Polisi yasema aliyevunja Kanisa Katoliki na kuharibu Vitu Geita ni Muumini aliyekuwa amelewa!

Polisi yasema aliyevunja Kanisa Katoliki na kuharibu Vitu Geita ni Muumini aliyekuwa amelewa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Polisi mkoani Geita wamesema uchunguzi wa awali unaonyesha aliyevunja Kanisa la Katoliki na kuharibu Vitu mbalimbali ni Muumini aliyekuwa amelewa

Uchunguzi unaendelea.

======

1677414935444-jpg.2530606

1677414922524-jpg.2530610
Pia soma: Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023

Source Star tv
 
Polisi mkoani Geita wamesema uchunguzi wa awali unaonyesha aliyevunja Kanisa la Katoliki na kuharibu Vitu mbalimbali ni Muumini aliyekuwa amelewa

Uchunguzi unaendelea

Source Star tv
Muumini ninja huyo hongereni polisi Kwa ngonjera tamu
 
Muumini ninja huyo hongereni polisi Kwa ngonjera tamu
Umeita ngonjera kwasababu kama vile jibu halijakufurahisha! Yaani watu wamefanya uharibifu kama huo bado pia ulitaka uambiwe ni flani ili ufurahi?

Sasa wewe na aliefanya huo uharibifu nani muharibifu zaidi? Maana umeambiwa ni mlevi hujajaridhika ulitaka uambiwe ni Masawe ili chuki iwepo baina ya waroma na Masawe?

Kama unasali kwa hiyo imani yako basi acha hizo habari
 
Kwanza kanisa limejengwa kwa sadaka yangu.......alisikika yule mlevi
 
wakiristo na pombe ni damdam.hadikanisani wakikaa vikaovyao kanisani siku ambazo sio za ibada wakimaliza wana shusha gambe mezani😅😅
 
Geita kwa matukio ya ajabu ajabu kwasasa wanaongoza naona wale ndugu zetu wa Mara wamewaachia usukani wana Geita
 
Huyo muumini mlevi atakua ameudhiwa kwa kiasi kikubwa na hilo kanisa, hapo alikua analipa kisasi tu.

Lakini bado haiingii akilini mlevi aweze kufanya vile, labda kuna mengine nyuma ya pazia
 
Kuna zaidi ya ulevi...! Mapadre na wasaidizi wote wa Askofu wahojiwe.

Nyamizi njoo huku uone muumini mlevi kavunja mlango akaingia ndani ya kanisa na kuharibu mapambo na vifaa vya kanisa...!
 
Back
Top Bottom