Polisi wengi wanatengwa na Jamii na kuishi kwa msongo mawazo

Jeshi libadilishwe liitwe police service, badala ya police force naona ndio kiini cha mahusiano mabaya na raia. Polisi wamekuwa ni watu wa madili wanaangalia fedha kuliko kutenda kwa haki.
 
Kwa hiyo maaskari wote wanatokea koo za kiaskari zisizokuwa na mchanganyiko wa watu.

Ina maana maaskari wote wamekosana na classmates wao na wakipata shida hawatoi msaada.

Hizo ni wrong assumptions tu na kama depression wanazo kama watu wanaofanya kazi katika kada zingine
 
Utafiti wangu mdogo umebaini Watanzania wengi hawana urafiki na polisi, yaani ule urafiki kama wa mtu na mshkaji wake, mfano kupigiana simu kujuliana hali, kutembeleana, kubadilishana mawazo, kushirikiana katika biashara na kupeana michongo.

Mapolisi wengi wanakuwa na urafiki wao kwa wao na kwavile wengi hukutana kazini tu tena ukubwani, basi urafiki wao huwa wa juu juu tu. Vipo visa kadhaa vya askari polisi kuchukua hatua za ajabu kutokana na msongo wa mawazo.

Niliwahi kuzungumza na mkuu mmoja wa FFU katika mkoa fulani akaniambia anaongoza vijana walevi, wagomvi, wenye madeni na mzigo mkubwa wa familia, alinieleza vijana wake ni kama wanaishi kwenye dunia yao.

Nilivyo muuliza hatua gani huzichukua kuwasaidia akasema huwa anajitahidi kuwasaidia wale walio katika hali mbaya zaidi kwa kuwapangia malindo kwenye taasisi za fedha au sehemu nzuri nzuri ili wapate posho ya ziada, pia huwa anawafariji kwa neno la Mungu.

Anasema laiti raia wangekuwa na huruma na upendo kwa polisi huenda jamii ingefuta uhalifu.

Mnaonaje tukianza utaratibu wa kuwatembelea polisi kwenye kota zao, kupiga nao ma stori, kuoa watoto wao, mnadhani itapunguza hizi kelele huku mtaani?
Wanajidai kwa rushwa, dhuluma, urafiki na wezi, vibaka na Majambazi, wavuta bangi, kutembea na wake za watu, kufadhili uhalifiu. Police si kiumbe wa kumuonea huruma kila siku wanafanya ukatili, Uonevu, na dhuluma za kila aina.

Ingefaa sana kama Mungu akawapa adhabu kubwa sana hapa Duniani hasa ukichaa na ukilema.
 
We fala kweli, kawatembelee mwenyewe. Hao jamaa hawafai kabisa, sitaki mazoea nao kabisa..
 
hakuna jamii iliyowatenga polisi,polisi wanaishi mtaani,wanaugua wanatibiwa,wanakopa wakikosa pesa,na hutoa misaada wanapohitajika.

shutuma walizo nazo ndizo wanachi wanalalamika nazo,bahati mbaya mwananchi yuko nafasi mbaya anakosa chaguo wakati huo unapofika zaidi ya kutekeleza anachoagizwa na polisi.
kwa kiswahili chepesi ni kwamba utamhitaji polisi wakati ambao huna chaguo jingine,hii huwafanya nao kutokunyenyekea watu.

msongo wa mawazo walio nao baadhi yao,unatokana na swala la kipato duni,,maisha mabovu,kazi ngumu yenye hatari kubwa na shinikizo kubwa kutoka kwa vingozi wasio na akili,malalamiko mengi kutoka kwa wateja wao yaani wananchi.
 
Wanajidai kwa rushwa, dhuluma, urafiki na wezi, vibaka na Majambazi, wavuta bangi, kutembea na wake za watu, kufadhili uhalifiu. Police si kiumbe wa kumuonea huruma kila siku wanafanya ukatili, Uonevu, na dhuluma za kila aina.

Ingefaa sana kama Mungu akawapa adhabu kubwa sana hapa Duniani hasa ukichaa na ukilema.
Mungu sio seleman wa mbosso.

unadhani wenye matendo hayo ni polisi peke yao!!!
 
Utafiti wangu mdogo umebaini Watanzania wengi hawana urafiki na polisi, yaani ule urafiki kama wa mtu na mshkaji wake, mfano kupigiana simu kujuliana hali, kutembeleana, kubadilishana mawazo, kushirikiana katika biashara na kupeana michongo.

Mapolisi wengi wanakuwa na urafiki wao kwa wao na kwavile wengi hukutana kazini tu tena ukubwani, basi urafiki wao huwa wa juu juu tu. Vipo visa kadhaa vya askari polisi kuchukua hatua za ajabu kutokana na msongo wa mawazo.

Niliwahi kuzungumza na mkuu mmoja wa FFU katika mkoa fulani akaniambia anaongoza vijana walevi, wagomvi, wenye madeni na mzigo mkubwa wa familia, alinieleza vijana wake ni kama wanaishi kwenye dunia yao.

Nilivyo muuliza hatua gani huzichukua kuwasaidia akasema huwa anajitahidi kuwasaidia wale walio katika hali mbaya zaidi kwa kuwapangia malindo kwenye taasisi za fedha au sehemu nzuri nzuri ili wapate posho ya ziada, pia huwa anawafariji kwa neno la Mungu.

Anasema laiti raia wangekuwa na huruma na upendo kwa polisi huenda jamii ingefuta uhalifu.

Mnaonaje tukianza utaratibu wa kuwatembelea polisi kwenye kota zao, kupiga nao ma stori, kuoa watoto wao, mnadhani itapunguza hizi kelele huku mtaani?
Watembelee wewe mimi hata lift siwapi
 
hakuna jamii iliyowatenga polisi,polisi wanaishi mtaani,wanaugua wanatibiwa,wanakopa wakikosa pesa,na hutoa misaada wanapohitajika.

shutuma walizo nazo ndizo wanachi wanalalamika nazo,bahati mbaya mwananchi yuko nafasi mbaya anakosa chaguo wakati huo unapofika zaidi ya kutekeleza anachoagizwa na polisi.
kwa kiswahili chepesi ni kwamba utamhitaji polisi wakati ambao huna chaguo jingine,hii huwafanya nao kutokunyenyekea watu.

msongo wa mawazo walio nao baadhi yao,unatokana na swala la kipato duni,,maisha mabovu,kazi ngumu yenye hatari kubwa na shinikizo kubwa kutoka kwa vingozi wasio na akili,malalamiko mengi kutoka kwa wateja wao yaani wananchi.
Ujinga wao ndiyo unawatesa
 
Mapolisi wengi wanakuwa na urafiki wao kwa wao na kwavile wengi hukutana kazini tu tena ukubwani, basi urafiki wao huwa wa juu juu tu. Vipo visa kadhaa vya askari polisi kuchukua hatua za ajabu kutokana na msongo wa mawazo.
Nilishawahi ambiwa nitalala lockup na mkuu wa kituo Ila polisi anaenifahamu rafiki yangu akaja kunitoa na kuniambia atazungumza na mkuu wa kituo hilo suala nimwachie yeye maana mkuu wa kituo alikua anataka nimpe RUSHWA kubwa ili aniachie nikagoma
 
Back
Top Bottom