Polisi yatoa siku 60 kwa wamiliki wenye silaha haramu kuzisalimisha

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza msamaha wa miezi miwili kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, ambapo watalindwa dhidi ya mashitaka endapo watasalimisha silaha hizo kwa hiari kuanzia Septemba 1 hadi Oktoba 31, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 1, 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, DCP David Misime, msamaha huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 66 cha Sheria ya Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015, Sura ya 223 na marejeo ya mwaka 2023.

“Serikali imetoa msamaha wa kutoshitakiwa kwa wamiliki wa silaha kinyume cha sheria endapo watasalimisha silaha haramu kwa hiari kuanzia tarehe 01/09/2025 hadi 31/10/2025, kama ulivyotangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 537 la tarehe 29/8/2025,” imeeleza taarifa hiyo.

Jeshi la Polisi limefafanua kuwa usalimishaji utafanyika nchi nzima, katika vituo vya Polisi, ofisi za Serikali za Mitaa, au kwa watendaji wa kata na shehia kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.

Msemaji wa Polisi ameongeza kuwa, yeyote atakayesalimisha silaha ndani ya kipindi cha msamaha “hatachukuliwa hatua zozote za kisheria”, lakini akatahadharisha kuwa, “mtu yeyote atakayepatikana na silaha baada ya kipindi cha msamaha atakamatwa na kuchukuliwa hatua zingine za kisheria.”

Msamaha huo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuhusu udhibiti wa silaha ndogo na nyepesi, ambayo yameeleza kuwa uzagaaji wa silaha haramu umeendelea kusababisha uvunjifu wa amani, vifo, majeruhi na hofu kwa wananchi.

Jeshi la Polisi pia limezitaka kampuni binafsi za ulinzi ambazo zimekuwa zikikodisha au kuazimisha silaha kinyume cha sheria kusitisha mara moja tabia hiyo na kuhakikisha silaha zinazotumika kiholela zinarudishwa kwa wamiliki au kusalimishwa katika kipindi hiki cha msamaha.

Aidha, wananchi ambao ndugu zao walimiliki silaha kihalali lakini wamefariki wametakiwa kuzisalimisha silaha hizo kulingana na masharti yaliyotolewa.
1756698730899.png

1756698753063.png
 
Nipeleke ili wanishike.. eeh 👽👽

Nitabaki nalo tuu

Janjaa ya nyani hiyoo.. lazima uhojiwe limetoka wapi, mwisho wa kuunganishe na mauaji
 
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetangaza msamaha wa kutoshitakiwa kwa wamiliki wa silaha haramu watakaosalimisha silaha kwa hiyari kuanzia leo Septemba 1, 2025 hadi Oktoba 31, 2025.

Msamaha huo umetolewa chini ya mamlaka ya Kifungu cha 66 cha Sheria ya Udhibiti wa Silaha na Risasi ya mwaka 2015, Sura ya 223 na marejeo ya mwaka 2023, kupitia Tangazo la Serikali Na. 537 la Agosti 29, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, iliyotolewa leo Jumatatu, Septemba 1, 2025, hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya kimataifa na kikanda kuhusu udhibiti wa silaha ndogo na nyepesi, ambazo mara nyingi zimekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani, hofu, majeruhi na vifo.

“Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, inatekeleza maazimio ya mikutano ya kimataifa ikiwemo ule wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa wa Julai 2018 na ule wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia, Julai 2017, ambapo ilikubaliwa Septemba iwe mwezi wa usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari hadi mwaka 2030.

“Kwa mujibu wa masharti ya msamaha huu, usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari utafanyika nchi nzima kuanzia leo Septemba 1 hadi Oktoba 31, 2025. Silaha zitakazokabidhiwa zitasalimishwa katika kituo chochote cha Polisi nchini, Ofisi ya Serikali za Mitaa au kwa Mtendaji Kata/Shehia kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Imeongeza kuwa mtu yeyote atakayesalimisha silaha katika kipindi tajwa hatowajibishwa kwa hatua zozote za kisheria, lakini yeyote atakayekutwa na silaha baada ya muda wa msamaha kumalizika atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.
 
Na utekaji huu unaoendelea unarudishaje zana za ulinzi...landa kama una uwehu....huu ndo wakati wa kufunga nayo ndoa...😄
 
Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza msamaha wa miezi miwili kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, ambapo watalindwa dhidi ya mashitaka endapo watasalimisha silaha hizo kwa hiari kuanzia Septemba 1 hadi Oktoba 31, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 1, 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, DCP David Misime, msamaha huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 66 cha Sheria ya Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015, Sura ya 223 na marejeo ya mwaka 2023.

“Serikali imetoa msamaha wa kutoshitakiwa kwa wamiliki wa silaha kinyume cha sheria endapo watasalimisha silaha haramu kwa hiari kuanzia tarehe 01/09/2025 hadi 31/10/2025, kama ulivyotangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 537 la tarehe 29/8/2025,” imeeleza taarifa hiyo.

Jeshi la Polisi limefafanua kuwa usalimishaji utafanyika nchi nzima, katika vituo vya Polisi, ofisi za Serikali za Mitaa, au kwa watendaji wa kata na shehia kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.

Msemaji wa Polisi ameongeza kuwa, yeyote atakayesalimisha silaha ndani ya kipindi cha msamaha “hatachukuliwa hatua zozote za kisheria”, lakini akatahadharisha kuwa, “mtu yeyote atakayepatikana na silaha baada ya kipindi cha msamaha atakamatwa na kuchukuliwa hatua zingine za kisheria.”

Msamaha huo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuhusu udhibiti wa silaha ndogo na nyepesi, ambayo yameeleza kuwa uzagaaji wa silaha haramu umeendelea kusababisha uvunjifu wa amani, vifo, majeruhi na hofu kwa wananchi.

Jeshi la Polisi pia limezitaka kampuni binafsi za ulinzi ambazo zimekuwa zikikodisha au kuazimisha silaha kinyume cha sheria kusitisha mara moja tabia hiyo na kuhakikisha silaha zinazotumika kiholela zinarudishwa kwa wamiliki au kusalimishwa katika kipindi hiki cha msamaha.

Aidha, wananchi ambao ndugu zao walimiliki silaha kihalali lakini wamefariki wametakiwa kuzisalimisha silaha hizo kulingana na masharti yaliyotolewa.
Silaha zilizotajwa na Mange kupita bandarini zitarudishwa ughaibuni?
 
Back
Top Bottom