Polisi yatoa tahadhari, baadhi ya mawakala wanaosajili laini mtaani ni matapeli

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP David Misime

Akitoa darasa kwa Maafisa Polisi Jamii na Polisi Kata kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam pamoja na wengine kutoka Kibaha na Mkuranga, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP David Misime amezungumzia utapeli wa mitandao unaofanyika maeneo mbalimbali Nchini.

Akitoa elimu hiyo katika mafunzo hayo ambayo yamefanyika Dar es Salaam, Machi 21, 2023, SACP Misime amesema: “Kuna kipindi zile SMS za ‘Tuma kwenye namba hii’ zilikuwa nyingi, lakini baada ya Serikali kuboresha mifumo, matapeli wamekuja na njia nyingine

“Kuna baadhi ya watu wanazunguka katika mitaa wakijinasibu kuwa wanasajili laini za simu kumbe wao ni matapeli, wapo ambao ni halali wanafanya kazi hiyo ya Uwakala.

“Kwa wale matapeli wao wanacholenga ni kukuibia fedha zako katika akaunti za benki au zilizopo kwenye simu, wanasema wanao uwezo wa kukuongezea simu yako kuwa na internet yenye kasi, kukuunganisha katika vifurishi vya chuo, kusajili laini mpya au kurejesha laini zilizopotea.

“Je, mwananchi anawezaje kutofautisha matapeli na wale ambao ni mawakala halali wa mitandao ya simu? Ukiona mtu anakwambia toa laini yako ya simu na iweke katika simu yake ili akuunganishe katika hizo huduma alizokwambia, basi jua huyo ni tapeli.

“Akishaweka hiyo laini kwenye simu yake kunakuwa na ‘App’ ambayo inadukua taarifa zako, hata anapokwambia ingiza namba yako ya simu yeye akiwa amegeukia pembeni, inakuwa haina faida kwa kuwa anaweza kukuibia kwa kumbukumbu zako kubaki katika simu.


“Pia anapokwambia nunua muda wa maongezi au hamisha fedha zako kutoka kwenye simu huyo ni tapeli, mawakala halali wanafuata mfumo na hawawezi kumuuliza mteja kutoa taarifa kama hizo.

“Kingine unapoenda katika ATM usikubali kumpa mtu kadi yako au neno lako la siri ili akusaidie, hali hii hasa inawakuta wastaafu, lakini ni angalizo kwa watu wote kuwa makini, unapokutana na mtu wa aina hiyo unatakiwa kutoa taarifa Polisi.

“Ameongeza kuwa tayari kuna watu kadhaa wameshikiliwa wakituhumiwa kufanya utapeli wa aina hiyo na Jeshi la Polisi linaendelea na msako kwa kuwa mtandao ni mkubwa na upo maeneo tofauti."
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…