja vijana waliokamatwa kwa kosa la kumlawiti na kumbaka binti huyo ni Clinton Damas jina maarufu Nyundo, Praygod Mushi, Amini Lema na Nikson Jakson.
Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani na Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili ambao walikuwa hawajapatikana mpaka wakati huo.
Mwananchi leo Jumapili Agosti 18, 2024 limezungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu kuhusiana na hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa sakata hilo na kipi kinaendelea.
Mwakitalu amesema jalada la tukio hilo bado halijamfikia mezani kwake kwa kuwa bado linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.
“Bado upelelezi unaendelea na likifika kwangu ni kukamilisha upelelezi tu, isipokuwa kwa sasa bado jeshi linaendelea na upelelezi,”amesema DPP Mwakitalu.
Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai amesema aulizwe Kamanda wa Mkoa wa Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi watakuwa na majibu sahihi.
“Suala hilo mtafute Kamanda wa Polisi Dodoma au Msemaji wa Jeshi la Polisi watakueleza hatua za tukio hilo lilipofikia,”amesema Kingai
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya amesema jalada la tuhuma hizo limekamilika na kwamba kesho Jumatatu Agosti 19, 2024 atafuatilia kama litapelekwa mahakamani.
Amesema katika uchunguzi, Jeshi la Polisi limebaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.
"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.
"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.
Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, Misime kutaka kujua kama watuhumiwa wengine wawili waliobakia kati ya sita wanaotuhumiwa hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe kwa whatsapp aliousoma lakini hakujibu chochote.
afande akili ndogo mno hapo anajisifu kwamba amemaliza utata wakati upumbavu wa wazi waziMuulize kamanda. Kwahiyo kahaba hana haki zake mana no kama vile anahalalisha kana kwamba kahaba kajitakia!
Hatuna Police......sio policyTanzania hatuna policy
Hayo mambo yalikuwa ya Magu angeshuka nao kuanzia waziri husikaYaaan Kama IGP napita kwanza na RPC mapema kesho hayupo kazini kwake.
Kwa akili zako mkuu huyo raia atabaki salama kwa ushuhuda atakaoutoa!?Ni muhimu ikiwa kuna raia mwema ana taarifa sahihi zenye uthibitisho vijana wale kutumwa na mtu kufanya walicho kifanya, ni vizuri na muhimu sana akashirikiana na vyombo vya uchunguzi au akawasilisha ushahidi huo usio na shaka kwa vyombo vya uchunguzi ili haki itendeke...
Vinginevyo, huruma pekee haitampatia haki muathirika na wahusika kupata adhabu stahiki 🐒
Hhahahaha. Hili jeshi letu la polisi ama kweli kwa usanii limekithiri. Kumbe wakati wanasema wapewe muda wa kufanya uchunguzi wakati ushahidi ulikuwa wazi ndio wakati huo wameutumia kutupikia stori na kubadilisha kibaoWakuu,
Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!
Mpaka utambulisho wa moja wao umebainika halafu leo maneno yanageuzwa hivi!
Nilikuwa saluni majuzi hapa, si mnajua stori za saluni zinavyonoga sasa wakawa wanajadili suala hili, sasa kwenye stori wakawa wanasema kwamba mmoja ya wale vijana waliohusika kwenye kumbaka binti ni mtoto wa askari mwenye cheo kikubwa, sasa katika malipo vijana wengine walipunjwa mgao, ili kumkomoa jamaa kwakua baba ake ni askari ndio wakaamua liwalo na liwe, wakaachia kideo. Ni kweli au ni story tu za vijiweni kama nyingine, sijui!
Anyways, kwa mara nyingine naona sheria inaenda kupindishwa wenye nguvu wanaenda kushinda hata kama ni wanyama na makatili wanaostahili kufungwa milele
=====
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imesema bado haijafikishiwa jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam.
Picha jongefu (video) kuhusu tukio hilo zilisambaa Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume cha maumbile.
Pia soma: Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama
Katika video nyingine watuhumiwa hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kumshurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la afande, naye alifanya hivyo.
Hata hivyo, katika taarifa aliyoitoa kwa umma Agosti 9, 2024, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema uchunguzi umewezesha kubaini tukio hilo lilifanyika Mei 2024 katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.
Aliwataja vijana waliokamatwa kwa kosa la kumlawiti na kumbaka binti huyo ni Clinton Damas jina maarufu Nyundo, Praygod Mushi, Amini Lema na Nikson Jakson.
Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani na Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili ambao walikuwa hawajapatikana mpaka wakati huo.
Mwananchi leo Jumapili Agosti 18, 2024 limezungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu kuhusiana na hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa sakata hilo na kipi kinaendelea.
Mwakitalu amesema jalada la tukio hilo bado halijamfikia mezani kwake kwa kuwa bado linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.
“Bado upelelezi unaendelea na likifika kwangu ni kukamilisha upelelezi tu, isipokuwa kwa sasa bado jeshi linaendelea na upelelezi,”amesema DPP Mwakitalu.
Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai amesema aulizwe Kamanda wa Mkoa wa Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi watakuwa na majibu sahihi.
“Suala hilo mtafute Kamanda wa Polisi Dodoma au Msemaji wa Jeshi la Polisi watakueleza hatua za tukio hilo lilipofikia,”amesema Kingai
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya amesema jalada la tuhuma hizo limekamilika na kwamba kesho Jumatatu Agosti 19, 2024 atafuatilia kama litapelekwa mahakamani.
Amesema katika uchunguzi, Jeshi la Polisi limebaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.
"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.
"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.
Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, Misime kutaka kujua kama watuhumiwa wengine wawili waliobakia kati ya sita wanaotuhumiwa hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe kwa whatsapp aliousoma lakini hakujibu chochote.
na hapo kafanya upelelezi na hajui kapeleleza niniNi kama wavuta bangi
Ni kama anajiuza
Naona kuna "kama" mbili hapo.
Ni kama hawana uhakika wanavuta bangi au kama anajiuza.
Kunatakiwa kuziondoa hizo "kama"
Mahakamani.
sasa unababaika n kutia huruma kwanini, na kuna haja gani ya kuendelea kumfedhehesha kijana wa watu kwa kujdaili kwa hisia ambacho hatuwez kukithibitisha kwa vyombo husika vinavyo deal na kutoa haki kulingana na ushahidi?🐒Kwa akili zako mkuu huyo raia atabaki salama kwa ushuhuda atakaoutoa!?
Au unataka kuponza uhai wa watu tu pasi na faida yeyote!?
Mkuu mambo yako wazi,ni kipi hakijaweza thibitishwa!??sasa unababaika n kutia huruma kwanini, na kuna haja gani ya kuendelea kumfedhehesha kijana wa watu kwa kujdaili kwa hisia ambacho hatuwez kukithibitisha kwa vyombo husika vinavyo deal na kutoa haki kulingana na ushahidi?🐒