Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu sera,Maandamano yalianza saa 4, yalifika uwanjani saa 5. Hotuba zimetolewa mpaka saa 9. sasa wamemaliza. Kwa maelezo zaidi mpigie Mchungaji Msigwa
serayamajimbo
Hatimaye baada ya Polisi Mkoa wa Iringa kukataa kuruhusu maandamano ya Dr Slaa toka jana. Muda mfupi uliopita wameruhusu maandamano hayo yafanyike kesho jumamosi Mei 2, 2009 kuanzia saa 3 asubuhi. Maandamano hayo yataanzia uwanja wa Mwembetogwa.
Kwa mujibu wa barua ambayo waombaji wameiwasilisha kwa kamanda wa polisi maandamano hayo yanataka mishahara na maslahi ya viongozi wote wa umma wenye nyadhifa za kisiasa yajulikane kwa wananchi kama alivyosema Dr Slaa. Pia waandamanaji hao wanapinga nyaraka za wizi na ufisadi kuitwa za siri halali za serikali. Pamoja na mambo mengine wanalaani ufisadi na usimamizi mbovu katika mgawanyo wa mbolea ya ruzuku na kupanda kwa gharama ya pembejeo katika taifa hali inayoathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya wakulima. Mkoa wa Iringa ndipo ambapo kulitangazwa azimio la "Siasa ni kilimo" lenye lililolenga kuwakomboa watanzania ambalo watawala wa sasa wamelipuuza.
Katika tangazo lao, viongozi hao wameeleza pia kuwa mwisho wa maandamano hayo watanzania watakaoshiriki watasimama kwa ukimya kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu waliofariki katika milipuko ya mabovu katika mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Manispaa ya Iringa mjini Mchungaji Msigwa ambaue ni mmoja wa wajumbe katika kamati ya wananchi ya maandalizi ya maandamano hayo, ametoa mwito kwa wanachi wa Iringa kuhudhuria kwa wingi na kwa wale wenye kuhitaji maelezo zaidi wawasiliane nae kupitia namba yake ya mkononi 0754360996. Shime mtanzania, huu ni wakati wetu wa kuleta mabadiliko
Serayamajimbo
Bila shaka hata maaskari wenyewe nafikiri kwa upande mwingine wameyafurahi maana nafikiri kwa nafasi kubwa wao ni wahanga wa kile ambacho Mh Slaa anakitetea
Kijana hebu wacha kukurupuka ,Seif ni mstaafu (Waziri kiongozi wa Zanzibar na si waziri wa Chama ) ,tunapoambiwa tutenge uongozi wa Chama na Uongozi wa Serekali ,kwa maana unapotumikia Serikali unahesabika vingine ,hivyo Seif alisimamia kudai haki yake ya msingi (Mafao pamoja na ulinzi ) kama kiongozi wa Serikali. Au weka sawa Seifu anatuhumika vipi kwa hapa ? Ila kumbuka jiwe moja linaweza kupiga ndege wawili.Mwiba,
Inawezekana Seif ni mzungumzaji mzuri, lakini kama umesoma vizuri ajenda za maandamano kwa " mujibu wa barua ambayo waombaji wameiwasilisha kwa kamanda wa polisi maandamano hayo yanataka mishahara na maslahi ya viongozi wote wa umma wenye nyadhifa za kisiasa yajulikane kwa wananchi kama alivyosema Dr Slaa." Seif ni mmoja wa viongozi hao wanaopokea marupurupu ya uongozi wa kisiasa, ambayo bado ni siri na ndio moja ya sababu za msingi wa maandamano hayo. Hivyo basi pamoja na uzuri wake wa kuzungumza, lakini hilo sio jukwaa lake kwani naye ni mmoja wa watuhumiwa.
Hapana na inawezekana kabisa mnanielewa kivyenuvyenu aidha kwa uvivu mlionao wa kupambanua mambu kwa kina. Ni kweli kabisa kila kitu naipa uungaji mkono ZNZ kwa sababu ZNZ kuna ujasiri ambao bado waTanganyika hamjaufikia,kumbuka tu muamko mkubwa wa siasa za upinzani upo Zanzibar na hata maamuzi ya kufanya kweli yanapokelewa vilivyo na wananchi na kuyatekeleza hadi dakika ya mwisho ,ukiwa ni msimamo wa kutekeleza lile walilolikusudia ,viongozi wanaposema CCM asipewe kura hata moja basi ujue kweli CCM hataambulia kitu ambacho kinaweza kumpa ushindi wa che, Kwa upande wa wananchi wa Tanganyika bado unaweza kwenda nao sambamba katika harakati na kujiona (Upinzani) una wapiga kura wengi lakini mwishowe ukajikuta wananchi uliowategemea wanabadilika na kukuacha solemba ,ni ukweli usiopingika kuwa bado wananchi hawajakuwa wa kuaminiwa, Viongozi wa upinzani Zanzibar via CUF wanaamini kuwa hata wale wanaopewa dhamana ya kusimamia uchaguzi (mawakala wa vyama vya upinzani) bara nao ni rahisi kurubuniwa na Chama Tawala tofauti na wale mawakala wa Zanzibar ambao ni jino kwa jino ambao huiwacha CCM na njia mbadala ya kubadilisha last result kwenye utangazaji kitu ambacho hakina wakala isipokuwa ni mkuu wa tume.Mkuu Bob hujamjua Mwiba, huyu Mwiba yeye ni CUF, Seif na Zanzibar tu. Hawezi kumuunga mkono yeyote zaidi ya hao watatu yaani chama CUF pekee, kiongozi Seif pekee na nchi Zanzibar no Muungano. kwa ujumla jamaa ni mbaguzi. Nawaunga mkono wananchi na CHADEMA wa Iringa kwa kuonyesha kwa vitendo support yao kwa Dr. Slaa na kupinga ufisadi na rushwa katika usambazaji na uuzaji wa mbolea. Watanzania wengine tuige na tusambaze ujumbe wa mabadiliko.