Polisi yakamata mtandao wa mauji nchini yafukua miili 7 Dodoma na 3 singida ,watekaji wadakwa

Akili za baadhi ya wafuasi wa CDM saa zingine dah. Yaani kwa mtazamo wao the world revolves around them.

Kwenye fikra zao jeshi la polisi halina kazi nyingine zaidi ya kuwalinda wananchi na watanzania wote wanawaza siasa.

Watu wamepoteza ndugu zao, unaambiwa miili saba imefukuliwa na genge la mashetani linalokamata na kuuwa watu kwa imani za kishirikana.

Mungu tu anajua bila ya kushikwa wangeuwa watu wangapi wengine. Badala ya kupongeza jeshi la polisi kwa kazi waliyofanya na kuwa na huruma na familia na jamaa waliopoteza ndugu na jamaa zao.

Unasoma post hii Ina maana gani kama sio polisi kutaka kuzima habari zao. Yaani polisi hawana kazi ya kulinda wengine. Just appaling hata kusoma comments zao.
 
Zitaje kazi za polisi zaidi ya kulinda raia na usalama wao boss WANACHADEMA HUENDA WAKAKUELEWA
 
Zitaje kazi za polisi zaidi ya kulinda raia na usalama wao boss WANACHADEMA HUENDA WAKAKUELEWA

Soma ☝️kaongeze na penal code

Halafu ushasema moja wapo ni kulinda raia na usalama. Kichwa chao raia ni wanachadema tu.

Vifo na uhalifu mwingine autakiwi kufanyiwa kazi na wakitoa report za uhalifu mwingine wakati wao wana hisia zao (au accusation zao) basi lengo la taarifa ya polisi ni kupotezea habari zao (ambazo wanadhani ni priority ya kila mtanzania).

Wana akili za kitoto sana wafuasi wa CDM ni mimi-mimi-mimi. Hawana empathy kabisa na shida za wengine kwenye jamii zinazohitaji muda wa polisi pia.
 
kama watu waliuliwa hivi na Polisi wakawa hawajui basi hatuna Jeshi la polisi.

kwa sababu kazi yao ni kuzuia Uhalifu sio kushughulika na madhara yamatukio ya uhalifu huo
Matokeo ya kudharau taarifa za wananchi wanapokuja kutoa taarifa kuhusu kupotea kwa ndugu zao Polisi huwa hawachukui hatua haraka watakwambia hadi masaa 24 yapite, ndipo uende kuripoti polisi. This is impossible.
 
Serial killers kill for the sake of killing
 
Matokeo ya kudharau taarifa za wananchi wanapokuja kutoa taarifa kuhusu kupotea kwa ndugu zao Polisi huwa hawachukui hatua haraka watakwambia hadi masaa 24 yapite, ndipo uende kuripoti polisi. This is impossible.
Na wananchi wamesema walikuwa wakiripoti polisi anakamatwa na kuachiwa
 
Polisi hii taarifa yenu inatakiwa iende mbali zaidi,ni kweli vifo vinahusihwa na ushirikina lakini hamtuambii ni kwanini huu ushirikina unafanyika na ni kwaajili ya kupata nini ,na nani anawatuma hawa watu,hawa watu inawezekana kabisa kuna watu wanawatumia kwa manufaa yao binafsi......
 
kama watu waliuliwa hivi na Polisi wakawa hawajui basi hatuna Jeshi la polisi.

kwa sababu kazi yao ni kuzuia Uhalifu sio kushughulika na madhara yamatukio ya uhalifu huo
Hata kikosi cha intelijensia nacho kilikuwa hakijui yote jhayo tangu June?
 
Kombo Mbwana, mwanachama wa Chadema Tanga, alifichwa na jeshi la polisi kwa zaidi ya siku kumi, pamoja na kutafutwa vituo vyote vya polisi hawakuambiwa alipo.

Mwisho wa siku ni kamanda wa polisi mkoa wa Tanga ndie akatoa mwenyewe taarifa ya kumshikilia, ukiona kitu kimeandikwa ujue mwandishi ana uhakika wa 100% wa kile anachoandika.

This is beyond kulinda raia na mali zao, kazi nyingine ya polisi imeshathibitika ni kuilinda CCM na interest zake.
 
je hakuna mpinzani hapo au mwanaharakati wa kuipinga serikali? uskute jamaa wameongezewa na maiti zingine
 
Hongera jeshi kwa kazi nzuri sana

USSR
kama watu waliuliwa hivi na Polisi wakawa hawajui basi hatuna Jeshi la polisi.

kwa sababu kazi yao ni kuzuia Uhalifu sio kushughulika na madhara yamatukio ya uhalifu huo
Mimi binafsi nitakuwa mtu wa mwisho kabisa kuja kuwaamini hawa Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi na Tiss wana kazi kubwa ya kujisafisha kutokana na tope zito walilojipaka wao wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…