Polisi: Watu 15 wafariki dunia kwa kusombwa na maji kuanzia Aprili 1 - 7

Polisi: Watu 15 wafariki dunia kwa kusombwa na maji kuanzia Aprili 1 - 7

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
TAARIFA KWA UMMA
Kuanzia Aprili 1,2024 hadi Aprili 7,2024 watu 15 wamefariki dunia kutokana na kusombwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha, wengine wakiwa wanaogelea, wengine wakiwa wanavuka maeneo ambayo maji yanatiririka kwa kasi na wengine kutokana na kutumbukia kwenye mashimo/madimbwi yaliyojaa maji. Miongoni mwa watu hao watoto ni 12 na watu wazima ni 3.

Matukio hayo yametokea katika Wilaya mbalimbali hapa nchini. Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa mtu mmoja mwanaume miaka 18, alisombwa na maji ya mvua yaliyokuwa yakitokea milimani wakati akijaribu kuvuka daraja Aprili 1,2024. Tarehe hiyo hiyo katika Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi watoto 2 wote wakiwa na miaka 12 walikufa maji baada ya kusombwa na maji ya mvua.

Aprili 2,2024 mwanaume mmoja wa miaka 28, huko katika Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe alikufa baada ya kufukiwa na udongo ulioporomoka kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha.

Aprili 3,2024 huko Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga, mtoto wa miaka 8 alikufa maji wakati akiogelea.

Mkoani Pwani Aprili 3,2024 Wilaya ya Mkuranga mtoto mmoja wa miaka 10 alifariki Dunia akiogelea mto Mzinga na Wilaya ya Kibaha mtoto wa miaka 12 alikufa maji yaliyokuwa yamejaa katika bonde la mpunga.

Aprili 5,2024 mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 55 huko Wilayani Babati moani Manyara alikufa maji baada ya kutumbukia kwenye shimo lenye maji.

Aidha, Aprili 7,2024 huko katika Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya watoto 5 wenye umri kati ya miaka 5 na 6 walifariki dunia baada ya kuzama kwenye dimbwi lilojaa maji ya mvua wakiwa wanaogelea.

Pia tarehe hiyo hiyo huko Mkoani Geita watoto 2 wenye umri wa miaka 9 na 14 walifariki dunia baada ya kusombwa na maji ya mvua yaliyokuwa yanatiririka kutoka milimani wakitoka kuokota kuni.


GKpSpLyWUAAqX-d.jpg
 
Back
Top Bottom