Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!
Kwani binti mwenyewe anasemaje
 
Tuko bara la giza ambapo kuna watu wapo juu ya sheria,hii kitu sio afya kama taifa sababu matukio kama yale yanaweza kufanywa tena na tena na mhusika akijua atalindwa kama alivyolindwa mwingine,tunatengeneza taifa la kijinga kwa vizazi vyetu vijavyo
Udhaifu wa jeshi letu la polisi ndio sababu ya watu kujichukulia sheria mkononi.

Mabadiliko katika jeshi la polisi yatakuwepo kama mwenye mamlaka ya kuteua mkuu wa mapolisi atachukizwa na utendaji wa polisi.
 
Mie nilisema tangu mwanzo humu jukwaani, hili tukio watu mmelichukulia kihisia tu, ila inawezekana binti na hao jamaa ni wameamua tu kujirekodi lakini hakuna tukio la ubakaji, yawezekana walifanya kwa makubaliano watu mkaja juuu. Haya tazameni sasa
 
Wakuu,

Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!

Mpaka utambulisho wa moja wao umebainika halafu leo maneno yanageuzwa hivi!

Nilikuwa saluni majuzi hapa, si mnajua stori za saluni zinavyonoga sasa wakawa wanajadili suala hili, sasa kwenye stori wakawa wanasema kwamba mmoja ya wale vijana waliohusika kwenye kumbaka binti ni mtoto wa askari mwenye cheo kikubwa, sasa katika malipo vijana wengine walipunjwa mgao, ili kumkomoa jamaa kwakua baba ake ni askari ndio wakaamua liwalo na liwe, wakaachia kideo. Ni kweli au ni story tu za vijiweni kama nyingine, sijui!

Anyways, kwa mara nyingine naona sheria inaenda kupindishwa wenye nguvu wanaenda kushinda hata kama ni wanyama na makatili wanaostahili kufungwa milele

=====

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imesema bado haijafikishiwa jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha jongefu (video) kuhusu tukio hilo zilisambaa Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume cha maumbile.

Pia soma: Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Katika video nyingine watuhumiwa hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kumshurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la afande, naye alifanya hivyo.

Hata hivyo, katika taarifa aliyoitoa kwa umma Agosti 9, 2024, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema uchunguzi umewezesha kubaini tukio hilo lilifanyika Mei 2024 katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.

Aliwataja vijana waliokamatwa kwa kosa la kumlawiti na kumbaka binti huyo ni Clinton Damas jina maarufu Nyundo, Praygod Mushi, Amini Lema na Nikson Jakson.

Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani na Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili ambao walikuwa hawajapatikana mpaka wakati huo.

Mwananchi leo Jumapili Agosti 18, 2024 limezungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu kuhusiana na hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa sakata hilo na kipi kinaendelea.

Mwakitalu amesema jalada la tukio hilo bado halijamfikia mezani kwake kwa kuwa bado linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.

“Bado upelelezi unaendelea na likifika kwangu ni kukamilisha upelelezi tu, isipokuwa kwa sasa bado jeshi linaendelea na upelelezi,”amesema DPP Mwakitalu.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai amesema aulizwe Kamanda wa Mkoa wa Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi watakuwa na majibu sahihi.

“Suala hilo mtafute Kamanda wa Polisi Dodoma au Msemaji wa Jeshi la Polisi watakueleza hatua za tukio hilo lilipofikia,”amesema Kingai

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya amesema jalada la tuhuma hizo limekamilika na kwamba kesho Jumatatu Agosti 19, 2024 atafuatilia kama litapelekwa mahakamani.

Amesema katika uchunguzi, Jeshi la Polisi limebaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.

"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.

"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.

Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, Misime kutaka kujua kama watuhumiwa wengine wawili waliobakia kati ya sita wanaotuhumiwa hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe kwa whatsapp aliousoma lakini hakujibu chochote.
FaizaFoxy weka neno hapa dada etu.
 
Muulize kamanda. Kwahiyo kahaba hana haki zake mana no kama vile anahalalisha kana kwamba kahaba kajitakia!
afande akili ndogo mno hapo anajisifu kwamba amemaliza utata wakati upumbavu wa wazi wazi
 
Ni muhimu ikiwa kuna raia mwema ana taarifa sahihi zenye uthibitisho vijana wale kutumwa na mtu kufanya walicho kifanya, ni vizuri na muhimu sana akashirikiana na vyombo vya uchunguzi au akawasilisha ushahidi huo usio na shaka kwa vyombo vya uchunguzi ili haki itendeke...

Vinginevyo, huruma pekee haitampatia haki muathirika na wahusika kupata adhabu stahiki 🐒
Kwa akili zako mkuu huyo raia atabaki salama kwa ushuhuda atakaoutoa!?
Au unataka kuponza uhai wa watu tu pasi na faida yeyote!?
 
Wakuu,

Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!

Mpaka utambulisho wa moja wao umebainika halafu leo maneno yanageuzwa hivi!

Nilikuwa saluni majuzi hapa, si mnajua stori za saluni zinavyonoga sasa wakawa wanajadili suala hili, sasa kwenye stori wakawa wanasema kwamba mmoja ya wale vijana waliohusika kwenye kumbaka binti ni mtoto wa askari mwenye cheo kikubwa, sasa katika malipo vijana wengine walipunjwa mgao, ili kumkomoa jamaa kwakua baba ake ni askari ndio wakaamua liwalo na liwe, wakaachia kideo. Ni kweli au ni story tu za vijiweni kama nyingine, sijui!

Anyways, kwa mara nyingine naona sheria inaenda kupindishwa wenye nguvu wanaenda kushinda hata kama ni wanyama na makatili wanaostahili kufungwa milele

=====

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imesema bado haijafikishiwa jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha jongefu (video) kuhusu tukio hilo zilisambaa Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume cha maumbile.

Pia soma: Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Katika video nyingine watuhumiwa hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kumshurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la afande, naye alifanya hivyo.

Hata hivyo, katika taarifa aliyoitoa kwa umma Agosti 9, 2024, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema uchunguzi umewezesha kubaini tukio hilo lilifanyika Mei 2024 katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.

Aliwataja vijana waliokamatwa kwa kosa la kumlawiti na kumbaka binti huyo ni Clinton Damas jina maarufu Nyundo, Praygod Mushi, Amini Lema na Nikson Jakson.

Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani na Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili ambao walikuwa hawajapatikana mpaka wakati huo.

Mwananchi leo Jumapili Agosti 18, 2024 limezungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu kuhusiana na hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa sakata hilo na kipi kinaendelea.

Mwakitalu amesema jalada la tukio hilo bado halijamfikia mezani kwake kwa kuwa bado linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.

“Bado upelelezi unaendelea na likifika kwangu ni kukamilisha upelelezi tu, isipokuwa kwa sasa bado jeshi linaendelea na upelelezi,”amesema DPP Mwakitalu.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai amesema aulizwe Kamanda wa Mkoa wa Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi watakuwa na majibu sahihi.

“Suala hilo mtafute Kamanda wa Polisi Dodoma au Msemaji wa Jeshi la Polisi watakueleza hatua za tukio hilo lilipofikia,”amesema Kingai

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya amesema jalada la tuhuma hizo limekamilika na kwamba kesho Jumatatu Agosti 19, 2024 atafuatilia kama litapelekwa mahakamani.

Amesema katika uchunguzi, Jeshi la Polisi limebaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.

"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.

"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.

Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, Misime kutaka kujua kama watuhumiwa wengine wawili waliobakia kati ya sita wanaotuhumiwa hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe kwa whatsapp aliousoma lakini hakujibu chochote.
Hhahahaha. Hili jeshi letu la polisi ama kweli kwa usanii limekithiri. Kumbe wakati wanasema wapewe muda wa kufanya uchunguzi wakati ushahidi ulikuwa wazi ndio wakati huo wameutumia kutupikia stori na kubadilisha kibao
 
Ni kama wavuta bangi
Ni kama anajiuza
Naona kuna "kama" mbili hapo.

Ni kama hawana uhakika wanavuta bangi au kama anajiuza.

Kunatakiwa kuziondoa hizo "kama"
Mahakamani.
na hapo kafanya upelelezi na hajui kapeleleza nini

hapo hapo watuhumiwa wamekamatwa na kuhojiwa na wakasema hawajatumwa

ila kitendo hakisemwi inasemwa ni kama wavuta bhangi, kama makahaba

ila ni suala la muda wataumbuka
 
video sijaiona.... ila nachoweza kusema na ambacho kipo sahihi kabisa hapo ni hakuna uchunguzi....wala kutafuta sababu ya kwanini walifanya uhalifu...wahukumiwe kutokana na matendo yao...kwa ushahidi wa video na mtendwa....majuto yao ni kama walilipwa au lah...majuto yaoni kumficha aliyewatuma kama yupo...nae ni muhalifu kama wao...
 
Kwa akili zako mkuu huyo raia atabaki salama kwa ushuhuda atakaoutoa!?
Au unataka kuponza uhai wa watu tu pasi na faida yeyote!?
sasa unababaika n kutia huruma kwanini, na kuna haja gani ya kuendelea kumfedhehesha kijana wa watu kwa kujdaili kwa hisia ambacho hatuwez kukithibitisha kwa vyombo husika vinavyo deal na kutoa haki kulingana na ushahidi?🐒
 
Mkuu mambo yako wazi,ni kipi hakijaweza thibitishwa!??
Yani kaka unakua kama mgeni wa hii nchi.Kuwa kada wa CCM tumeshakukosa kaka,haukuwa hivi wewe.
 
Back
Top Bottom