Polisi yatoa ufafanuzi kuhusu kusambaa kwa picha ya Askari akiwa na pesa zinazodhaniwa kuwa za Rushwa

Polisi yatoa ufafanuzi kuhusu kusambaa kwa picha ya Askari akiwa na pesa zinazodhaniwa kuwa za Rushwa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Jeshi la polisi kuchukua hatua kali iwapo ushahidi utaonesha askari wake alichukua rushwa.

IMG_20220120_095401_680.jpg



Kuona picha hizo soma >>Kila Mtanzania ale usawa wa Kamba yake. Trafiki akamatwa kwa rushwa
 
Labda alikuwa anakusanya mchango wa msiba
Mbona kesi hiyo anaitusua mapema tu akitulia!

Hao mashahidi wakiitwa au wakiambiwa waje hawatotokea

Wamwachie tu huyo afande aendele kupiga kazi

Ova
 
kwani PGO inasemajeee pale askari ashikapo burungutu la fedha mkononi ama kuonekana kwa gari ili hali yeye ni trafic police?
 
mbona barua yenyewe haijakidhi walichotaman kukisema! huyo askari kaoneka na ofsa wake labda ndiye aliyemkamata! sasa maelezo hayaeleweki kwa barua
Yaani taarifa ya ufafanuzi ndio inaleta utata mkubwa kuliko picha zenyewe. Imeandikwa bila kufafanua chochote!!! Imeandikwa Kikanjanja
 
Hapo kaka afande atajitetea kua alitoka kuvunja kibubu ili akalipe ada ya watoto.
 
Kawaida yao hao, kwani kwenye ile ajali iliyotokea maeneo ya Mkata sijua pale kati ya mabasi ya polisi na lori la kokoto si tuliambiwa dereva wa lori ndo mwenye makosa alikuwa anaovateki wakati picha zinaonyesha kila kitu!!!
 
Mbona hela zenyewe ata sio nyingi
Mleta mada unalijua burungutu la fwedha wewe[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom