Polisi yakiri kumshikilia Kada wa CHADEMA Kombo aliyedaiwa kutoweka kwa siku 29!

Zikiwa zimepita siku 29 tangu kada wa Chadema, wilayani Handeni mkoani Tanga, Kombo Mbwana (29) adaiwe kupotea, hatimaye leo Julai 14, 2024 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zacharia Bernard amesema wanamshikilia kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Julai 14, 2024 Kaimu kamanda Benard amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vifaa vya kielektroniki pamoja na laini za simu za mitandao mbalimbali zisizo na usajili wake katika kutekeleza uhalifu huo kinyume cha sheria za nchi.

Pia soma: Mke wa Kombo alivyosimulia jinsi Kombo alivyotekwa na watu wasiyojulikana na juhudi zilizofanyika kumtafuta Julai 2, 2024

Amesema upelelezi wa matukio hayo umefikia hatua nzuri na wakati wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Anadaiwa kutenda makosa hayo kwenye mikoa tofauti na kuongeza Jeshi hilo linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo ni kosa kisheria.

View attachment 3042263
Kombo Mbwana

Hata hivyo, Julai 2, 2024 Mwananchi lilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando kuhusu madai hayo ya kupotea kwa Kombo ambapo alisema tukio hilo lipo kwenye uchunguzi chini ya Jeshi la Polisi na amewaomba wanafamilia na wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikilishughulikia.

“Serikali haijawahi kushindwa jambo, nawaomba tuwe watulivu,” alisema Msando.
Mlishangilia kifo Cha Magufuli kuwa ndiye aliyekuwa anawateka, Sasahivi mnakula kuku kwa mrija dhalimu hayupo, sijui Sasahivi hizi lawama mnamtwisha nani, Maana mama yenu kipenzi hawezi fanya mambo hayo, Makonda jiandae maana kila baya nchi hii lilifanywa Magufuli na Makonda, Magufuli hayupo kabaki Makonda.
 
Zikiwa zimepita siku 29 tangu kada wa Chadema, wilayani Handeni mkoani Tanga, Kombo Mbwana (29) adaiwe kupotea, hatimaye leo Julai 14, 2024 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zacharia Bernard amesema wanamshikilia kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Julai 14, 2024 Kaimu kamanda Benard amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vifaa vya kielektroniki pamoja na laini za simu za mitandao mbalimbali zisizo na usajili wake katika kutekeleza uhalifu huo kinyume cha sheria za nchi.

Pia soma: Mke wa Kombo alivyosimulia jinsi Kombo alivyotekwa na watu wasiyojulikana na juhudi zilizofanyika kumtafuta Julai 2, 2024

Amesema upelelezi wa matukio hayo umefikia hatua nzuri na wakati wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Anadaiwa kutenda makosa hayo kwenye mikoa tofauti na kuongeza Jeshi hilo linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo ni kosa kisheria.

View attachment 3042263
Kombo Mbwana

Hata hivyo, Julai 2, 2024 Mwananchi lilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando kuhusu madai hayo ya kupotea kwa Kombo ambapo alisema tukio hilo lipo kwenye uchunguzi chini ya Jeshi la Polisi na amewaomba wanafamilia na wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikilishughulikia.

“Serikali haijawahi kushindwa jambo, nawaomba tuwe watulivu,” alisema Msando.
Siku 29 bila kumfikisha mahakamani?... Kazi kweli kweli
 
nadhani ni baada ya mtoa maelekezo kutumbuliwa na kupangiwa kazi nyingine. polisi hawawezi kuteka watu bila DG wa teeth. samia kastuka mapema sana kaona upunguani wa jiwe umerudishwa ameamua kuadjust watu wake manake wanamuaibisha. nina uhakika issue ya sativa maza hakuifurahia, either kuona amepona kifo au kuona ametekwa na kuaibika ndio maana aliamua kumchangia hadi pesa.
DG hafanyi kitu bila maelezo. Issue ya Sativa ilisababisha watu wapigwe chini sababu wali under perform.
 
Ni kutukana wananchi kama mlinda na mtunza sheria akivunja sheria huku akiwa amevaa uaskali... uvunjifu wa katiba kuinea raia.... Kila raia hata hatia hadi pale atakapo thibitika ana hatia ndipo sheria inachukua mkondo wake... Majeshi hayatakiwi kuendeshwa kwa mihemko binafsi... ndio maana kina waziri wa Ardhi iliyoumbwa na Mungu anafikia kusema OCD mchukue huyu... mihemko tu... ni kukosa hadhi ya uongozi na kujigeuza mtawala... tizama mtu kama silaa anafaida gani bora tu wakoloni miji ilipangika..

Ukajibikaji mkuu wa polisi aatakiwa achukuae hatua kwa wanajeshi wasio na maadili pengine hawana akili mental diseases zipo jamani walishasema kati ya watanzania 10 mmoja ni kichaa
 
Zikiwa zimepita siku 29 tangu kada wa Chadema, wilayani Handeni mkoani Tanga, Kombo Mbwana (29) adaiwe kupotea, hatimaye leo Julai 14, 2024 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Zacharia Bernard amesema wanamshikilia kwa tuhuma za makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Julai 14, 2024 Kaimu kamanda Benard amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia vifaa vya kielektroniki pamoja na laini za simu za mitandao mbalimbali zisizo na usajili wake katika kutekeleza uhalifu huo kinyume cha sheria za nchi.

Pia soma: Mke wa Kombo alivyosimulia jinsi Kombo alivyotekwa na watu wasiyojulikana na juhudi zilizofanyika kumtafuta Julai 2, 2024

Amesema upelelezi wa matukio hayo umefikia hatua nzuri na wakati wowote mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Anadaiwa kutenda makosa hayo kwenye mikoa tofauti na kuongeza Jeshi hilo linatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo ni kosa kisheria.

View attachment 3042263
Kombo Mbwana

Hata hivyo, Julai 2, 2024 Mwananchi lilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando kuhusu madai hayo ya kupotea kwa Kombo ambapo alisema tukio hilo lipo kwenye uchunguzi chini ya Jeshi la Polisi na amewaomba wanafamilia na wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikilishughulikia.

“Serikali haijawahi kushindwa jambo, nawaomba tuwe watulivu,” alisema Msando.
Sheria ya ukamataji ipo hivyo?.
Natamani niwe IGP.
 
Back
Top Bottom