Polisi yatoa ufafanuzi kuhusu kusambaa kwa picha ya Askari akiwa na pesa zinazodhaniwa kuwa za Rushwa

Polisi yatoa ufafanuzi kuhusu kusambaa kwa picha ya Askari akiwa na pesa zinazodhaniwa kuwa za Rushwa

Hakuna kesi hapo

F056D842-278C-4915-932E-CFF989E1B0EA.jpeg
 
Mbona kwenye maelezo ya polisi Hakuna au hamkutaja kiasi cha fedha zilizokutwa kwenye Siti ya gari?
Pili ni Lini Atakuwa mahakamani?
Tatu, ni nani atakuwa mchunguzi wa hii kesi?
TAKUKURU Mbona hawajaongea chochote?
Kwanini jeshi la polisi halijakiri ?

View attachment 2089094

View attachment 2089095
Kwa kiasi Hicho cha pesa wanamuonea BURE tu Hapo haizidi laki,, au Inaonekana Ana bifu na mtu
 
Ukiwa askari polisi hasa wa barabarani LAZIMA ule rushwa (ukusanye mapato) la sivyo ukalinde kwa mkuu wa mkoa/wilaya
 
Hapo sio nyingi koz hizo ndio alizokutwa nazo,, hapo nyuma hatujui kakusanya sh ngapi
 

Ushauri wa bure kwa IGP:-​

1. Polisi wote washonewe uniform ambazo hazina mifuko kama polisi wa Kenya.​

2. Polisi wasiruhusiwe kutumia magari binafsi kwenda kwenye shughuli Za kipolisi barabarani.
3. Yatengwe maeneo ambayo polisi watakuwa barabarani na maeneo hayo ziwekwe CCTV camera.
 
Hao wapiga picha wamempiga picha mlokole.
Yaani rahisi tu unakubali kupigwa picha au kukamatwa Mimi pangechimbika ardhi Ingekuwa chekundu inakuaje unakubali kukamatwa na kupigwa picha na mamlaka nyingine kizembe zembe tu utafikiri ndondocha,kama ni mbwai iwe mbwaika.Bora kesi juu ya kesi kuliko kesi.
 

Ushauri wa bure kwa IGP:-​

1. Polisi wote washonewe uniform ambazo hazina mifuko kama polisi wa Kenya.​

2. Polisi wasiruhusiwe kutumia magari binafsi kwenda kwenye shughuli Za kipolisi barabarani.
3. Yatengwe maeneo ambayo polisi watakuwa barabarani na maeneo hayo ziwekwe CCTV camera.
Elewa lakini police wakifata sheria Hakuna gari litakalo tembea barabarani huu ndo ukweli,magari mengi ni mabovu hayatakiwi yawepo barabarani.
Ni huruma ya police tu ndo maana yapo barabarani.

Jibu mtii sheria mkifata sheria rushwa zitakuwa likizo.

Hivi kwa akili yako unadhani kuna mfumo unaoweza mdhibiti mwenye njaa asipige nchi hii ya wapigaji kuanzia juu hadi chini.

Hizo cctv camera hao askari ni robot yaani wakae palipo na cctv au nazo zitakuwa zinahama maana hawakai sehemu moja wakiona tu pesa haziingii wanahama wanajua tayari madereva washapeana signals.

Kubandua mifuko sio ishu atawekwa hata muuza miwa barabarani.au kwenye vigogo,magunia.
Labda unaishi nje uwajui waswahili wewe.
 
Labda alikuwa anakusanya mchango wa msiba
Mbona kesi hiyo anaitusua mapema tu akitulia!

Hao mashahidi wakiitwa au wakiambiwa waje hawatotokea

Wamwachie tu huyo afande aendele kupiga kazi

Ova
Kwa nchi yenye watu wenye akili , hiyo kesi hawezi kushinda ila kwakuwa ni Tz, sioni ajabu!!
 
KILA mtza anakula kulingana na urefu wa kamba yake hii imeruhusiwa ukusikia hata majuzi.
 
Hapo kaka afande atajitetea kua alitoka kuvunja kibubu ili akalipe ada ya watoto.
Kibubu ukivunjie kwenye siti ya gari?
Badala ya kukivunjia nyumbani.
[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Tunatekeleza kwa vitendo kauli ya Mheshimiwa-tunakula kwa urefu wa kamba
 
Mbona kwenye maelezo ya polisi Hakuna au hamkutaja kiasi cha fedha zilizokutwa kwenye Siti ya gari?
Pili ni Lini Atakuwa mahakamani?
Tatu, ni nani atakuwa mchunguzi wa hii kesi?
TAKUKURU Mbona hawajaongea chochote?
Kwanini jeshi la polisi halijakiri ?

View attachment 2089094

View attachment 2089095
Madhaifu katika tukio hili;
Hilo gari unaloona noti zimewekwa kwenye kiti ni la Afisa mmoja wa TAKUKURU.
Hakuna aliyelalamika isipokuwa TAKUKURU wamemkamata na noti na kumpekua wenyewe.
Hakuna shahidi anayeshuhudia upokeaji wa noti hizo kwa mtuhumiwa ila ghafla tu tunashitukia anapakua noti kuweka kwenye kiti cha gari la TAKUKURU.
Kama kesi hii itapata mafanikio mahakamani basi nitaamini huyo Polisi ni Zuzu.
 
Back
Top Bottom