Polisi wamejaribu kuzuia baadhi ya waandamanaji kuingia katika eneo la biashara la katikati ya jiji la Nairobi (CBD) leo Jumatatu, Oktoba 26, 2026, huku mvutano ukishuhudiwa barabarani.
Video iliyorekodiwa jijini inaonyesha baadhi ya waandamanaji wakikabiliana na maafisa wa polisi katika kile kinachoonekana kuwa mapambano ya kukimbizana barabarani.
Maandamano hayo yaliandaliwa na Coalition of Human Rights Defenders kupinga kupanda kwa bei ya mafuta na gharama ya maisha. Waandaaji walikuwa wametangaza wiki iliyopita kuwa maandamano yangeanzia Kimathi Street na kuelekea Ikulu ya Nairobi.
Hatua hiyo inafuatia ongezeko la bei za mafuta kwa kipindi cha Oktoba na Novemba, huku bei ya petroli Nairobi ikifikia KSh 226.96 kwa lita na dizeli KSh 227.76 kwa lita.
Waandaaji walitarajia washiriki kati ya 500 na 900 na kuahidi kuwa maandamano hayo yangekuwa ya amani.
Je, una maoni gani kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta na hatua za polisi wakati wa maandamano?.