Polisi yaruhusu maandamano ya Dr Slaa

Tafadhali mkuu, Unaweza kutupa kilichojiri mkuu? turn up, ujumbe na mapokeo?
 
Maandamano yalianza saa 4, yalifika uwanjani saa 5. Hotuba zimetolewa mpaka saa 9. sasa wamemaliza. Kwa maelezo zaidi mpigie Mchungaji Msigwa

serayamajimbo
Ndugu sera,
Tumwagie cheche zilizo temwa huko, mahudhurio yalikuwaje? si unajua hata huyo mchungaji si wote tunaweza mpata kwa cmu, tafadhali mkuu mwaga mambo hapa
 


Bila shaka hata maaskari wenyewe nafikiri kwa upande mwingine wameyafurahi maana nafikiri kwa nafasi kubwa wao ni wahanga wa kile ambacho Mh Slaa anakitetea
 
Bila shaka hata maaskari wenyewe nafikiri kwa upande mwingine wameyafurahi maana nafikiri kwa nafasi kubwa wao ni wahanga wa kile ambacho Mh Slaa anakitetea

Akili hiyo hawana. Wadogo kweli ni wahanga lakini ni watu wakufuata tu amri zinazotolewa na wakubwa wao ambao si wahanga.
Hiyo inakuwa hivi; IGP si mhanga, anamminya mkuu wa kanda ambaye naye si mhanga ambaye naye anamkandamiza mkuu wa polisi wa mkoa, naye si mhanga naye anamkandamiza mkuu wa polisi wa wilaya, si mhanga vile vile anamkandamiza mkuu wa kituo huyu ni mhanga anategemea rushwa kwa nafasi yake, kama kutoa dhamana, kuamua kesi iende mbele au asuruhishe hapa akishirikiana na mkuu wa upelelezi wa wilaya. Wengine wote chini ya mkuu wa kituo ni wahanga na wanategemewa kufuata amri sababu ya elimu ndogo na ufinyu wa mawazo ndio maana hawwwezi kutofautisha kati ya mtetezi wao na mnyonyaji.
 
Kijana hebu wacha kukurupuka ,Seif ni mstaafu (Waziri kiongozi wa Zanzibar na si waziri wa Chama ) ,tunapoambiwa tutenge uongozi wa Chama na Uongozi wa Serekali ,kwa maana unapotumikia Serikali unahesabika vingine ,hivyo Seif alisimamia kudai haki yake ya msingi (Mafao pamoja na ulinzi ) kama kiongozi wa Serikali. Au weka sawa Seifu anatuhumika vipi kwa hapa ? Ila kumbuka jiwe moja linaweza kupiga ndege wawili.
 
Mlioko huko Iringa, tupeni pia 'feedback' ya maandamano, tujue nini kilitokea huko. Hongereni sana!
 
Hapana na inawezekana kabisa mnanielewa kivyenuvyenu aidha kwa uvivu mlionao wa kupambanua mambu kwa kina. Ni kweli kabisa kila kitu naipa uungaji mkono ZNZ kwa sababu ZNZ kuna ujasiri ambao bado waTanganyika hamjaufikia,kumbuka tu muamko mkubwa wa siasa za upinzani upo Zanzibar na hata maamuzi ya kufanya kweli yanapokelewa vilivyo na wananchi na kuyatekeleza hadi dakika ya mwisho ,ukiwa ni msimamo wa kutekeleza lile walilolikusudia ,viongozi wanaposema CCM asipewe kura hata moja basi ujue kweli CCM hataambulia kitu ambacho kinaweza kumpa ushindi wa che, Kwa upande wa wananchi wa Tanganyika bado unaweza kwenda nao sambamba katika harakati na kujiona (Upinzani) una wapiga kura wengi lakini mwishowe ukajikuta wananchi uliowategemea wanabadilika na kukuacha solemba ,ni ukweli usiopingika kuwa bado wananchi hawajakuwa wa kuaminiwa, Viongozi wa upinzani Zanzibar via CUF wanaamini kuwa hata wale wanaopewa dhamana ya kusimamia uchaguzi (mawakala wa vyama vya upinzani) bara nao ni rahisi kurubuniwa na Chama Tawala tofauti na wale mawakala wa Zanzibar ambao ni jino kwa jino ambao huiwacha CCM na njia mbadala ya kubadilisha last result kwenye utangazaji kitu ambacho hakina wakala isipokuwa ni mkuu wa tume.

Hivyo upande wa bara kuna hitilafu kubwa sana ambayo inaviweka vyama vya upinzani katika wakati mgumu pamoja na harakati zao za kuushawishi umma ,bado pengo ni kubwa sana ukiingia katika hatua za mwisho ambazo ndio critical point za mapambano ,CUF imewasoma mawakala wa bara ambao imewaona wanakuwa wanapotea siku ya uchaguzi na kutoonekana katika nafasi walizo pangiwa na kutoa mwanya wa kubadilisha kuingiza matokeo feki.

Hivyo kusema ni mbaguzi hiyo ni haki yako kuniona hivyo, lakini ukweli Chadema bado hamjajipanga na wala hamjakumbana na hila za CCM ambazo zimekuwa zinasomwa na CUF kwa muda mrefu na kuzitafutia njia za kuziziba na kila siku ziendavyo CUF imekuwa ikifanikisha katika kuzibana njia hizo ambazo ni pamoja na kuwadhibiti mawakala wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…