Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chadema watulize vishundu kwanza mamlaka zifanye kazi yake. Hata wangeandamana miezi mwisho wa siku ni haohao Polisi watakaotakiwa kutafuta na kukamata watuhumiwa na ni hizohizo Mahakama za Tanzania ambazo wanadai hawaziamini zitakazoshughulikia.

Waache siasa kwenye sheria
Kishundu anacho mamako??
 
Chadema wanataka kuja Dar kuandamana. Wanataka kuja kutoka mikoani kwa makumi na mamia .
Wakiruhusiwa kuja Dar litakuwepo tatizo gani?
Kumbuka Kennedy aliruhusu Martin Luther King jr kuwaongoza Wanegro elfu kumi kwenda Washington DC.
Halafu baadaye wakashindwa kuvumilia wakamuua Martin Luther King jr. We know who killed him Lakini we don't want to shorten our life span.
Lakini hofu yao ilikuwa ikiwa riot itatokea watakuwa hawana askari wa kutosha kuizuia.
Lakini hawa Chadema wanataka kufanya peaceful march,kwa nini wasiruhusiwe?
 
Uko sahihi kabisa kwa swali lako kwanini wasiruhusiwe?
Swali lingine la muhimu kabisa ni lile alilouliza Kikeke, kwanini hawakujitokeza kuzungumzia utekaji badala yake wakasubiri hadi kifo?

Kwanini katibu mkuu aliogopa kupokea simu ya mbowe kuhusu kifo cha kibao ?
Nini kilimshtua zaidi ilihali taarifa za utekaji walikuwa nazo?
Au lengo lilikuwa kumtesa kidogo ili wapate walichohitaji kutoka kwake badala yake waliotumwa wakasababisha mauaji?
Ni nani anayewatuma hao watekaji wenye kujivika upolisi?

Ipo siku haya yote yatafika mwisho!
 
Stori za mitego hizi
 

Attachments

  • 2B1A5CC4-DEC3-4E30-82E6-7EFD28561DFA.jpeg
    2B1A5CC4-DEC3-4E30-82E6-7EFD28561DFA.jpeg
    50.8 KB · Views: 2
Huyo mjinga hajui hata vitu vidogo sana vya kisheria.

Kwani kuna mtu ametaka kujua kama polisi wanataka maandamano yafanyike au yasifanyike?

Wao wasubirie kupewa taarifa. Halafu waseme kama wana polisi wa khsimamia maandamano au hawana. Kama hawana, CHADEMA watengeneze utaratibu wao wa kuhakikisha maandamano yanakuwa ya amani, au wasuburie siku polisi watakapokuwa na nafasi ya kusimamia maandamano.

polisi, jielimisheni, mjue angalao kujua sheria zinasemaje. Utasemaje unasimamia sheria wakati hata sheria zenyewe huzijuo?Mamlaka ya kuzuia maandamano ya amani nani amewapa Polisi? Polisi wetu wajinga kweli. Halafu huyo utakuta ni kamanda, sasa hao polisi wa kawaida sijui watakuwa na akili ya namna gani!!
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23 katika jiji kuu la kibiashara, Dar es Salaam. Marufuku hiyo imetolewa kwa lengo la kudumisha amani na usalama wa wananchi.


Misime aliongeza kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakipanga mikakati ya kuchochea vurugu nchini, hali ambayo inaleta hatari kwa amani ya nchi. Alisema kuwa mara kadhaa serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini walipo wanachama waliodaiwa kupotea, lakini baadhi ya watu wanaendelea kutoa mipango inayolenga kuharibu amani.

Soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

"Kwanini wanataka kututoa kwenye reli hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia Suluhu kuagiza kufanyika kwa uchunguzi, mara kadhaa viongozi na wafuasi wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa mipango yenye lengo la leta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi yetu kwasababu zao wenyewe, kutokana na taarifa hiyo jeshi la polisi nchini limepiga marufuku kuacha kuendelea kuhamasisha kujihusisha katika uhalifu huo"
Mimi kwa vile ni mdau wa sheria na haki za binadamu sifurahishwi na matamko kama haya. Mbona hapo nyuma wamekuwa wakiandamana kwa amani na hawajafanya uhalifu wowote? I believe that the more people express their viewpoints, the more they relax (release tension,), and the more they are mazzled, the more they build up tension/anger. Je, si kuvunja Katiba?
 
Sisi wanatanga tunasema, Ali Mohamed Kibao asitumike kama turufu ya kisiasa. Serikali iwachwe huru ifanye uchunguzi wake.

Msioelewa; Ali Mohamed Kibao ni zaidi ya siasa, kishakua CCM, Kishakua CUF kishakua Chadema na pengine hivi karibuni angekua ni ACT.

Hajawahi kua na ugomvi na CCM wala CUF wala Chadema wala chama kingine chochote cha kisiasa.
Simba.
Arsis, anasemaje?
Marehemu alikuwa nani ?
Maandamano yawepo au yasiwepo kabisa ?
Na kwanini ?
Naomba mwulize atufafanulie 😅
 
Mimi kwa vile ni mdau wa sheria na haki za binadamu sifurahishwi na matamko kama haya. Mbona hapo nyuma wamekuwa wakiandamana kwa amani na hawajafanya uhalifu wowote? I believe that the more people express their viewpoints, the more they relax (release tension,), and the more they are mazzled, the more they build up tension/anger. Je, si kuvunja Katiba?
Naunga mkono hoja kuhusu haki ya kuandamana, ila kwa vile polisi ndio mwenye dhamana ya usalama, kama wamepokea taarifa za kiintelijensia kuhusu uwezekano wa vurugu, then nawashauri Chadema Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

P
 
Hao polisi wapewe tu hata kofia za ccm wawe wanavaa ijulikane moja tu kuwa wao ni wana ccm. Wanataka CDM inyamaze wakati wao ni watuhumiwa wa utekaji na upoteaji wa wanachama wake.
 

Attachments

  • 5793447-d05126d2cf760a954dec3168c92d63a7.mp4
    8 MB
Naunga mkono hoja kuhusu haki ya kuandamana, ila kwa vile polisi ndio mwenye dhamana ya usalama, kama wamepokea taarifa za kiintelijensia kuhusu uwezekano wa vurugu, then nawashauri Chadema Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

P
In my opinion, this appears to be an old song, and with the new leadership I thought its stanzas should have been improved to appreciate and affirm a new beginning which embraces 4Rs.
 
Kabla sijauliza swali naomba ni wapongeze police wetu. Wamegundua kuwa maandamano ya chadema ya tavulugha Amani. Hata kabla haya jafanyinka sasa naomba kuuliza ma swali mawili tu

1: Kwanini wasitumie hiyo interenensia iliyogundua maandamano ya chadema ya kuwa yataleta fujo kabla ya kufanyika kubaini watekaji kabla hawajateka watu?
2: Kwanini wasitumie hiyo interenensia kubaini wauwaji na watekaji wako wapi ili wawakamate? Interejensia ya police ina uwezo wa kubaini Fuji za maandamano tu

Aliye najibu anijuze
 
Tamko la hovyo, warudishe vijana wetu kwanza. Halafu Chadema waje na mkakati mwingine, maandamano hayajawahi kuwa suluhisho kwenye jambo lolote nchi hii,watu wataumia tu na bado mambo yatabaki vile vile.
Kwa nini unaishia tu kukosoa wazo la chadema bila kutoa wazo mbadala ?
 
Polisiccm bwana, kwenye maandamano hata wakisikia tu na si taarifa rasmi kwamba wamepelekewa. Harakaharaka wanakataza.
Watu wanatekwa mchana kweupe, wanauwawa hawaji haraka kuyaongelea na kutafuta ufumbuzi. Shida ni ccm kuingiza mifumo yote, kuwa ya kisiasa hatutaenda kokote mpaka Katiba mpya, wabanwe spana kwanza.
Wao mapolisi wakiongozwa na mafwele ndio wanaoteka na kuua raia wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom