Polisi watoa taarifa kifo cha Ulomi wasema alifariki kwa ajali ya pikipiki

Polisi watoa taarifa kifo cha Ulomi wasema alifariki kwa ajali ya pikipiki

Wakuu,

Hivi mnaona hii pattern ya watu kutekwa sasa hivi pamoja na reporting yake?

Wote (uliondoa wanasiasa mashuhuri) ni wafanyabiashara au wanahusishwa na biashara, na zote bwana Ayo amekuwa mstari wa mbele utafikiri anapewa headsup kuwa hii freshi unaweza kuripoti?!

Halafu tayari kulikuwa na taarifa ya Ulomi kupotea na kutafutwa na polisi, ina maana mifumo haisomani mwili wa mtu asiyetambulika unapopatikana toka tar 11 mpaka leo?🤔

Nawaza tu.... kuna ka kitu kanatengenezwa hapa.

Pia soma: Katibu wa Afya Hospitali ya Mwanyamala: Ulomi alipata ajali, mwili uliletwa December 11, 2024

View attachment 3178170
Ajali ya pikipiki ni instant crash na hutokea highway. Ina maana siku zote hizo toka ajali imetokea watu wasijue tu😄? Kasongo mbona wewooo??!
 
Naweka taarifa kama nilivyoikuta bila kuweka wala kuongeza neno langu hata moja.soma hapo chini👎

#HABARI Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa Daisle Simion Ulomi, aliyekuwa ameripotiwa kwamba amepotea, alifariki dunia baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia siku ya Desemba 11, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 16, 2024 na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro ambapo ameeleza kuwa tarehe 11 Desemba, 2024 Jeshi hilo lilipata taarifa ya kupotea kwake na ndugu hawakuwa wanampata kwenye mawasiliano ya simu, baada ya yeye kuondoka ofisini kwake Sinza na kudai anaelekea Temeke kufuatilia makontena yake ya biashara.

"Ulomi aliondoka eneo lake huku akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe, ufuatiliaji umefanyika kwa kushirikiana na ndugu na kubainika kuwa Ulomi alipelekwa kituo cha afya cha Makuburi Ubungo External mchana wa tarehe 11 Desemba, 2024 baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia, wasamaria wema walimsadia kumpeleka kwenye kituo hicho akiwa hajitambui na hakuwa na kitambulisho chochote," imeeleza taarifa ya Kamanda Muliro.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, " Baadae alipelekwa Mwananyamala hospitali na ikabainika tayari alikuwa amefariki na maiti yake kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo kama mtu asiyefahamika akisubiri kutambuliwa na ndugu, ndugu tayari wameutambua mwili huo ukiwa na majeraha maeneo mbalimbali ya mwili. Aidha, Pikipiki aliyopata nayo ajali pia imepatikana ikiwa imeharibika. uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na taarifa zaidi itatolewa,".

#EastAfricaTV
Screenshot_20241216-212832_1.jpg
 
Kuna mtu anasema alimpigia marehemu kuwa anafuatiliwa na Landcruiser
Alipotajiwa namba ikaonekana namba za gari hilo ni za gari la Kahama ila liko Ilala
Hiyo ajali ilitokea eneo gani na mashuhuda ni nani
Unachanganya desa, siyo huyu.
 
Polisi wangeacha tu kutoa hizi taarifa, bahati mbaya sana zinabakia mitandaoni kuna watu wanazifanyia analysis na kuzihifadhi.

Zitakuja kuwaumbua kuwa tulikuwa na jeshi la hovyo kumbe sio sahihi. Bora kukaa kimya tu.
 
Kuna mtu anasema alimpigia marehemu kuwa anafuatiliwa na Landcruiser
Alipotajiwa namba ikaonekana namba za gari hilo ni za gari la Kahama ila liko Ilala
Hiyo ajali ilitokea eneo gani na mashuhuda ni nani
Mkuu kila mkoa kuna usajili wa gari zake? Unaposema gari la Kahama unamaanisha nini?
 
Wakuu,

Hivi mnaona hii pattern ya watu kutekwa sasa hivi pamoja na reporting yake?

Wote (uliondoa wanasiasa mashuhuri) ni wafanyabiashara au wanahusishwa na biashara, na zote bwana Ayo amekuwa mstari wa mbele utafikiri anapewa headsup kuwa hii freshi unaweza kuripoti?!

Halafu tayari kulikuwa na taarifa ya Ulomi kupotea na kutafutwa na polisi, ina maana mifumo haisomani mwili wa mtu asiyetambulika unapopatikana toka tar 11 mpaka leo?🤔

Nawaza tu.... kuna ka kitu kanatengenezwa hapa.

Pia soma: Katibu wa Afya Hospitali ya Mwanyamala: Ulomi alipata ajali, mwili uliletwa December 11, 2024

View attachment 3178170
Taarifa ya polisi imejaa matobo.
 
Mkuu kila mkoa kuna usajili wa gari zake? Unaposema gari la Kahama unamaanisha nini?
Soma hizi thread humu imesema huyo marehemu alipigiwa simu na rafiki yake kuwa kuna landcruiser inamfuatilia ... ilipofuatiliwa namba ikaonekana mmiliki ni wa Kahama na gari hilo lilikuwa Ilala, walipolifuatilia mwenye gari akaonekana kushangaa kwakuwa hakuwa anajua lolote

Soma threads zote zinazohusu jambo hili humu utaona wameeleza
 
Yaani mfanyabiashara asiwe na kitambulisho? Tafuteni Taahira wa kumpa huu ufala wenu.., yaani ukakague kontena na usibebe ID yeyote?! Hata kusearch jina la mmliki wa pikipiki walishindwa?
 
Je hakuwa na vitambulisho?
Je hakuwa na simu mfukoni? Namba ya simu iliyo mfukoni ilikuwa na line iliyosajiliwa kwa jina lipi?
Je namba ya pikipiki aliyokuwa anaiendesha ilikuwa imesajiliwa kwa jina lipi?
Majibu yote yako humu toka tar 11
 
Yaani humu kuna watu mnauzi,sasa kama mke wake alihojiwa akasema aliondoka na pikipiki akiendesha mwenyewe we unakataa.
Ni kweli swali la kijinga, inawezekana kabisa alikua na usafiri mkubwa ila mida na kepusha foleni kijiweni sinza ukipa boda msimbazi anakuachia boda uende nayo hata moro.
 
Wakuu,

Hivi mnaona hii pattern ya watu kutekwa sasa hivi pamoja na reporting yake?

Wote (uliondoa wanasiasa mashuhuri) ni wafanyabiashara au wanahusishwa na biashara, na zote bwana Ayo amekuwa mstari wa mbele utafikiri anapewa headsup kuwa hii freshi unaweza kuripoti?!

Halafu tayari kulikuwa na taarifa ya Ulomi kupotea na kutafutwa na polisi, ina maana mifumo haisomani mwili wa mtu asiyetambulika unapopatikana toka tar 11 mpaka leo?🤔

Nawaza tu.... kuna ka kitu kanatengenezwa hapa.

Pia soma: Katibu wa Afya Hospitali ya Mwanyamala: Ulomi alipata ajali, mwili uliletwa December 11, 2024

View attachment 3178170
Kuna taarifa niliisoma jana ikielezea kuwa "ndugu wametqfuta vituo vyote vya polisi, hospitali zote na vyumba vyote vya kuhifadhia maiti." inamaana hilo neno "zote/vyote/kote" litakuwa lilitumika isivyo?
 
Iweke hiyo post hapa mkuu
Huyu aliyefariki ni yule inadaiwa alipigiwa simu na wakala wao wa mzigo wao kwamba anaitwa na TRA hvyo anatakiwa aende, akachukua boda yake kwenda ndiyo ikawa kimoja mpaka mwili wake kukutwa Mwananyamala, Yule ndugu Masawe anayedaiwa na Polisi kuuza gari la ndugu yake na kujiteka bado haijajulikana Ngoja tusubili Polisi watakuja na Sinema gani...
 
Wakuu,

Hivi mnaona hii pattern ya watu kutekwa sasa hivi pamoja na reporting yake?

Wote (uliondoa wanasiasa mashuhuri) ni wafanyabiashara au wanahusishwa na biashara, na zote bwana Ayo amekuwa mstari wa mbele utafikiri anapewa headsup kuwa hii freshi unaweza kuripoti?!

Halafu tayari kulikuwa na taarifa ya Ulomi kupotea na kutafutwa na polisi, ina maana mifumo haisomani mwili wa mtu asiyetambulika unapopatikana toka tar 11 mpaka leo?🤔

Nawaza tu.... kuna ka kitu kanatengenezwa hapa.

Pia soma: Katibu wa Afya Hospitali ya Mwanyamala: Ulomi alipata ajali, mwili uliletwa December 11, 2024

View attachment 3178170
Mimi nashindaga wilaya ya ilala kulala wilaya ya temeke ndani ndani huko..

Natumia barabara zote kilwa road ,keko road e.t.c kuanzia mwezi December nimeshuhudia ajar nyingi Sana za ma bodaboda..nyingi sanaaa Sanaa..

Ajari zipo na hazina kinga Ila bodaboda sio usafir wa kuaminika kabisa

Probably, olomi alipata ajar kweli ya bodaboda maana inasemwa ndio ulikua usafir wake ama ni spinning?! Who know
 
Tunaomba RB ya ajali ya tarehe 11 ambayo mtu alipoteza maisha.

MaAna taarifa ya polisi RB ni tarehe 12
 
Back
Top Bottom