KWELI Polisi yakiri watu 45 wafariki Dar wakati wa kumuaga hayati Magufuli

KWELI Polisi yakiri watu 45 wafariki Dar wakati wa kumuaga hayati Magufuli

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Chanzo cha habari gazeti la the The Citizen la leo Machi 30, 2021.

Dunia ina mambo mengi sana na vichekesho vingi sana, Hawa Jamaa Polisi mara ya kwanza waliogopa kutangaza.

Hongereni Polisi kwa kutoa ukweli ingawa mmechelewa mlikuwa mnasoma upepo.
1658211327963.png
 
Tunachokijua
Jeshi la polisi limesema watu 45 walifariki kufuatia mkanyagano Machi 21, 2021 jijini Dar-es-Salaam katika tukio la waombolezaji kutoa heshima ya mwisho kwa John Pombe Magufuli ambapo familia moja inayoishi eneo la Kimara ilipoteza watu 5 yaani mama na watoto wake wanne.

Kamanda wa kanda ya jiji la Dar-es-Salaam, Lazaro Mambosasa Machi 21, 2021 alisema kwamba kulikuwa na umati mkubwa wa watu waliotaka kuingia katika uwanja wa michezo wa Uhuru ambao ulitumika kuuga mwili wa Rais Magufuli na baadhi yao walikosa subira na kujaribu kuingia kwa mabavu katika uwanja huo na hatimae kusababisha hali ya mkanyagao.

Kadhalika kamanda huyo wa jeshi la polisi amesema watu wengine wengi walijeruhiwa lakini wengi waliruhusiwa kuondoka hospitali.

Aliyekuwa Rais wa Tanzania Dk John Joseph Pombe Magufuli alifariki dunia machi 17, 20221 kutokana na matatizo ya Moyo na alizikwa tarehe 26 mwezi 2021 nyumbani kwao Chato mkoani Geita.
Back
Top Bottom