Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Polisi siyo sehemu salama tena
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo polisi wanajiunga watu waliofeli F4 na wavuta bangikuna vitu unafanyiwa mpaka unajiuliza hivi mimi n mtz kweli
bora mara 12Kwa hiyo ni bora njiani ukutane na wanyama wakali au wahuni lakini siyo hawa wa upande wa pili.
Pumbavu kabisa!
Rais Samia kuna siku alikuwa anasimulia madhira ya polisi aliyowahi kukutana nayo cha kushangaza anaongea then aoneshi dalili zozote za kuzitatua wakati nguvu na uwezo kwasasa anazoTulifanya kosa sana tulipoifanya kazi ya polisi ni ya watu wasio na akili. Jitu lisilo na akili huwezi kujua litafanya nini wakati gani.
Kufanyike maboresho ya jeshi la polisi ya kiwango cha juu. Kwanza kupima uwezo wao wa akili na uwezo wa kufundishika. Mtu asiyefundishika hata ukimpa mafunzo ya kiasi gani, haisaidii. Tunao polisi ambao akili yao ni kidogo sana na hivyo hawawezi kufundishika. Hawa wanatakiwa kufutwa kazi. Kama kuna kazi za kukata magogo na kuyanyanyua, labda wanaweza kufaa huko lakini siyo kazi zinazohitaji reasoning.
Kuna baadhi tunakutana nao humo barabarani, unamhoji sababu ya kukusimamisha anachoeleza ni upuuzi mtupu. Unaanza kumwelewesha anabaki ametumbua tu macho. Unashindwa kuelewa hata kule kwenye chuo chao wanafundishwa nini, na kama huwa wanapimwa kujua kiwango chao cha uelewa.
Rais Samia amelalamika sana juu ya mambo ya hovyo wanayofanya polisi, wakuu wao wamekuwa wanawapa maagizo kila wakati lakini wanawapa maelekezo watu ambao hawana uelewa wala maadili. Hawa hawawezi kubadilika.
Jeshi hili la polisi lililopo, kama tunataka liwe jeshi halisi la polisi na siyo genge la wanyang'anyi na wahunj, yumkini robotatu wanatakiwa kufukuzwa.
DuuhNaitwa Clement Nkwabi mkazi wa Geita. Napenda kukushirikisha suala la mdogo wangu Joel Raphael Nkwabi. Tarehe 15/12/2023 majira ya saa 2 usiku alienda kuangalia mpira lakini hakurudi. Tar.16 asubuhi mke wake alipigiwa simu na namba mpya. Kupokea ilikua sauti ya mumewe akimjulisha kuwa amelazwa hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kupigwa risasi na polisi walipotoka kuangalia mpira.
Alimuomba mkewe ampelekee nguo za kubadilisha kwani alizokuwa nazo zimechafuka damu sana. Mke alipokea taarifa hiyo kwa mshtuko na kuwajulisha ndugu wengine wa mume. Wakaenda hosptalini ambapo walikumkuta yupo chumba cha Emergency. Wakamkabidhi nguo na kumuuliza imekuwaje.
Akamjibu kuwa walipotoka kutizama mpira, walivamiwa na watu ambao hawakujitambulisha. Wakawataka walale chini. Wakahisi ni majambazi hivyo wakakimbia ili kujinusuru. Lakini watu hao wakafyatua risasi.
Wenzie walikimbia lakini yeye alijeruhiwa kiunoni. Risasi ikabaki mwilini. Akakimbizwa hospitalini na tar.16 akafanyiwa operation kuitoa. Mke aliambiwa mumewe kapigwa risasi na askari wa mali asili. Alipouliza sababu akaambiwa ataifahamu mahakamani.
Kesho yake mke alimpelekea chai mumewe lakini hakumkuta hospitalini. Alipouliza akaambiwa aende kituo cha Polisi Geita. Akaenda lakini hakumkuta. Akaambiwa labda amepelekwa kituo cha Kasamwa, nako hakumkuta. Akaambiwa ajaribu kituo cha Katoro, lakini huko nako hakumkuta.
Tarehe 19/12/2023 mkewe aakapigiwa simu na namba mpya. Ilikua sauti ya mumewe ikimueleza kwamba yupo kituo cha polisi Buseresere, akilalamika yupo kwenye maumivu makali kwani alitoroshwa hospitali baada tu ya operation. Alidai hakuna dawa yoyote aliyopewa zaidi ya kutolewa ile risasi, na huko mahabusu hapati matibabu yoyote. Kesho yake mkewe allienda Buseresere lakini polisi wakakanusha kumshikilia. Akarudi nyumbani bila matumaini.
Na tangu wakati huo hajasikia tena sauti ya mumewe. Ndugu zake hatujui kama yupo hai au amekufa. Hatujui kwanini alipigwa risasi? Kwanini alitoroshwa hospitali? Kwanini hakupewa haki ya matibabu? Hata kama ni mtuhumiwa si angetibiwa kwanza halafu ashtakiwe? Tunaomba utupazie sauti ili ndugu yetu aweze kupata haki yake. Au kama amekufa watupe maiti tuzike, tujue moja.
View attachment 2867106
Inasikitisha sana.Rais Samia kuna siku alikuwa anasimulia madhira ya polisi aliyowahi kukutana nayo cha kushangaza anaongea then aoneshi dalili zozote za kuzitatua wakati nguvu na uwezo kwasasa anazo
CCM na uovu ni pete na kidole. Bila CCM nchi itabaki salama na wananchi watabaki salama lakini vinginevyo tulie tu haijalishi nani yuko madarakani. Salama ya Polisi wetu ni CCM kubaki madarakani na ndio maana polisi wetu wanakuwa mstari wa mbele katika wizi wa kuraYale yale ya mwendazake yamerudi kwa kasi tena kasi ya ajabu
Mfano hii kesi wa kukamatwa hapo ni mkurugenzi wa hospitali, aeleze nani alimmtoroshabmgonjwa!Polisi waovu wasiachwe kujiamulia kufanya uovu wapendavyo. Kila mkoa liundwe jopo la majaji kiwe kikosi kazi cha haki na utengamano ili aliyeonewa na polisi/jeshi lolote apate pa kulalamikia na kudai hakiyake maana huwezi shtaki polisi Kwapolisi.