Polisi yaruhusu maandamano ya Dr Slaa

Bobby,
Usijali sana huyu Mwiba ni mwenzetu katika hii crusade ya mikasa ya nchi yetu. Ila tu matumaini yake makubwa kawayaweka kwa Maalimu Seifu; sasa ukisema kinyume cha huyo yeye demokrasia humtoka!!

SLaa for presidency
 

Bravo Bobby, sasa hivi ni aibu sana kwa mtanzania kutaja utaifa wake kwa sababu ya mambo ya aibu yanayoendelea ndani ya nchi. Wana JF tumuunge mkono Dr Slaa kwa sababu ya ujasiri wake wa kupambana na MAFISADI walio ndani ya Serikali na wasio ndani ya Serikali.
 
Mbona Slaa is better than Kikwete ,Mkapa and Mwinyi ,the only problem for him to get to Ikulu ni mwamko mdogo na uelewa mdogo wa wapiga kura hasa wa vijijini !!!

Hawezi kwenda Ikulu kama hajaenda Jela ,wala hajakumbana na vipigo vya Sultani CCM.

hebu tuone Slaa akitumia maneno ya ghadhabu mbele ya vipaza sauti na kusababisha waandishi kutetemeka vidole wanapoandika habari zake, Wakuu jemedari wa Serikali ya Sultani CCM ni Seifu peke yake, bado hajatokea kwa Tanzania ya leo na kama mnataka mkutano unogele basi tumieni karata ya CUF Simba wa Nyika Maalim Seif Sharif Hamadi ,hata akina Slaa wanamjua na kumheshimu sana tu ,sasa nyie magabachori ikiwa mnamwona amepotea na hafai itakuwa ni woga ndio unaowahangaisha.
Mnajua kama mnataka kaseti ya kideo a mkutano wenu ifike Ikulu mpeni nusu saa huyo Mpemba muone itakavyouzika ,na siku hiyo mwambieni asichane nywele hapo itakuwa ni moto tu ,wengine wanasema kama halewi anavuta ila nimuonavyo ni mtu wa dini sana ,ila nimewahi kumuona kwenye mkutano ikiwa ameweka matuta kwenye nywele na kweli macho yameiva na ndipo hapo husema mpaka waandishi huacha kuandika na kushika tama kwa jamaa anavyomwaga mboga na ugali wa Chama tawala.
 
Mwiba,
Tuache ushabiki nani ni nani; lakini kweli Slaa kawasha moto; na sasa hivi kweli ni zamu ya upinzani kukaa chonjo na kuchukua nchi kama mkiacha ubishi kama unaotaka kuuleta. Tangu mwaka 1995 Maalifu Seifu kashindwa kuchukua madaraka; ok; sababu unazo wewe kuwa CCM wana mbinu; ok, Maalimu Seifu angetoa mbinu zake pia. Ameshindwa 1995/2000/2005; unafikiri ataweza lini?

Sasa hivi lazima akubali na mwenzie Lipumba au the like; kuwa; wapangane na kuunda coalition kama ile rainbow ya kenya; pale juu wamweke Slaa, wa pili awe Maalim, labda kidogo mambo yanaweza kubadilika. Halafu kwa sasa hivi coalition imechelewa kwa vijijini kule inabidi wawe na muda wa kuwajua hawa coalition, otherwise huyo Sultani unayesema kila siku atazidi kutawala.
 

Mkuu Bob hujamjua Mwiba, huyu Mwiba yeye ni CUF, Seif na Zanzibar tu. Hawezi kumuunga mkono yeyote zaidi ya hao watatu yaani chama CUF pekee, kiongozi Seif pekee na nchi Zanzibar no Muungano. kwa ujumla jamaa ni mbaguzi. Nawaunga mkono wananchi na CHADEMA wa Iringa kwa kuonyesha kwa vitendo support yao kwa Dr. Slaa na kupinga ufisadi na rushwa katika usambazaji na uuzaji wa mbolea. Watanzania wengine tuige na tusambaze ujumbe wa mabadiliko.
 
NO, NO, MWIBA SI MBAGUZI, NI MAPENZI YAKE TU NA CHAMA CHAKE, KUPENDA KWAKE SI UBAGUZI ILA DEMOKRASIA IMTUMAVYO!!

Slaa for Presidency!
 
Kama sio kuwa mbali na Iringa ningekuwapo katika maandamano hayo tena nikiwa na bango lisemalo NI WAKATI WA KUIZIKA SISI MIJIZI. Watu wa Iringa wamefanya kitu natamani watanzania wote tungefanya kila siku tena hata kama Polisi wanazuia sisi tunaweza kuwaonyesha nguvu ya umma.
Enyi wananchi wa Iringa mmeonyesha njia. Ni wakati wa sisi wengine kuendesha the same thing kwenye mikoa mingine ili kuongeza nguvu kwenye hoja ya shujaa Dr Slaa.
 
All the best Dr. Slaa. I'm sure Iringa residence will never let you down. We're together
 
Watu wa mikoani ndipo hapo huwa wana nipa raha, yaani wao ni vitendo kwa kwenda mbele.
DSM sijui maraha yanatuzidia, ama maisha ni magumu sana? uelewa mwingi taarifa zote za tunavo ibiwa tunazo kuliko hata wa mikoani ila haaa... tupo kama vile hatupo!

BRAVO WAKAZI WOTE WA IRINGA
Hili ni jambo la kuigwa na wazalendo wote wa Tanzania, ina bidi kuunga mkono wapambanaji, hata hao wanao jidai kumzomea Slaa bungeni labda waishi huko huko DODOMA wakirudi mitaani kwetu tunao nasi tuwazomee, Wamerikologa inabidi walinywe wabinafsi wakubwa watetea matumbo yao! badala ya wananchi walio watuma kha!
 
Bobby,
Usijali sana huyu Mwiba ni mwenzetu katika hii crusade ya mikasa ya nchi yetu. Ila tu matumaini yake makubwa kawayaweka kwa Maalimu Seifu; sasa ukisema kinyume cha huyo yeye demokrasia humtoka!!

SLaa for presidency

mzee umechemka sana kwa mwiba. fuatilia posting zake za mwanzo utaona kabisa kuwa huyu ni ccm damu kabisa na ni watu wanaotumiwa kwani ghafla akapiga u turn na kujifanya eti ni cuf ili tu kupenyeza mambo yake. Huyu anajua kabisa kuwa huku bara cuf haina nguvu ila anaitumia kuisaidia chama chake.

kama hauamini tafuta post za mwiba 1-100 za kwanza halafu utaniambia. Watu hawa humu wamo wengi tu wengine utawaona wakija na viabari mbuzi wakidai ni watetezi wa wanyonge kumbe wana ajenda zao. Leo namtaja mmoja tu Gembe na yeye ni kama mwiba tu hakuna tofauti ni watumishi wa mafia wakiongozwa na baba yao anayejuana na viongozi!
 
Kma itashindikana kuifanya hii iwe ajenda inayojitegemea, Chadema wanaweza kuiingiza kuwa sehemu ya operesheni sangara
 
Wapinzani wangeungana kwa nafasi ya urais asimame lipumba pekee labda itasaidiaaa....si kila kichama...kiwe kinataka kusimamisha rais tuuu
 
Ningekuwa jirani ningebeba bango kabisa!! Wizi hauwezi kuwa siri bana. Dr. Slaa you are our Hero, tunapigana sambamba katika vita hivi hauko peke yako.
 
Tumuunge mkono Mesimiwa Dr. Slaa, maana anachokifanya ni kwa ajili ya watanzania wote kama sio wengi, tusikamane sote kwa pamoja.

Karibu sana shemeji hapa JF ndo penyewe hapa.
Hivi punde nitakutambulisha kwa Masanilo.
Huko Zenji mnatunyima nini lakini.


Big up Dr.Slaa
 
Mwiba,
Inawezekana Seif ni mzungumzaji mzuri, lakini kama umesoma vizuri ajenda za maandamano kwa " mujibu wa barua ambayo waombaji wameiwasilisha kwa kamanda wa polisi maandamano hayo yanataka mishahara na maslahi ya viongozi wote wa umma wenye nyadhifa za kisiasa yajulikane kwa wananchi kama alivyosema Dr Slaa." Seif ni mmoja wa viongozi hao wanaopokea marupurupu ya uongozi wa kisiasa, ambayo bado ni siri na ndio moja ya sababu za msingi wa maandamano hayo. Hivyo basi pamoja na uzuri wake wa kuzungumza, lakini hilo sio jukwaa lake kwani naye ni mmoja wa watuhumiwa.
 
Kwa wale walioko Iringa mjini, tafadhali je kuna lolote ambalo twaweza lisikia kutoka kwenu kuhusiana na yaliyojiri kwenye maandamanoo na haswa hotuba ya mpiganaji Dr. Slaa?
 
Ulichosema Shaom ni kweli,especially kuhusu Mwiba,nadhani aliyeifufua ile thread yake ya 2007 kuwa hakuna chama mbadala ndiye amemuumbua zaidi.
 

Mkuu naona umeamua kuwapa za uso. Safi sana huu ni ufisadi pia
 
Walioko Iringa tunaweza kupata matangazo ya moja kwa moja?
 
Maandamano yalianza saa 4, yalifika uwanjani saa 5. Hotuba zimetolewa mpaka saa 9. sasa wamemaliza. Kwa maelezo zaidi mpigie Mchungaji Msigwa

serayamajimbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…