Pre GE2025 Polisi yaanza uchunguzi kufuatia tukio la utekaji wa kijana aliyechoma picha ya Rais

Pre GE2025 Polisi yaanza uchunguzi kufuatia tukio la utekaji wa kijana aliyechoma picha ya Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
1722834641961.png

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeanza uchunguzi wa kubaini watu wasiojulikana wanaodaiwa kumteka Shadrack Chaula (24), mkazi wa Kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe.

Chaula anadaiwa kutekwa na watu hao ikiwa ni takribani siku 20 zimepita tangu alipotoka Gereza la Ruanda Mkoa lililoko mkoani Mbeya, alipokuwa amehukumiwa kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya Sh5 milioni.

Baada ya kifungo hicho kilichotolewa Julai 4, 2024, wadau mbalimbali waliendesha michango mitandaoni na kufanikiwa kupata kiasi hicho cha fedha na Julai 8, 2024 ililipwa na kuachiwa.

Agosti 3, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC), Benjamin Kuzaga amesema kimsingi wanafuatilia uwepo wa tukio hilo.

Pia soma > Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo

"Tayari tumeanza uchunguzi ili kubaini ni kweli alitekwa kama mitandao ya kijamii ilivyoripoti maana wapo waliomchangia kutoka gerezani," amesema.

Mmoja wa viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Kijiji cha Ntokela ya Ndato, aliyeomba hifadhi ya jina lake, amesema wanashindwa kuelewa matukio hayo yako vipi dhidi ya familia ya huyo kijana.

"Alikuwa magereza alipotoka kama viongozi hatukujua na tulisikia tu kaenda Dar es Salaam, leo lingine limeibuka kama katekwa kweli wazazi wake walishindwa kutoa taarifa ili tufuatilie," amesema kiongozi huyo.

Pia soma: Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesema jambo hilo lina mkanganyiko, kama kuna jambo nyuma ya pazia watafuatilia kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, kama ni masuala ya kisiasa yanatumika kupitia kwake itaeleweka maana ni kipindi cha kuelekea uchaguzi," amesema.

Mwananchi

---
Baba mzazi wa Shedrack asimulia mwanaye alivyotekwa

Kufuatia taarifa za kutekwa kwa Shadrack Chaula, akizungumzia tukio hilo Baba Mzazi, Mzee Yusuph Chaula amesema kuwa ni kweli mwanae alichukuliwa kwa nguvu na Watu wasiojulikana ambao walikuwa na gari, tofauti na alivyokamatwa mara ya kwanza kabla ya kufunguliwa kesi.

"Mara ya kwanza alikamatwa na askari, sasa hao walikuja na gari ambayo sio ya Serikali harafu ni watu ambao hawakutumia taratibu za kumkamata Mtu, basi nasikia wakamchota kinguvunguvu na kumuingiza kwenye gari na kuondoka naye"

Akizungumza na JamiiForums amesema walitoa taarifa kwenye kituo cha Polisi Kiwila, ambapo amesema baada ya kutoa taarifa hiyo zilifanyika taratibu wakaitwa Ofisa Upelelezi Wilaya (OC CID) kwenda Tukuyu ambapo walihojiwa namna alivyotekwa.

Amesema kuwa wamefanya jitihada za kujua wapi alipo lakini mpaka sasa hawafahamu alipo, ambapo amesema kuwamujibu wa taarifa walizopatiwa na Jeshi la Polisi ni kuwa Chaula wamekosekana kwenye vituo vya Polisi ambako wamefuatilia.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga kwa ajili ya kutaka kujua madai hayo, baada ya kujitambulisha kwake alisema "Subiri nipo msibani"

Itakumbukwa Chaula hivi karibuni alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kuchoma picha inayodaiwa kumuonesha Rais Samia. Hata hivyo alishtakiwa na kukutwa na mashtaka lakini iliripotiwa kuwa alitimiza masharti ya hukumu na kuachwa huru.
 
Back
Top Bottom