Polisi yasema inamshikilia msaidizi wa Membe Jerome Luanda, anatuhumiwa kwa kosa la kutakatisha fedha

Ndio tunamsubiria bosi wa ACT, mate yatutiririka kwa uchu wa udaku hapa
Kwa taarifa yako tu.

Membe ni mtaalamu katika fani ya kuwaangusha watu wanaomshabikia.

Anaweza kutangaza atamwaga mboga, mkajazana hapo kumsikiliza, akawaambia ile mboga tumeipiga picha, picha zinasafishwa kwanza iwepo kumbukumbu kabla ya kuimwaga, nitawajulisha maendeleo zaidi.

Halafu mnabaki na msawali, digital camera zote mpaka kwenye simu Mzee Baba bado anasafisha picha mpaka leo?
 
Kwa taarifa yako tu.

Membe ni mtaalamu katika fani ya kuwaangusha watu wanaomshabikia.

Anaweza kutangaza atamwaga mboga, mkajazana hapo kumsikiliza, akawaambia ile mboga tumeipiga picha, picha zinasafishwa kwanza iwepo kumbukumbu kabla ya kuimwaga, nitawajulisha maendeleo zaidi.
Katoa mkwara kabla ya masaa 12 wawe wameishamuachia watekaji, na kweli wametoa taarifa kuwa watekaji ni polisi tumewajua. Na sasa tumejua kuwa hawa ndio wasiojulikana, tunasubiria watuambie wamemteka kwa sababu gani.
 
BREAKING NEWS : Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema msaidizi wa @BenMembe Jerome Luanda yuko mikononi mwa polisi na ni mzima wa afya hivyo wanaodai ametekwa ni waongo...
YES!
 
Katoa mkwara kabla ya masaa 12 wawe wameishamuachia watekaji, na kweli wametoa taarifa kuwa watekaji ni polisi tumewajua. Na sasa tumejua kuwa hawa ndio wasiojulikana, tunasubiria watuambie wamemteka kwa sababu gani.
Wamemuachia?
 
Duuh kwani angemfanyaje zaidi labda ya kulalamika tu kwenye media maana huwa najaribu kuimagine mikwara mama hiyo utekelezaji wake unakuwaje nashindwa kuelewa.
unaelewa nini huoni mkwara umetekelezwa c wangesubiri huo muda chezea Membe wewe
 
BREAKING NEWS : Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema msaidizi wa @BenMembe Jerome Luanda yuko mikononi mwa polisi na ni mzima wa afya hivyo wanaodai ametekwa ni waongo.

====

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, leo Septemba 17, 2020, amesema msaidizi wa Mgomba Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe, aitwaye Jerome Luanda, yuko mikononi mwa polisi akiwa ni mzima wa afya na hakutekwa.

Amesema hayo akiwa anazungumza na East African Radio ya jijini Dar es Saalam, ambapo amethibitisha msaidizi huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na akakanusha habari za kutekwa.

“Huo ni uongo na uzushi; tumemkamata akiwa airport pale Julius Nyerere, nasikia wengine wanasema wamemtafuta vituo vyote hawajamuona. Ni uongo, sisi tupo naye na ni mzima wa afya, tunamshikilia kutokana na kesi zake ambazo hatuwezi kuzitaja,” amesema na kuongeza:

“Na huyu nasema amekamatwa, anatuhumiwa kwa kosa la kutakatisha fedha, kwa hiyo anayetaka kuthibitisha hilo ni suala la kuja tumueleze ukweli wa jambo hilo.”

Tukio hilo limejiri baada ya Mgombea Urais huyo, kuandika katika ukurasa wake wa Twitter Septemba 16, 2020, kuwa msaidizi wake amechukuliwa na watu wasiojulikana, na hivyo akatoa masaa kadhaa ili awe amepatikana.

Pia Soma > News Alert: - Bernard Membe ataka Msaidizi wake Jerome Luanda aliyetekwa arudishwe bila Mchubuko, vinginevyo watafikishana Mbali, hela za Kampeni zatajwa

KUNA WATU HUWA WANAJAMBA MAVI,KABLA HAJAANZA KUNUKA, WANAPULIZIA PAFYUME. UMETEKA BAADA YA KUBAINIKA, UNAJIFANYA UNAMSHIKILIA 🤣🤣🤣
 
Sasa mbona hawajasema wamemshikilia kituo gani?
 
Ni wazi kuwa huyo msaidizi wa Membe, Jerome Luanda, alitekwa na hakuwa wa kwanza kutekwa kwani wametekwa wengi katika awamu hii ya tano. Mwandishi Azori Gwanda naye alitekwa hivyo hiyvo kama alivyotekwa Jerome Luanda ila tofauti ni kwamba waliodaiwa kumteka kwa namna moja au nyingine hawakujitokeza kwa sababu hakuna aliyethubutu na kuwa tayari kuwaumbua. Safari hii watekaji imebidi wajitokeze kwa sababu ya mkwara waliowekewa na Membe mwenyewe wa kuwataja hadharani.

Hii imenikumbusha jinsi waliotaka kumteka yule mura wa Tarime ilivyobidi haraka haraka wajitambulishe ili wajiokoe na pigo ambalo lingewakuta kama hawakufanya hivyo. Afande Mambosasa amejikuta hana namna bali kujitokeza haraha haraka na kuokoa jahazi la wasiojulikana ambao kwa miaka mitano wameteka, wametesa na wamepoteza kama ilivyotokea kwa Azory Gwanda. Hatimaye wingu zito lililokuwa limewafunika wasiojulikana limeondolewa na kwa mara ya kwanza tunawaona kwa sura zao halisi.
 
Kujitokeza na kukiri kumteka sasa hatopotea sababu tumewajua wasiojulikana
Hujajibu swali nililokuuliza na ulilojibu sijakuuliza.

Membe alisema wamuachie, la sivyo...

Wamemuachia?
 
  • Kicheko
Reactions: Dua
Back
Top Bottom