Polisi wavamia Ofisi za ACT-Wazalendo Vingunguti alizokuwepo Zitto Kabwe

Polisi wavamia Ofisi za ACT-Wazalendo Vingunguti alizokuwepo Zitto Kabwe

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Jeshi la Polisi @tanpol wamevamia Ofisi ya ACT -Wazalendo Kata ya Vingunguti ili kumkamata Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe aliyekuwa Ofisini hapo kuratibu Maandamano kwa Njia ya Buguruni kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi
===

27F74D8B-90CE-4F6B-899F-9E8F6D4D8FBF.jpeg
 
Hii ni hatari kubwa!

Ndio maana wazungu huwa wanatudharau, Utakuta jambo la kufanya kistaarabu na kwa kutumia muda na nguvu ndogo tu, Sisi waafrika tunahangaika vibaya mno na hata kutumia rasilimali nyingi isivyostahili! Donald Trump aliwahi kuwaponda viongozi wa Afrika akisema ....Give them weapons and they will kill themselves instead of fighting their enermies!

Hili tumeliona hata kwa serikali na CCM, wametumia nguvu na gharama kubwa sana za uchaguzi wakati kumbe mkononi walishaandaa njia ya mkato ya kushinda uchaguzi kwa asilimia zote! Wastage of time and resources!

After all; jesh la polis wanapaswa kufahamu kuwa kuitisha maandamano sio kosa bali kosa ni kuandamana bila kibali. Pia kosa la kuandamana bila kibali adhabu yake sio kupigwa mabomu wala au kudhuriwa kwa namna yoyote bali, adhabu yake ni kushtakiwa na mahakama ndio itowe uamuzi kama wahusika wana hatia au lah!

Kinyume cha hapo ni kujichukulia sheria mkononi huku jeshi lenyewe likijuwa fika kuwa katika suala zima la wananchi kuandamana, jukumu la jeshi sio kutoa kibali cha kuruhusu au kutoruhu maandamano bali ni kutoa ulinzi kwa waandamanaji!
 
Wasituchoshe watz, nia yao ni kuvuruga amani. Kama wanaona wameonewa kwenye uchaguzi waende kwa mabeberu washitaki, tuone kama watanyima misaada.

Kuhamasisha maandamano ni kuleta taharuki isiyo na sababu kwa wananchi.
Mbona hamuongelei haki, kitu ambacho ni moja ya misingi ya katiba ya nchi?
 
Wananchi wamewakataa kabisa , wanataka kuichafua njia nyingine kuichafua nchi, asiyekubali kushindwa si mshindani wanadhani wananchikuwa hawajawaelewa ndio hata maandamano wananchi hawataki.

Asiyekubali kuibiwa ni mshindani wa kweli. Ila mwizi!
 
Swali la Msingi.

Hivi mtu aliyekupigia kura ambayo unasema imeibiwa umwambie aandamane halafu ashindwe kuandamana ina make sense kweli?? La hasha nina wasiwasi yamkini vyama vya upinzani wao ndio wameiba hizo kura walizozipata. Hakuna mtu anayeibiwa ahalafu ashindwe kutafuta kitu chake kilichoibiwa.

Tanzania Hatutaki Maandamano
 
Kwani wanaandamania wapi? Mbona siwaoni na niko hapa Kibo, nimepita hapo kwa Tundu Lissu pia, naona pako kimya!
 
Back
Top Bottom