Polisi Wapata Muonekano Mpya: Rais William Ruto Azindua Sare Mpya Kiganjo

Polisi Wapata Muonekano Mpya: Rais William Ruto Azindua Sare Mpya Kiganjo

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Rais William Ruto amezindua rasmi sare mpya za maafisa wa General Duty wa Kenya Police Service katika hafla iliyofanyika Ijumaa, Agosti 28, 2026, katika Kenya Police Training College, Kiganjo, Kaunti ya Nyeri.

1787985917361.jpeg

Chini ya muundo huo mpya, maafisa watavaa shati za rangi ya sky blue, suruali za dark blue pamoja na berets. National Police Service pia imeanzisha mavazi ya aina ya dress kwa maafisa wanawake kama sehemu ya mabadiliko hayo.

Mabadiliko hayo yanakuja baada ya maafisa wa polisi kukataa sare za sasa za navy blue wakati wa zoezi la public participation lililofanyika mwaka 2023. Inspector General Douglas Kanja amesema sare mpya zitaletwa kwa hatua kwa maafisa wa General Duty kote nchini, akisema pia zinatarajiwa kuongeza morale ya maafisa.

1787986134688.jpeg
Zaidi ya maafisa wapya 6,000 waliohitimu Kiganjo ndio waliokuwa wa kwanza kuvaa sare hizo katika pass-out parade, huku rollout pana ikitarajiwa kuanza Agosti 31.

Hata hivyo, maafisa wa General Service Unit (GSU) na Administration Police Service (APS) wataendelea kutumia sare zao za sasa.

Mabadiliko hayo pia yamefungua mjadala mpana kuhusu vipaumbele vya police reforms. Baadhi ya wakosoaji wamehoji kama kubadilisha sare kunapaswa kwenda sambamba na mageuzi makubwa zaidi kuhusu uwajibikaji, mazingira ya kazi na uhusiano kati ya polisi na wananchi.

a1cb39248c8b874a.jpeg

FotoJet (6) (1)-1787901528.jpg

7079-Screenshot 2026-08-28 101656.webp

1787985978161.jpeg

1787986022029.jpeg


1787986075309.jpeg

1787988119799.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: 650
Kenya wanabadilisha uniform za hawa watu kila mara
 
Back
Top Bottom