Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
JESHI la Polisi mkoani Tabora limewatia mbaroni watu wawili kwa tuhuma za kuhujumu miradi ya maji ukiwamo wa Ziwa Victoria kwenda mkoani humo katika operesheni iliyofanywa na jeshi hilo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoani wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa, alitaja waliokamatwa kuwa ni Creti Mabula (20), mkazi wa mtaa wa elimu wilayani Igunga na wenzake wanne.
Alisema Mabula na wenzake walikamatwa wakiwa na mali za wizi zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. milioni 57.6.
Alifafanua kuwa vifaa hivyo vyote vinamilikiwa na Kampuni ya Wachina ya Afcons-SMC JVC REF inayotekeleza mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tabora unaofadhiliwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya Sh. bilioni 600.
Vile vile, Kamanda alisema kuwa Jeshi la Polisi limemkamata Thomas Katoro (38), mkazi wa Nzega na wenzake watatu kwa kukutwa na pampu kubwa ya kuvuta maji mali ya halmashauri ya wilaya hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 32.
Alisema baada ya kuhojiwa na polisi, watuhumiwa walikiri kuiba pampu hiyo na kwenda kuiuza mkoani Shinyanga huku wakieleza kuwa waliifungua kutoka kwenye mradi ilipokuwa imefungwa.
Pia, alisema watuhumiwa hao tayari wamefikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi wa miundombinu ya miradi ya maendeleo.
Alionya vitendo vya wizi au uhalifu wa namna yoyote wa mali ya umma ikiwamo miundombinu ya miradi ya maendeleo havitafumbiwa macho na kwamba Jeshi la Polisi limejipanga vizuri na yeyote atakayebainika atashughulikiwa.
Kadhalika katika tukio lingine jeshi hilo limemkamata Ramadhan Juma (65), mkazi wa Ndekeli, wilaya ya Nzega akiwa na silaha aina ya shotgun yenye namba za usajili TZCRA 36462 na risasi nne za shotgun, alizohifadhi ndani ya nyumba yake.
Kamanda Mwakalukwa alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akiiazimisha kwa wahalifu ambao walikuwa wakiitumia katika matukio mbalimbali ya kihalifu likiwamo la unyang’anyi wa kutumia silaha lililotokea katika kijiji hicho.
Nipashe