Polisi watii maelekezo ya Rais Samia, wawalinda CHADEMA

Polisi watii maelekezo ya Rais Samia, wawalinda CHADEMA

Joined
Sep 17, 2021
Posts
39
Reaction score
84
Tulioko Mwanza tumeshuhudia, Polisi wanatii maelekezo ya Rais Samia Suluhu anayetaka viongozi na wanachama wa upinzani wapewe ulinzi wa kutosha wakitimiza haki zao za Kidemokrasia.

Mika michache hapo nyumba tuliona viongozi wa upinzani wakikamatwa kila walipojaribu kusimama hadharani kufanya siasa, kinyume chake kina Mbowe walipokuja Mwanza, Polisi wamewaongoza kutoka uwanja wa ndege hadi hotelini, viongozi hao wanalindwa kila mahali.

Tunaamini watatumia vizuri uhuru huu, tunaamini watafanya siasa za kistaarabu kwa maslahi ya nchi.
 

Attachments

  • Jeshi la Polisi waongoza msafara wa viongozi wakuu asubuhi hii walipowasili uwanja wa ndege wa...mp4
    1.2 MB
Baada ya dalili zote za mkutano wa Chadema jijini Mwanza kudoda, katibu mkuu wa chama hicho bwana Mnyika ameonekana akizurula mitaani na masokoni akikagua bei ya vyakula na changamoto mbalimbali zinazowakumba wananchi, lakini namshauri ili apate angalau uungwaji mkono kidogo kutoka kwa wananchi wa Mwanza aende atembelee miradi yote waliyokuwa wakiipinga kama daraja la kigongo- busisi na ujenzi wa meli mpya ziwa victoria maarufu kama Mv Mwanza hapa kazi tu.
Akifika kwenye hiyo miradi awaombe wananchi wasimame kwa dakika moja kama heshima kwa mwasisi wa miradi hiyo hayati rais Magufuli na kisha awaombe radhi wana Mwanza kwa yote yaliyopita.
 
Asante kwa kuutangaza mkutano wa CHADEMA. Hongera CHADEMA.
 
Back
Top Bottom