Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Keyword "KAMA", hilo neno tayari limeshabeba walakini na sheria haitakiwi kuwa hivyo. Anything that can't be proven beyond reasonable doubt, has loopholes.
Natamani wajue hili watu wanajua hii nchi haina haja ya sheria tukiwa wendawzima tukikubali sheria isifuatwe tutakua taifa la hovyo km sheria haina umuhimu basi harmonize alipokopwa asamehewe deni manake ni amesingiziwa tu kakopa
 
Wakuu,

Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!

Mpaka utambulisho wa moja wao umebainika halafu leo maneno yanageuzwa hivi!

Nilikuwa saluni majuzi hapa, si mnajua stori za saluni zinavyonoga sasa wakawa wanajadili suala hili, sasa kwenye stori wakawa wanasema kwamba mmoja ya wale vijana waliohusika kwenye kumbaka binti ni mtoto wa askari mwenye cheo kikubwa, sasa katika malipo vijana wengine walipunjwa mgao, ili kumkomoa jamaa kwakua baba ake ni askari ndio wakaamua liwalo na liwe, wakaachia kideo. Ni kweli au ni story tu za vijiweni kama nyingine, sijui!

Anyways, kwa mara nyingine naona sheria inaenda kupindishwa wenye nguvu wanaenda kushinda hata kama ni wanyama na makatili wanaostahili kufungwa milele

=====

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imesema bado haijafikishiwa jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha jongefu (video) kuhusu tukio hilo zilisambaa Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume cha maumbile.

Pia soma: Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Katika video nyingine watuhumiwa hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kumshurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la afande, naye alifanya hivyo.

Hata hivyo, katika taarifa aliyoitoa kwa umma Agosti 9, 2024, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema uchunguzi umewezesha kubaini tukio hilo lilifanyika Mei 2024 katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.

Aliwataja vijana waliokamatwa kwa kosa la kumlawiti na kumbaka binti huyo ni Clinton Damas jina maarufu Nyundo, Praygod Mushi, Amini Lema na Nikson Jakson.

Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani na Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili ambao walikuwa hawajapatikana mpaka wakati huo.

Mwananchi leo Jumapili Agosti 18, 2024 limezungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu kuhusiana na hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa sakata hilo na kipi kinaendelea.

Mwakitalu amesema jalada la tukio hilo bado halijamfikia mezani kwake kwa kuwa bado linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.

“Bado upelelezi unaendelea na likifika kwangu ni kukamilisha upelelezi tu, isipokuwa kwa sasa bado jeshi linaendelea na upelelezi,”amesema DPP Mwakitalu.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai amesema aulizwe Kamanda wa Mkoa wa Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi watakuwa na majibu sahihi.

“Suala hilo mtafute Kamanda wa Polisi Dodoma au Msemaji wa Jeshi la Polisi watakueleza hatua za tukio hilo lilipofikia,”amesema Kingai

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya amesema jalada la tuhuma hizo limekamilika na kwamba kesho Jumatatu Agosti 19, 2024 atafuatilia kama litapelekwa mahakamani.

Amesema katika uchunguzi, Jeshi la Polisi limebaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.

"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.

"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.

Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, Misime kutaka kujua kama watuhumiwa wengine wawili waliobakia kati ya sita wanaotuhumiwa hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe kwa whatsapp aliousoma lakini hakujibu chochote.

Pia soma: Waziri Gwajima: Alichofanyiwa binti wa Yombo ni kitendo kibaya kisicho na utu, nimewasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani ili haki itendeke
Alietuma wahuni huyo hapo ni afande anahudumu bungeni dodoma
 
Attachments

  • IMG_20240812_185605.jpg
    IMG_20240812_185605.jpg
    67.9 KB · Views: 2
Kweli mkuu.
Wenzetu washatoka kwenye kuangalia miguvu ndo mana marekani ili uwe mwanajeshi unabid atleast utokee college ukileta wahuni jeshini huchelewi kumkuta afande yuko lindo na chupa ya hennessy wenzetu wako smart sana.
 
uko sahihi kabisaa
 
Nilishasema humu kuwa hao vijana hawatofanywa chechote kile kwasababu dalili zilionekana mwanzo hakika magufuli atakumbukwa kwa mengi
wafanywe nini wakati kahaba alikuwa anajiuza.
tupinge biashara ya ukahaba.
 
Yeye mwenyewe sio kahaba? Hicho cheo mpaka anapofika hapo amepitia milango ipi?
Huyo afande aliewatuma ni kahaba mzee anamiliki grocery dodoma...huyu hapa na sura yake ya kiume
 
Attachments

  • IMG_20240812_185611.jpg
    IMG_20240812_185611.jpg
    25.1 KB · Views: 2
Uchawa unafanya watu kuwa watumwa wa viongozi 🐷
huruma, mizaha, harakati za kisiasa na hisia potofu kwenye mambo serious ya kisheria mahakamani, zinasababisha wengi kupoteza haki zao za msingi dhidi ya dhuluma walizopitia 🐒
 
Kwa hiyo kahaba ni ruksa kubakwa na kulawitiwa!
Ama nimeelewa vibaya?
 
Mimi ni aina ya watu Kama JPM sija angalia video Ila nimekua msomaji na mfuatiliaji wa hii saga kupitia JF na pia redion wasafi media

Kwenye jamii Kuna dada zetu Malaya na kwa ridhaa zao wanaamua kukubali kufanyiwa hivyo vitendo unakuta mtu (Malaya) kashindikana tabia za ajab kabisa alaf wakifanyiwa wanakimbilia haki za binadamu sijui katiba (malalamiko mengi)

All in all,
Kama kweli dada kaonewa Basi haki itendeke, sio TU kutendeka ionekane inatendeka

Ona Sasa afande anaingia matatizoni inamaana kabla afande Mallya hajafanya public speaking 🗣️ huwa hafanyi meeting na wataalan wake kujua ni Nini akazungumze kwa umma na Nini si Cha kuzungumza kwa UMMA (public speaking)
 
Hajabakwa bhana na wewe usitumie hisia, yule kataka mwenyewe, abakwe asishitak police
Au wewe unawazidi wenye taaluma Yao waliochunguza
Mambo ya kubakwa au umalaya au alitoa ushirikiano, hayo yote RPC angeiachia office ya mashitaka na Mahakama, yeye.angeishia kwenye kusema jalada la upelelezi lishakamilika kwa hatua zaidi z kisheria linapelekwa kwa office ya mashitaka!!
 
Eti Jeshi la Polisi linajinasibu kwa kuikataa kauli ya RPC, kama hawamjui vile.... 😃😃😃
 
Chawa siulikua unatetea kamanda wa polisi wa dodoma haya wamemtoa
sijatetea mtu popote gentleman,
na sibabaiki kusema ukweli kwamba hisia na huruma za mitandaoni katika mambo serious hasa ya kiuchunguzi na kimahakama dhidi ya manyanyaso na dhuluma za kingono alizopitia yule binti, kamwe hazitafua dafu katika kumpatia haki yake dhidi ya udhalilishaji alopitia,

by the way,
hayupo alietolewa popote,
ni vema ikafahamika vizuri kwamba mtumishi wa umma anaweza kubadilishwa kituo cha kazi kadiri inavyoonekana inafaa na kwa wakati wowote, ili kuimarisha na kuboresha utendaji wa taasisi au idara za umma na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi kwa haki, usawa na uwazi :pulpTRAVOLTA:

kuna tatizo lolote hapo gentleman?:DisGonBGud:
 
Back
Top Bottom