Hii ni hatari kubwa!
Ndio maana wazungu huwa wanatudharau, Utakuta jambo la kufanya kistaarabu na kwa kutumia muda na nguvu ndogo tu, Sisi waafrika tunahangaika vibaya mno na hata kutumia rasilimali nyingi isivyostahili! Donald Trump aliwahi kuwaponda viongozi wa Afrika akisema ....Give them weapons and they will kill themselves instead of fighting their enermies!
Hili tumeliona hata kwa serikali na CCM, wametumia nguvu na gharama kubwa sana za uchaguzi wakati kumbe mkononi walishaandaa njia ya mkato ya kushinda uchaguzi kwa asilimia zote! Wastage of time and resources!
After all; jesh la polis wanapaswa kufahamu kuwa kuitisha maandamano sio kosa bali kosa ni kuandamana bila kibali. Pia kosa la kuandamana bila kibali adhabu yake sio kupigwa mabomu wala au kudhuriwa kwa namna yoyote bali, adhabu yake ni kushtakiwa na mahakama ndio itowe uamuzi kama wahusika wana hatia au lah!
Kinyume cha hapo ni kujichukulia sheria mkononi huku jeshi lenyewe likijuwa fika kuwa katika suala zima la wananchi kuandamana, jukumu la jeshi sio kutoa kibali cha kuruhusu au kutoruhu maandamano bali ni kutoa ulinzi kwa waandamanaji!