aada ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando kuwataka madereva kuyaondoa mabasi yao katika Stendi ya Magufuli kwani muda wa kukaa ndani ya stendi hiyo umeisha, Jeshi la Polisi limeanza kuondoa namba za magari kwa mabasi ambayo madereva wake hawajayaondoa.
Msando ametoa kauli hiyo leo Septemba 29, 2026 kutokana na mgomo wa madereva Stendi ya Magufuli na maeneo mengine nchini wakipinga mfumo mpya wa Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama barabarani kukata pointi kwenye leseni za udereva wanapofanya makosa ya barabarani.
Pia soma: Mgomo wa Madereva na Wafanyakazi wa mabasi wafanya mgomo Morogoro na Dar